Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, January 25, 2019

Tume ya Taifa ya Uchaguzi Yafanya Uteuzi wa Diwani Mwanamke wa Viti Maalumu

 Kwa mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 23 Januari, 2019 imemteua Ndg. FATUMA MICHAEL SHIJA kuwa Diwani wa Viti Maalum (CCM) katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
 
Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hiyo wazi, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) baada ya aliyeteuliwa awali kufariki dunia.
Imetolewa  tarehe 23 Januari, 2019.

Dkt. Athumani J. Kihamia
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )