Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 3, 2019

Seth, Rugemarila Kuendelea Kysota rumande

Washtakiwa katika kesi ya Uhujumu Uchumi, Habinder Seth na James Rugemarila, wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokukamilika.

Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Juni 2017, kujibu mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha.

Rugemarila ambaye ni Mkurugenzi wa VIP na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Sethi ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa PAP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Wakili wa Takukuru, Leonard Swai amedai leo Alhamisi Januari 3, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Wanjah Hamza kuwa, kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi wake bado haujakamilika, hivyo anaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Hamza ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 17, 2019 itakapotajwa tena, washtakiwa wamerudishwa rumande.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...