Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 23, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 58

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA       
Nikawatumia meseji ya Qeen na Latifa, nikiwaomba muda wa mchane nikakutane nao mwenge ili niweze kuongozana nao kuelekea alipo ficha Clara. Kila mmoja akanijibu  atakuwa tayari japo sijawaeleza ni wapi tunakwenda. Mlango wa ofisini kwangu ukafunguliwa na Biyanka akaingia, akayatazama mafaili yaliyo jazana ofisini kwangu.
“Mume wangu hujafanya kazi leo?”
“Ndio”
“Ohoo unaonaje ukaenda hotelini ukapumzike na mimi niweze kushuhulika na hii kazi hapa kwani ofisini kwangu nimesha maliza kila jambo”
‘Usiende sehemu yoyote huo ni mtego’
Niliisikia sauti ya Ethan ikinikanya kwa ukali sana, jambo lililo nifanya nibaki nimekodelea macho Biyanka na kushindwa kumjibu kwani sifahamu ni mtego gani ambao mwanamke huyu amekusudia kuniwekea.

ENDELEA
“Usijali mke wangu, nitajitahidi kuzifanya kazi zote mwenyewe.”
Nilizungumza huku nikitabasamu.
“Kweli mume wangu?”
“Ndio, nitazifanya taratibu kwa sas anahitaji muda wa kupumzika kidogo kisha nitaendelea na majukumu mpenzi wangu”
“Sawa”
Biyanka akanibusu mdomoni kisha akatoka ofisini kwangu. Nikamuona Ethan akiwa amekaa kwenye moja ya sofa zilizopo hapa ofisini.
 
“Umesema mtego gani?”
“Tayari amesha anaza kukutilia mashaka”
“Mashaka ya nini?”
“Anahitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea kwa maana jana ulivyo toka hotelini kuna muhudumu alimtumia meseji kwamba umetoka”
“Kwahiyo amewahonga wahudumu ili waweze kunichunguza?”
“Ndio na hapa alihitaji uweze kutoka ili afahamu unaelekea wapi, angekufwata nyuma kwa nyuma na taksi na wewe akili yako ilisha panga kukutana na wale wasichana wako. Ingekuwa ni bonge la tatizo katika siku ya leo”
“Mmmmm kazi kweli kweli, je mtoto yupo wapi?”
“Tayari yupo sehemu salama, ila nahitaji tuelekee sisi wenyewe sasa hivi, hao wasichana wako kwa sasa achana nao. Umenielewa?”
“Sawa”
 
Ethan akanisogelea na kunishuka kifuani mwangu, nikamshuhudia akiingia mwilini mwangu na mwili wangu wote ukaanza kusisimka na kujawa na nguvu ya ajabu. Sikuweza kulishangaa hili kwani si mara ya kwanza kwa Ethan kuweza kufanya hivi. Kufumba na kufumbua nikajikuta nikielea angani kwa kasi huku magorofa ya jiji hili la Dar es Salaam tukiyaona kwa chini sana. Tukafika kwenye moja ya kisiwa ambacho kina miti mingi sana na katikati kuna nyumba moja tu. Tukashuka ardhini na Ethan akatoka mwilini mwangu.
“Hapa ndipo ulipo muweka Clara?”
“Ndio amelala kwa sasa humo ndani hajaniona”
“Kuna usalama kweli?”
“Ndio kwa maana wale vijana nime waua. Sasa wewe utakuwa ni mtu wa kumshawishi aendelee kuishi hapa na asidhubutu kuinigia jiji la Dar es Salaam kwani itakuwa ni hatari sana.”
“Sawa”
 
Tukaongozana na Ethan hadi ndani. Japo hii nyumba kwa nje ina onekana ni ya kawaida sana ila kwa ndani ni nyumba moja nzuri. Ina kila kiti kizuri kinacho hitajika katika nyumba nzuri, nikaingia chumbani na kumkuta Clara akiwa bado usingizini. Nikaka taratibu pembeni ya kitanda chake na nikaanza kumuita kwa sauti ya upole sana. Clara akafumbua macho yake, tukatazamana kwa sekunde kadhaa huku akionekana kujaribu kuitathimini sura yangu. Clara akaka kitako na kwa haraka akanikumbatia huku akimwagikwa na mchozi.
“Ethan umekuja kuniokoa tena”
“Ndio mdogo wangu. Nimekueleta sehemu salama”
“Wapi?”
“Hii ni nyumba ambayo nimekununulia, ipo huku porini kisiwani. Nina imani kwamba hapa hakuna adui ambaye anweza kukufikia”
Clara akaanza kuangaza huku na kule ndani ya chumba hichi. Chumba hichi kimejaa midoli mingi ambayo kwa mtoto kama Clara inaweza kumuondolea mawazo pale atakapo amua kuanza kucheza nayo.
 
“Twende ukaone huku”
Nilizungumza huku nikinyanyuka kitandani, Clara akashuka kitandani na nikamuonyesha bafu lililomo humu ndani ya chumba chake, kisha nikamtoa hadi sebleni, nikampelekea jikoni kisha nikatoka naye nje ambapo nyumba hii imezungukwa na bustani nzuri sana za maua.
“Kila kitu unacho kiona hapa mdogo wangu ni mali yako”
“Kweli kaka Ethan?”
“Ndio mdogo wangu. Kitu ninacho kihitaji ni wewe kuwa salama”
 
“Nashukuru sana”
Clara alizungumza huku akinikumbatia kwa nguvu na kuanza kulia. Nikamnyanyua na kurudi naye sebeleni, nikamalisha kwenye moja ya sofa kisha nikaka kwenye sola lililopo mbele yake na tukaanza kutazamana.
“Naamini unamfahamu maadui wanao kuwinda si ndio?”
“Ehee”
“Unamfahamu nani na nani?”
“Kwa majina siwafahamu”
“Ohoo ngoja kwanza”
Nikatoa simu yangu mfukoni na kuanza kumuonyesha Clara picha ya kwanza ya mzee Poul Mkumbo. Clara akastuka sana huku macho yakimtoka.
 
“Ni huyu?”
“Eheee ni huyu”
Nikamuonyesha Clara picha ya Biyanka. Pia akastuka sana.
“Huyu dada amekufanya nini?”
“Aliniteka”
“Alikuteka?”
“Ndio na alinikabidhi kwa watu ambao siwafahamu na walitaka kuniua na sikujua ni nini kilicho weza kutokea”
Clara alizungumza kwa sauti iliyo jaa mtetemesho. Nikamtazama Ethan aliye kaa sofa jengine na Clara hakuweza kumuona.
“Unamkumbuka aliye kusaidia?”
Clara akatingisha kichwa akimaanisha kwamba hakumbuki.
“Sawa. Unaweza kupika?”
“Ndio”
“Kule jikoni kuna kila kitu, nitakuwa ninakuja kukujulia hali kila baada ya simu moja”
“Sawa sawa”
Nikatazama simu ya mezani.
 
“Hiyo simu utaitumia kuwasiliana nami kila pale utakapo kuwa na haja nami”
“Sawa kaka Ethan”
Nikatoa kadi yangu ya biashara ambayo ina namba ya simu na kumkabidhi Clara. Nikaagana naye kisha tukoandoka na Ethan. Katika muda mfupi tu tukafika ofisini kwangu huku kidogo nikiwa na furaha.
“Ngoja nikusaidie”
Ethan alizungumza huku akika kwenye kiti changu, akaanza kupitia faili moja baada ya jengine huku akiifanya kazi hiyo kwa kasi kubwa sana. Ndani ya dakika kumi akamaliza kila kitu, kwa ishara akaniomba niweze kukaa kwenye kiti changu.
“Vipi unaonanaje kampuni yangu?”
“Inakwenda vizuri, ila inabidi uwaambie watu wanao shuhulika na maswala ya matangazo wazidishe ubunifu katika matangazo yao. Pia muboreshe vifurushi vya internet, viwe vikubwa ila kwa bei nafuu sana”
 
“Sawa nimekupata rafiki yangu”
“Kitu kingine kuwa makini na hao wanawake wako. Siku ukiwagonganisha, kutachimbika”
“Hahaaaa”
“Wewe cheke. Camila anakula tizi, sasa siku akija kukupiga mimi sinto kutetea kwa maana huo ni ugomvi wa mke na mume nitakaa pembeni”
“Hivi unahisi kwamba Camila anaweza kufahamu juu ya haya mahusiano yangu mapya”
“Hata sasa hivi akihitaji kufahamu anaweza kufahamu, ila shukuru Mungu nimefunga ufahamu wake wa akili katika maswala ya mahusiano. Wewe mwenyewe nina imani kwamba una fahamu jinsi alivyo na wivu”
“Ndio“
“Haya, namuona mke wako feki anakuja kukuchukua mukale luch baadae”
“Poa”
 
Kitendo cha Ethan kupotea hapa ofisini, Biyanka akaingia huku akiwa na furaha sana.
“Vipi mke wangu?”
Nilimchangamkia huku nikinyanyuka kwenye kiti changu na kumlaki kwa kumkumbatia.
“Baba amenipigia simu muda mchache ulio pita na kudai kwamba amemkamata yule mtu aliye kutumia meseji za vitisho”
“Weeeee!!”
Niliitikia kinafki tu kwa maana nina elewa kila kitu kinacho endelea.
“Ndio na kwa sasa yupo polisi kwa mahojiano huku wenzake ambao walikuwa wamemkamata mtoto, wawili wameuwawa huku yeye akiwa amekamatwa na polisi”
 
“Na mtoto je?”
“Mtoto sijui wamempeleka wapi hapa ndioa anaendelea kuminywa na askari wapelelezi, kwani afande Kimaro hajakupigia simu?”
“Hapana hajanipigia”
Nikaitoa simu yangu mfukoni na kwa bahati mbaya nikaikuta ikiwa imezima chaji.
“Ohoo imezima chaji”
“Ndio maana nahisi alikupigia sana hajakupata hewani”
“Basi twende huko polisi”
“Mmm sasa hivi ni saa saba, twende tukapate chakula cha mchana kisha ndio tueleke huko polisi”
“Sawa, tukirudi hivi niandalie kikao na watu wanao dili na kitengo cha matangazo”
 
“Kuna nini tena?”
“Wewe anda kikao mke wangu”
“Sawa, basi ninaomba dakika tano nikawape taarifa”
“Poa”
Biyanka akatoka ofisini humu na kuniacha peke yangu. Nikafungua droo na kutoa chaji yangu na kuichomeka simu yangu huku nikijaribu kuiwasha. Simu ilipo fanikiwa kuwaka, nikawatumia meseji Qeen na Latifa na kuwajulisha kwamba hatuto weza  kwenda sehemu niliyo waahidi kwenda mchana wa leo.
“Tayari mume wangu”
Biyanka alizungumza huku akiwa amefungua mlango. Tukatoka humu ofisini na kueeka eneo la magesho. Tukaeleka kwenye moja ya mgahawa, tukapata chakula cha mchana kisha tukaelekea kitua kikuu cha polisi. Tukapokelewa na afande Kimaro ambaye moja kwa moja akatupeleka hadi kwenye chumba cha mahujiano. Nikajikuta nikiachia msonyo mkali sana hadi Biyanka na afande Kimaro wakashangaa.
 
“Tuliza jazba mume wangu, acha polisi wafanye kazi yao”
Biyanka alizungumza huku akinishika mkono wangu wa kulia, akihisi msonyo wangu unahusika na hasira kumbe sivyo kwani mtu waliye mkamata hapa ni tofauti kabisa na yule ambaye Biyanka alikuwa ampiga vizungu.
“Wanampiga kweli atazungumza?”
Nilimuuliza afande Kimaro huku tukiwa tumekaa katika chumba cha pilia na katikati kuna kioo kikubwa ambacho sisi tunaweza kuwaona watu waliopo katika chumba hicho cha mahojiano ila wao hawawezi kutuona sisi tulipo katika chumba hichi cha wasililizaji.
 
“Ndio kwa kumpiga vile ni lazima atataja ni nani ambaye amemuagiza”
“Ila naona kama haito saidia”
“Hiyo ni adhabu moja tu Ethan, ila kuna adhabu nyingine nyingi sana ambazo zitafwata ni lazima atataja”
Afande Kimaro alizungumza huku akijichekesha chekesha. Laiti watu hawa wangekuwa wanajua kwamba nina fahamu ujinga wao wote wala wasinge kubali hata kukaa karibu na mimi.
“Badilisha adhabu”
Afande Kimaro alizungumza huku akiminya moja ya batani. Askari wawili walio ndani ya chumba hicho nikawaona wakivaa gloves mikononi mwao.
 
“Samahani, munaweza kunipa dakika hata moja nikazungumza naye?”
Biyanka na afande Kimaro wakanitazama kwa mshangao, kisha wakatazamana na Biyanka akakubali kwa ishara ya macho.
“Sawa ila inabidi askari hao waweze kubaki ndani ya chumba hicho”
“Hapana nahitaji watoke kabisa na vifaa vyao hivyo vya mateso. Nahiji wakalishe kwenye kile chumba wamfunge tu pingu basi”
“Ila huyo tuliye mkamata Ethan ni mtu hatari ni jambazi moja hatari sana”
 
“Usijali nitakuwa salama”
“Ila mume wangu h…..”
“Hapana mke wangu, niamini, nitakuwa sawa”
Afande Kimaro akawaamuru vijana wake kufanya vile nilivyo hitaji. Nikavua koti langu la suti na kumkabidhi Biyanka, nikavua saa yangu hii ya dhahabu ambayo niliinunua dola elfu ishirini na tano na nikamkabidhi pia Biyanka.
“Kuwa makini mume wangu”
“Usijali”
Nilizungumza huku nikianza kuelekea katika mlango wa kuingia katika chumba hichi. Nikaikunja mikono ya shati langu, nikaburuza kiti kimoja cha chuma na kukiweka mbele yake. Nikatazama kamera nne tatu zilizo weka kwenye kona za hichi chumba. 
 
Jamaa huyu aliye jaa majaraha mwili mzima akanitazama kwa macho yaliyo jaa huzuni kubwa sana. Kwajinsi tu anavyo onekana kwenye macho yake hana hata sifa ya ujambazi. Nikanyanyuka na kuanza kumzunguka jamaa huyu kama mara nne hivi huku nikiendelea kumdadisi huku nikihakikisha kwamba udadisi wangu hauwezi kunaswa na kamera hata moja iliyo kwenye chumba hichi kwani kila kiti kina rekodiwa. Nikajikuta nikitabasamu mimi mwenyewe huku nikikaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia hapo awali. 
 
‘Waseng** hawa wamemleta bubu humu ndani sasa atazungumza nini?’
Nilijikuta nikizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama jamaa wa watu jinsi anavyo chirizika damu, nikashusha mikono yangu chini kidogo usawa wa mweza hii na nikaanza kuzungumza na ishara za vidolea huku nikimuuliza jamaa huyu ni kosa gani ambalo limemfanya hadi kukamatwa na polisi. Nikajikuta nikishtajabu sana mara baada ya jamaa huyu kuniambia kosa la yeye kukamatwa na polisi ni kuiba kuku tena jogoo tena mitaa ya uswahilini, taratibu nikajikuta nikishusha pumzi huku nikitingisha kichwa kwa kumsikitia jamaa huyu mnyonge.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )