Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 5, 2019

RC Makonda Ataka Watendaji Kuongeza Kasi Ya Makusanyo Ya Kodi Pasipo Kuwasumbua Wananchi

adv1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji kuhakikisha wanasimamia ipasavyo makusanyo ya kodo ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu mpya na rafiki za ukusanyaji pasipo kuwatisha wala kuwabugudhi wananchi.

RC Makonda ametoa kauli hiyo wakati wa kikao mkakati baina yake ya mamlaka za ukusanyaji wa kodi ambapo amesema mwaka huu jiji hilo limedhamiria kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ili kuendelea kuwa kinara.

Aidha RC Makonda amewataka watendaji kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza idadi ya walipa kodi, kufanya mabadiliko ya sheria kandamizi zilizopitwa na wakati pamoja na kuanzisha mfumo wa malipo kwa kadi Kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Pamoja na hayo RC Makonda ameshauri kuanzisha kwa kitengo cha ushauri kwa wafanyabiashara jambo litakalowajengea wananchi hamasa ya kulipa kodi na kuondoa dhana ya kuonekana ni watu wa kukusanya mapato pekee.

RC Makonda anaamini kuwa wananchi wapo tayari kulipa kodi serikalini endepo watawekewa mazingira rafiki ya kuwawezesha kulipia ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara kuwekwa katika data base moja.

Kikao hicho kimehusisha wakuu wa wilaya, makatibu tawala, TRA, BOT, TIC, NBS, Wizara ya fedha na kamati za ulinzi na usalama.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )