Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 4, 2019

Kanisa la Shekinah Presbyterian Tanzania Latoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi Wasio na Uwezo wa kumudu baadhi Ya Mahitaji ya shule.

adv1
Kanisa la Shekinah Presbyterian Tanzania limetoa vifaa mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao hawana uwezi wa kumudu baadhi ya shule. 


Tukio hilo limefanyika katika maeneo ya Madale, Mbande-Kisewe, Kibaha pamoja na kanisa lililo katika mtaa wa Kulangwa jijini Dar es salaam. Vifaa vilivyotolewa ni sare, daftari, kamusi kwa wanafunzi wa sekondari na fedha taslimu Tsh. 10,000 kwa kila mwanafunzi wa shule ya Msingi, na kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Tsh. 20,000. 

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa msaada tarehe 1/2/2019 huo katika kanisa la Mbande Kisewe, mchungaji kiongozi wa Shekinah Daniel John Seni alisisitiza kwamba mojawapo ya majukumu ya kikanisa, ukiachilia kuhubiri Injili ni kuwasaidia watu wa makundi tofauti.


 Aliongeza kwamba “sisi tumeona tushughulike na suala la Elimu, kwa sababu ni haki ya mtoto kupata Elimu.” Hata hivyo aliwalaumu viongozi wa serikali za mtaa wa Msongola-Mbande Kisewe kwa kushindwa kushirikiana na taasisi kama za kidini ili kuwasaidia watoto wa eneo hilo. 

Alisema “nashangaa kwa nini hakuna kiongozi hata mmoja wa serikali ambaye amehudhuria tukio hili? Nimesikia walipata mwaliko, lakini hakuna hata mwakilishi hata mmoja. Ninawaomba watu wa namna hii wakija kuomba kura msiwape kwa sababu wao wanawatumia kwa faida yao wenyewe.” 

Aliwapongeza wanafunzi waliopokea msaada huo alisema kwamba “ninyi wanafunzi someni kwa bidii, hakuna sababu ya kukosa shule eti kisa huna sare za shule, tumekununulia sare mpya kabisa, tumieni vizuri.”

Akitoa msaada huo katika eneo la Kibaha kwa Mfipa (Galagaza) tarehe 2/2/2019 Mchungaji Seni aliwashukuru viongozi wa serikali na waalimu wa shule ya msingi Galagaza kwa kushiriki tukio hilo. Aliwasihi wazazi washirikiane pamoja na waalimu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu bora katika maeneo yao. 


Alisisitiza kuwa “ingawa ni wajibu wa serikali kujenga madarasa kwa ajili ya watoto, lakini sisi kama wazazi ni lazima tujitoe mali zetu kwa ajili ya kujenga. Ingawa elimu inatolewa bure, lakini kuna masuala mengine ambayo wazazi lazima tuwe na ufahamu wa kuyatatua badala ya kushitaki kwa wakuu wa wilaya.” 

Vilevile akitoa msaada katika eneo la Madale, Jumapili tarehe 3.2.2019 mchungaji Seni alisisitiza kwamba, “pesa hizi ni sadaka ambayo watu wa Mungu wamejitolea kwa ajili ya watoto wa Tanzania, ni vyema itumike kama ilivyokusudiwa kwa kuwasaidia wanafunzi. Ingawa ni kiwango kidogo, lakini kitawasaidia kwa namna yake.” 

Katika msaada huo, ni jumla ya watoto mia moja na thelathini na nane (138) wamepata msaada huo. Mchungaji Seni aliwashukuru sana wachungaji Shadrack Misungwi wa Shekinah Mbande Kisewe, mchungaji Marko Shija wa Shekinah Galagaza, pamoja na Mwinjilist Maria Masanja wa Shekinah Kulangwa kwa bidii zao katika kazi ya Mungu na kwa jamii pia. 


Alisema kuwa “ hawa watumishi wa Mungu wanastahili pongezi kwa sababu pengine wangeamua kukataa kwamba tusilete msaada kwenu, na kweli tusingeleta. Wana moyo wa Upendo, tuwaombee kwa Mungu ili awatie nguvu zaidi na zaidi.”

 Mwisho alimaliza kwa kusema kwamba  Watanzania ni lazima tushirikiane na serikali ya awamu ya tano ambayo imeonesha nia ya kuwasaidia watoto wapate elimu bure, tuunge mkono shughuli za maendeleo na wala siyo kupinga. Alisisitiza kwamba “kanisa hili litaendelea kushirikiana pamoja na serikali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanafunzi wanapata mahitaji yao ya msingi kwa ajili ya kuelendelea na masomo yao”

Imetolewa na uongozi wa kanisa
Shekinah Presbyterian Church/ Madale
P.O.BOX 32807 Dar es salaam
0769080629

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )