Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 2, 2019

Jeshi La Polisi Mkoa Wa Mbeya Linawashikilia Wahamiaji 15 Raia Wa Nchini Ethiopia

adv1
Ni kwamba Februari 01, 2019 saa 01:30 usiku huko katika maeneo ya Mlima Igawilo kwenye kizuizi [Road Block] kilichopo barabara kuu ya Mbeya kwenda Tukuyu, Askari Polisi waliokuwepo eneo hilo walimkamata ALEMEYKU MAKANE [15] raia wa nchini Ethiopia akiwa na wenzake 14 wakiwa wameingia nchini kinyume cha sheria.

Wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kwenye gari lenye namba za usajili T.645 ADP aina ya Scania lori ambalo kumbukumbu zake zinaonyesha linamilikiwa na ndugu SALUM ALLY MBARUKU, Mkazi wa Kiwira, Mkoani Mbeya. Wahamiaji hao walikuwa wakisafirishwa kuelekea Afrika ya Kusini kupitia Wilaya ya Kyela kisha nchi jirani ya Malawi hadi Afrika Kusini.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na msako mkali kumtafuta dereva wa gari hilo ADAM YUSUPH @ SAFARI, Mkazi wa Mpanda ambaye alikimbia na kulitelekeza gari hilo baada ya kusimamishwa na askari katika kizuizi cha barabarani.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )