Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

UPDATES: Serikali Gabon Yafanikiwa Kuzima Jaribio la Wanajeshi Waliotaka Kuipindua Serikali

adv1
Waziri wa mawasiliano nchini Gabon anasema wanajeshi waaminifu kwa serikali ya Rais Ali Bongo wamefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi ya serikali nchini humo.

Bw Guy-Bertrand Mapangou ameambia BBC kwamba wanajeshi wanne waliohusika katika jaribio hilo wamekamatwa na mwingine wa tano anasakwa.

“Hali ni tulivu. Polisi ambao huwa hapo wamerejea na kuchukua udhibiti wa eneo lote la makao makuu ya mashirika ya redio na runinga, kwa hivyo kila kitu kimerejea kawaida,” amesema.

“Walikuwa watano. Wanne wamekamatwa na mmoja yupo mafichoni na atakamatwa saa chache zijazo.”

Kundi la wanajeshi nchini Gabon lilikuwa limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi na kutangaza amri ya kutotoka nje.

Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita walikuwa wakishika doria katika barabara za mji mkuu Libreville.

Kwa mujibu wa BBC, Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo lilitangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo.

Walichukua udhibiti wa kituo hicho cha redio mwendo wa saa kumi alfajiri (saa kumi na mbili alfajiri Afrika Mashariki).

Wanajeshi hao walikuwa wamesema wamechukua hatua hiyo “kurejesha demokrasia” na wametangaza kwamba wanataka kuunda ‘Baraza la Taifa la Ufufuzi/Ukombozi’. Taarifa yao pia ilipeperushwa kupitia runinga ya taifa.

Walikosoa hotuba ya Mwaka Mpya iliyotolewa na Rais Bongo mnamo 31 Desemba, na wanasema kwenye hotuba hiyo mawazo yake yalionekana kutotiririka na sauti yake ilikuwa dhaifu.

Bw Bongo amekuwa nje ya nchi hiyo kwa zaidi ya miezi miwili, akipokea matibabu nchini Morocco kutokana na maradhi ambayo hayajafichuliwa baada yake kuugua akiwa ziarani Saudi Arabia 24 Oktoba kuhudhuria mkutano mkubwa wa kiuchumi nchini humo.

“Hauwezi kumlaumu mtu kwa kuwa mgonjwa. Bado anapata nafuu. Ni lazima angalau uwe na heshima kidogo, na kumheshimu mtu mgonjwa, hasa kiongozi wa nchi,” alisema msemaji wa serikali Mapangou baada ya jaribio hilo la mapinduzi kuzimwa.

Familia ya Bongo imetawala taifa hilo kwa miaka 51 iliyopita, na imetuhumiwa kwa kujilimbikizia mali na utajiri mkubwa kutokana na rasilimali za taifa hilo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )