Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 30, 2019

Waziri Lugola Asema Chanzo cha Mauaji Watoto Watatu Njombe ni Imani za Kishirikina

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, Kangi Lugola amesema imebainika kuwa mauaji ya watoto mkoani Njombe ni ya imani za kishirikina.

Lugola ametoa kauli hiyo leo Jumatano Januari 30, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola.

Mbunge huyo amehoji ni mkakati gani umewekwa na Serikali katika kukomesha mauaji ya watoto katika mkoa wa Njombe ili kurudisha amani mkoani humo.

Akijibu swali hilo, Waziri Lugola amesema tangu juzi Januari 28, 2019 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni yupo mkoani Njombe ambako anafanya vikao vya ndani na kamati za ulinzi ili kutafuta chanzo.

"Tumeshapata orodha ya majina ya wahusika na tumebaini sababu kubwa ni imani za kishirikina, lakini nawaonya wote wanaohusika kuwa wasitingishe kibiriti katika serikali ya Rais John Magufuli, watashughulikiwa," amesema Lugola

Waziri amesema Serikali iko macho na itaendelea kuwa macho katika kuwalinda watu wake na vyombo vya ulinzi havitalala.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )