Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Panga pangua ya Takukuru yawakumba maofisa 40.....Wamo wakurugenzi, wakuu wa kanda

adv1
Hatimaye  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Diwani Athuman ameanza kutekeleza agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuifumua na kuisuka upya taaasisi hiyo

Taasisi hiyo imefanya mabadiliko ya watumishi 40, wakiwamo wakurugenzi, wakurugenzi wa kanda, wakuu wa Takukuru wa mikoa, wakuu wa vitengo na sehemu ya makao makuu.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo, baada ya kumwapisha Diwani Ikulu Dar es  Salaam Septemba 18, mwaka jana .

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya  Dar es Salaam jana na Ofisa Uhusiano wa taasisi hiyo, Doreen Kapwani ilisema uhamisho huo umehusisha watumishi hao kwenda idara nyingine za Serikali.

Taarifa hiyo, iliwataja wakurugenzi waliohamishwa, kuwa  ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Alex Mfungo, Mkurugenzi wa Upelelezi, Mbengwa Kasomambuto na aliyekuwa Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Ekwabi Mujungu

“Taarifa hii inatolewa kutokana na  maswali yaliyowasilishwa kwetu kutoka vyanzo mbalimbali kuhusu uhamisho huu.

“Tunapenda kusisitiza uhamisho huu ni wa kawaida kama ambavyo mmekuwa mkisikia unafanyika katika wizara au idara nyingine za Serikali.

“Yawezekana kwa TAKUKURU, ikawa ni mara ya kwanza kuhamishwa kwa idadi kubwa, lakini kama mnavyofahamu, sisi kama watumishi wa umma hatulazimiki kufanya kazi katika taasisi moja tu,”ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo, imewasihi wananchi kuendelee kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo, ikiwa ni pamoja na kutoa  taarifa kupitia simu ya dharura nambari 113 ambayo hupigwa bure.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )