Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.

adv1
Katika kuhakikisha Nchi inakwenda na kauli mbiu ya hapa kazi tu na kuendanana na kasi ya Rais John Magufuli katika uwajibikaji hasa kwenye sekta ya Anga, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimezindua Kozi ya wahudumu wa ndani ya ndege ili kuhakikisha uwekezaji wa ndege nchini unaendana na Rasilimali watu wenye ujuzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha NIT jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kuwepo kwa kozi hiyo, kutasaidia kupata wajuzi wazawa wengi na kuacha kutoa wahudumu wa ndege nje ya maji.

“Kozi hii itasaidia sana, sasa hatuwezi kutoa wahudumu wa ndege nje ya nchi, na nitahakikisha hawa waliofundishwa wanafanya kazi ATCL” alisema mhandisi Kamwele

Mhandisi Kamwelwe alisema upatikanaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga utasaidia sana kuhakikisha tunakuza uchumi wa ndani na kupunguza changamoto ya kutokuwepo kwa rasilimali ambayo ilikuwa ukipelekea watu wengi kusoma nje ya nchi au kuhitajika kwa watu wa nje ya nchi ambao wanalipwa fedha nyingi.

Ameongeza kuwa uchumi wa viwanda unategemea zaidi, usafiri wa anga katika usafirishaji wa bidhaa katika masoko ya nje kwa haraka zaidi.

Alisema anaamini kuwa wataalamu mbalimbali wakiwemo wahandisi wa masuala ya ndege wanaofundishwa katika chuo cha NIT wanaujuzi wa kutosha wa kuweza kutengeneza ndege zetu sita ikiwemo iliyoingia  nchini hivyo- amewataka kuhakiksha wanaitumia KIA kuonyesha ujuzi huo.

Aidha Ameongeza, serikali inaendelea kununua ndege hivyo wahudumu wa ndege hawawezi kuwatoa nje ya Tanzania bali itawaajiri wale wote waliopata mafunzo ya kozi hiyo katika chuo cha NIT.

Amesema lengo la kuboresha elimu inayotolewa katika chuo cha NIT, Serikali kupitia wizara yake imeshakamilisha mazungumzo ya kupata fedha kutoka Benki ya Dunia na Serikali ya China kwa ajili ya kuboresha miundombinu, kukarabati kalakana na ununuzi wa vifaa vya kufundishia katika chuo hicho.

Aidha Mhandisi Kamwelwea amewataka NIT kuendelea kubuni zaidi katika kuzalisha Rasilimali watu wa kuweza kuhudumia ndege zetu na kuacha kutegemea rasilimali inayotoka nje ya nchi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )