Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 28, 2019

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 62

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Wakanishusha kwenye moja ya kituo waendesha bajaji na pikipiki, nikangia kwenye moja ya bajaji na kuondoka eneo hili na safari ya kurudi hotelini ikaanza majira haya ya saa tatu kasoro usiku. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitazama na kukuta ni namba kutoka nchini Ujerumani. Nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni mwangu.
“Ethan”
Niliisikia sauti ya Mery akiniita huku akilia lia.
“Naam”
“Mama hali yake mbaya na kama inawezekana rudi Ujerumani, anahitaji kukuambia neno la mwisho kabla ya kukata roho”
Mwili mzima ukahisi kuzizima na viungo vyote vikafa ganzi, nikajikuta mapigo ya moyo yakinienda kasi hadi jasho likaanza kunitiririka mwilini mwangu.

ENDELEA
“Ethan unanisikia?”
“Ndio ninakusikiliza dada”
Nilizungumza kwa kujikaza tu.
“Fanya uje, ninaogopa nipo peke yangu huku”
“Sawa ngoja niangalie maswala ya usafiri”
“Sawa”
Simu ikatwa, nikashusha pumzi nyingi sana huku nikifikiria ni kitu gani ninacho weza kukifanya mtu. Mtu wa kwanza kunijia kichwani mwangu ni Camila mwanamke ninaye mpenda kuliko kitu chochote kwenye maisha yangu. Nikaitafuta namba yake kwenye simu yangu kwa haraka na nikaipata, nikaipga na kuiweka sikioni mwangu, simu yake ikaita baada ya sekunde kadha ikapokelewa.
“Ndio mume wangu”
“Upo wapi?”
“Nipo nyumbani baby, tunapata chakula cha usiku”
“Inabidi twende Ujerumani leo hii hii”
“Leo!! Kuna tatizo gani mume wangu?”
“Hali ya mama ni mbaya sana na anahitaji hospitalini. Hivyo pakiza kili kitu chako nina imani usiku huu utaweza kufika Dar, hapa nitashuhulikia maswala ya ndege ya kukodi”
“Sawa mume wangu”
 
Camila alinijibu kwa sauti ya unyonge kisha nikakata simu. Nikaingia kwenye mtandoa wa google, nikatafuta ni shirika gani ambalo lina ndege za kukodi, kwa habati nzuri nikapata shirika moja liitwalo THRIPPLE P AIR WAYS. Nikaangalia baadhi ya ndege zao ambazo ni private jet. Nikaridhika nazo, nikachukua namba yao ya simu na kuwapigia.
“Karibu Tripple P Air Ways, unazungumza na Liliana, nani mwenzangu”
Niliisikia sauti ya kike nzuri sana ambayo kidogo ikanita hata ujarisi wa kuzungumza kama mweume mwenye pesa zake.
“Mimi ni Ethan, ninahitaji ndege ya kukodi kuelekea nchini  Ujerumani”
“Karibu sana, unahitaji kwa lini”
“Nahitaji kwa leo, nimeona ndege moja aina ya Gulfstreem N60983. Nina imani kwamba ipo nchini Tanzania”
“Ndio muheshimiwa inapatikana. Kutoka hadi Tanzania hadi Ujerumani, itakugarimu kiasi cha dola laki sita na nusu”
“Sawa niwekeeni, nafanya malipo ya awali kwenye akaunti yenu sasa hivi na nikifika hapo uwanja wa ndege kwenye ofisi zenu nitafanya malipo mengine ya mwisho”
“Sawa karibu sana na akaunti namba yetu ndio hiyo iliyopo kwenye tovuti yetu”
 
“Ninashukuru sana”
Nikakata simu na kwa mara kadhaa dereva huyu bajaji macho yake yote anayaelekezea kwangu.
“Kaka wewe ndio yule Ethan, huku tumezoea kukuita Messi?”
“Ndio”
“Aisee tukifika tunapo kwenda ninaomba tuweze kupiga picha japo moja”
“Sawa”
Tukafika hotelini. Dereva akatoa simu yake, akasimama pembeni yangu na kuanza kupiga picha kadhaa huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Nikamkabidhi kiasi cha pesa ambacho hata sikuzihesabu. Nikakimbilia ndani ya hoteli, nikaingi kwenye lifti na kuelekea juu gorofani. Nikaingia chumbani kwangu, kwa haraka nikavua nguo zangu zote nilizo zivaa. 

Nikafungua laptop yangu na kuingia kwenye akaunti yangu ya benki ya Bacrays na kuhamisha kiasi cha dola laki tatu na nusu kwenye akaunti ya shirika hili la ndege kisha nikaingia bafuni, kwa haraka nikaoga kisha nikarudi chumbani. 

Nikaweka begi langu juu ya kitanda na kuanza kuweka nguo zangu kadhaa. Nikampigia Camila simu yake, kwa bahati mbaya sikuweza kuipata hewani. Nikaumbuka kwamba kuna watu wa kuwaga. Nikampiagia simu Qeen kisha nikaiunganisha na Latifa.
 
“Jamani nina habari sio nzuri”
“Habari gani tena mkuu?”
“Hapa ninapo zungumza nipo kwenye harakati za kuelekea nchini Ujerumani, mama yangu ana umwa sana hivyo ninaondoka usiku huu na nimesha kodisha ndege moja ya kutupeleka huko”
“Ya kuwapelekea huko na nani?”
“Mimi na mke wangu”
“Unataka kusema kwamba unakwenda na Biyanka?”
“Nani aliye waambia Biyanka ni mke wangu, ninakwenda na mke wangu halisi”
“Mmm tuyaache na hayo pole sana Ethan”
“Nashukuru Latifa”
“Pole sana boss’
 
“Asante Qeen. Ila mipango yetu ipo pale pale hakuna jambo lililo haribika mume nielewa?”
“Tumekuelewa mkuu”
“Kitu kingine hakikisheni kwamba hamtoi siri hii kwa mtu yoyote”
“Tumekuelewa mkuu”
“Nashukuru”
Nikakata simu na kumpigia tena simu Camila huku nikimalizia kulifunga begi langu. Simu yake ikaanza kuita, nikaiweka simu yangu loud speaker na kuiweka kitandani na kuendelea kuvaa nguo haraka haraka.
 
“Mume wangu?”
“Mbona simu nakupigia haipatikani?”
“Tupo njiani na Dany, kuna sehemu nyingine hazina mtandao”
“Mumefikia wapi?”
“Sijajua ni wapi?”
“Hembu  mpe simu Dany”
“Ethan”
“Ndio, mume fika wapi?”
“Kwasasa tupo sehemu inaitwa Mkata, ila kama baada ya lisaa moja hivi na nusu tutafika hapo”
“Sasa nakuomba muje moja kwa moja uwanja wa ndege kwa maana mimi huko ndipo ninapo elekea kwa sasa, kuna mambo ninakwenda kuyamalizia kuyakamilisha kwa ajili ya safari”
“Sawa”
 
Nikakata simu, nikajiweka vizuri suti hii  ya rangi ya kaki niliyo ivaa. Nikaangaza huku na huku kwenye hichi chumba, nikaingiza laptop yangu kwenye begi langu la mgongoni kisha nikalivaa. Nikabeba begi langu hili la nguo na nikatoka chumbani humu. Moja kwa moja nikaeleka hadi mapokezi, nikawakabidhi kadi yao ya kufungulia mlango.
 
“Akija mke wangu muta mkabidhi hii kadi sawa”
“Una safiri?”
“Acha maswali mengi dada. Mkabidhi hii kadi umenielewa”
“Sawa”
Nikatoka nje na kuingiza begi kwenye gari langu hili. NIkawasha gari na kuanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege. Picha ya sura ya mtoto Clara ikanijia kichwani mwangu, wasiwasi  wa kuondoka pasipo kuweza kumuaga ikanijaa moyoni mwangu.
 
‘Nitarudi’
Nilijifariji huku nikiogeza mwendo kasi wa gari langu. Kuna baadhi ya maeneo iliniladhimu kusimama kutokana na foleni za magari. Simu ikaanza kuita na nikaitazama na kuona ni namba ya Biyanka, moyo wangu ukaendelea kujawa na wasiwasi kwa mana sijamueleza juu ya hili swala la mimi kuondoka.
“Ndio mke wangu”
“Samahani mume wangu, tumeshindwa kupata ndege ya kundoka, hivyo tutarudi kesho asubuhi na kikao pia hakuna kwa usiku wa leo”
 
“Sawa, ila samahni mke wangu. Mama anaumwa nchi Ujerumani amelazwa na yupo mahututi na ana hitaji kuniona haraka iwezekanavyo”
“Ohoo Mungu wangu, ni nini tena kinamsumbua?”
“Madaktari bado hawajananiweka bayana. Hivyo sasa hivi ninaelekea uwanja wa ndege, nimepata moja ya tiketi kwenye shirika la ndege la  fly Emirates. Hivyo ninaondoka Tanzania usiku huu”
Nilimuongopea Biyanka.
“Jamani mume wangu nina kuoena huruma. Ningekuwepo tungeondoka na ndege ya baba”
“Usijali, tutawasiliana, yaani kichwa changu hapa kimevurugika sana, hadi nimesahau kukufahamisha”
“Natambua kwa habari kama hiyo ni lazima kichwa kichanganyikiwe mume wangu. Sawa, nitamueleza mama na baba na tunazidi kukuombea uweze kurudi salama”
 
“Nashukuru. Kampuni, ninakutegemea mpenzi wangu”
“Usijali mume wangu, nitasimama imara na hakuna ambacho kitakwenda vibaya”
“Sawa ninashukuru kusikia hivyo”
“Ukipanda ndege, samahani nina omba uweze kunifahamisha”
“Sawa”
Nikakata simu na kuendelea na safari yangu ya kuelekea uwanja wa ndege. Nikafanikiwa kufika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Nikashuka kwenye gari langu na kuelekea moja kwa moja kwenye shirika la Thipple P Air ways,  nikapokelewa vizuri sana na muhudumu niliye zungumza naye.
 
“Tumeweza kupokea kiasi ulicho kituma. Ndege ipo tayari ni wewe kuweza kufanya malipo ya mwisho ili uweze kuondoka”
“Sawa”
Nikalipia kiasi cha mwisho cha pesa ambacho kimesalia. Tukaandikishana mkataba wa safari hii na endepo kutaotokea tatizo lolote ama ajali ya angani basi kampuni hii italipa familia yangu fidia ya asilimia hamsini ya kile kiasi nilicho lipia.
 
“Kama unahitaji kwenda kukagua ndege inaweza kuongozana na wataalamu wetu”
Lilian alizungumza mara baada ya kumaliza kulipa kiasi hichi cha pesa.
“Sawa, hili begi langu si ninaweza kuliacha hapa?”
“Ndio unaweza kuliacha tu hapa”
Nikaondoka na mainjinia wawili wa shirika hili, tukafika katika ndege hii, wakaanza kunionyesha sehemu moja baada ya nyingine. Ni ndege nzuri sana.
 
“Hii spidi mita yake ni kilomita 900 kwa lisaa moja. Sifa yake nyingine inaweza kwenda umbali wa kilomita 8, 000 bila ya kuongezwa mafuta, hivyo boss hapa upo salama”
Injinia huyu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hivi hizi viwandani zinauzwa kiasi gani?”
“Mmmm inategemea na kile kitu unacho hitaji kutengenezewa na kiwanda husika.”
“Nashukuru nitalifwatilia hilo”
 
Tukarudi ofisini kwao. Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni Camila ndio anaye piga, nikaipoke.
“Tumefika uwanja wa ndege mume wangu njoo unichukue nje”
“Sawa”
Nikatoka hadi nje na kuwakuta Camila na Dany wakiwa wamesimama kwenye maeneo ya maegesho ya magari. Camila akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kuninyonya lipsi zangu, alipo ridhika tukaachiana na nikasalimiana na Dany.
“Nashukuru kwa kumleta mke wangu”
“Usijali, ila poleni sana kwa mama kuumwa”
“Nashukru Dany, kuna gari ile BMW, kidogo ilipata itilfu ipo kwenye gereji moja hapa mjini”
 
Nikamuelekeza Dany gereji hiyo sehemu ilipo na akanielewa. Nikamkabidhi funguo ya gari langu hili jipya na kumuomba alipeleke kwenye kampuni jengo la kampuni yangu na funguo aikabidhiwe kwa mkurugenzi msaidizi ambaye ni Biyanka. Nikamtumia meseji Biyanka ya kumfahamisha kwamba gari atalikuta ofisini kwetu. Tukaagana na Dany kisa nikabeba mabegi mawili ya Camila na kuelekea kwenye ofisi za Tripple P air ways.
 
“Tupo tayari kwa safari”
“Sawa na marubani tayari wapo ndani ya ndege”
Lilian alizungumza huku akitutazama.
“Nashukuru”
Tukasaidiwa na vijana wabeba mizigo wa kampuni hii hadi ilipo ndege. Baada ya kuhakikisha kwamba mizogo  yote imepakizwa kwenye ndege, tukaingia kwenye ndege hii ya kifahari na safari ikaanza taratubu, baada ya ndege kuwa hewani Camila akafungua mkanda wa siti yake na kunifwata sehemu nilipo kaa, akanikalia mapajani mwangu huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Nina hamu na wewe mume wangu”
“Hata mimi nina hamu na wewe mke wangu, ila tupo angani kwa sasa hatuwezi kufanya chochote”
Nilizungumza kwa unyonge huku nikizichezea chezea nywele nyingi za Camila. Taratibu akakilaza kichwa chake kifuani mwangu na ndani ya muda mchache usingizi ukaanza kumpiti, nami usingizi ukaanza kunipitia, nikajikaza nisilale, ila nikashindwa kujizuia na nikalala usingizi fofofo.Sauti ya rubabi akituomba tuweze kufunga mikanda, ndege ikataka kutua ikatustua kutoka usingizini. 
 
“Tumefika Ujerumani?”
Camila aliniuliza huku akinitazama usoni mwagu”
“Nahisi mke wangu”
Camila akarudi kwenye siti yake na kufunga mkanda, nikafungua kijipazia kidogo cha dirisa na kuchungulia nje, nikaanza kuona baadhi ya majengo marefu ya nchi hii ya Ujerumani, nikashusa pumzi kwani safari hii imetuchukua masaa mengi na sijui ni kwanini tumelala sana. Ndege ikatua uwanja wa ndege, hatukuhitaji kupoteza muda, tukakodi helicopter hadi katika hospitali aliyo lazwa bi Jane Klopp. Da Mery akatupokea, huku akilia kwa uchungu sana, nikakumbatiana naye huku nikihiataji kufahamu ni nini kinacho endelea kwa mama yetu.

==>.ITAENDELEA KESHO
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )