Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 14, 2019

Mbunge CHADEMA Ampigia Promo ya Urais Tundu Lissu

adv1
Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Jesca Kishoa amesema zawadi pekee ambayo Watanzania wanaweza kumpa mbunge wa chama hicho jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu ni kumuunga mkono katika ndoto zake za kugombea urais mwaka 2020.

Kishoa ametoa kauli hiyo leo Januari 14, 2019 katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali kuhusu afya na maendeleo ya Lissu.

“Lissu ni kaka yangu, ni mbunge mwenzangu na kiongozi wangu, mambo ya kuangalia ni kupata baraka za chama lakini anafaa,” amesema Kishoa.

Amesema wakati ukifika atatamani kuona jina la Lissu likipitishwa kuwania urais, kwa kuwa Watanzania wanajua msimamo wa kiongozi huyo na ndio anayefaa kuwaongoza.

Lissu kwa sasa anaendelea na ziara yake kwenye nchi za Ulaya na marekani kwa ajili ya kuelezea mkasa wa kupigwa risasi uliompata Septemba 2017 Jijini Dodoma.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )