Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, January 29, 2019

Maandalizi ya Mkutano Wa Wakuu Wa Nchi Wa EAC Yaanza Jijini Arusha

adv1
Mkutano wa dharura wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umeanza jijini Arusha nchini Tanzania ukihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi zote sita wanachama ambao utahitimishwa na mkutano wa wakuu wa EAC, Februari Mosi, 2019.

Mkutano huo wa siku tatu unawakutanisha maofisa waandamizi kutoka nchi hizo kisha utafuatiwa na makatibu wakuu na mawaziri wa wizara za kisekta zinahusika moja kwa moja na Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Taarifa ya EAC iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Jumatatu Januari 28, 2019 imesema mkutano huo wa 38 wa Baraza la Mawaziri ni maandalizi ya mkutano wa 20 wa wakuu wa nchi za EAC ambao uliahirishwa mara mbili kutokana na kukosa akidi.

Miongoni mwa ajenda katika mkutano huo wa mawaziri ni ukamilishaji wa maamuzi ya vikao vya mawaziri, hoja kuhusu ofisi ya katibu mkuu, ripoti kuhusu  mipango ya miundombinu, uzalishaji na huduma za jamii, hali ya kisiasa, forodha na biashara, utawala na fedha pamoja hoja kuhusu taasisi za EAC.

Katika hatua nyingine wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za EAC ajenda kuhusu mgogoro wa kisiasa kati ya nchi za Rwanda na Burundi imepewa kipaumbele ikikumbukwa kuwa mkutano wa Novemba 30, 2018 ulishindwa kufanyika kutokana na Burundi kususia mkutano huo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )