Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, February 2, 2019

Marekani Kutangaza uamuzi MGUMU Sakata la Makombora ya Nyuklia ya Masafa Marefu

adv1
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Mike Pompeo, anatarajiwa wakati wowote kutoka sasa kutangaza uamuzi wa nchi yake wa kubatilisha makubaliano yanayositisha matumizi ya makombora ya kinyukilia yenye uwezo wa kushambulia kutoka bara moja hadi jingine (INF).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali duniani, vimeripoti kwa sauti moja kwamba Marekani imeshawaarifu washirika wake katika Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) kuhusu uamuzi huo.

Makubaliano hayo ya kudhibiti mbio za kutengeneza silaha, yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na Umoja wa Usovieti yamechangia pakubwa katika kumalizika vita baridi.

Mataifa yote mawili yaliahidi kuachana moja kwa moja na makombora ya kinyukilia ya masafa ya wastani. Kwa miaka sasa Marekani imekuwa ikiituhumu Urusi kwenda kinyume cha makubaliano hayo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )