Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 23, 2019

Mchungaji Amani Lyimo wa KKKT Amuomba Rais Magufuli Aawache Watu Wazungumze Kwa Uhuru

adv1
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Amani Lyimo amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwaachia uhuru wananchi wazungumzie inapowezekana kwa sababu hiyo ndiyo demokrasia.

Mchungaji Lyimo amesema hayo leo Jumatano Januari 23, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam katika kikao kati ya Rais Magufuli na viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini.

“Rais tuliyekuwa tunamuomba ni wewe, nimeanza kukuombea tangu ukiwa Waziri wa Ujenzi na leo umekuwa Rais bado nakuombea na tunawaza 2025 baada yako itakuwaje, maana tunahitaji Kiongozi kama wewe.

“Mheshimiwa Rais Magufuli, suala la Demokrasia ni muhimu, watu wana hofu hata kama huambiwi na watendaji wako, kama kazi baba unapiga kweli wewe waachie wazungumze maana Watanzania hawatachagua maneno bali watachagua kazi, wape uhuru waseme." 
– Amesema Mchungaji Amani Lyimo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )