Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, February 16, 2019

Mgimwa: Sheria Za Kilimo Zilizopo Kwa Sasa Hapa Tanzania Ni Za Tangu Ukoloni Na Za Unyonyaji Kwa Wakulima

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mwenyekiti wa kamati za kudumu za bunge ,kamati ya kilimo ,Mifugo na Maji Mhe.Mahamoud Mgimwa amesema kuwa sheria za kilimo  zilizopo kwa sasa  hapa Tanzania ni za  tangu ukoloni na hazina tija yoyote kwa mkulima wa kawaida bali zipo kwa ajili ya kumwumiza na kunufaisha watu wa tabaka  la juu.

Mgimwa ameyasema hayo  Februari 15 jijini Dodoma wakati akifunga mkutano  mkuu wa tano wa wadau wa Sekta  ya  kilimo hapa nchini ambapo amezitolea  mfano baadhi ya sheria ambazo serikali imezikuta kutoka kwa wakoloni ni pamoja na sheria   ya bodi ya korosho,sheria ya bodi ya pamba na sheria ya tumbaku hivyo kuna uhitaji mkubwa wa kutunga sheria zitakazoleta tija kwa wakulima.
 
“Sheria nyingi  ukiangalia ni za kikoloni hatujazitunga sisi,kuna sheria ya bodi ya korosho,sheria ya bodi ya tumbaku,sheria ya bodi ya Pamba nakadharika,angalia hazikuwa zinamfever mkulima zilikuwa zinamfever mkoloni kwa hiyo tunahitaji kuwa na sheria yetu watanzania,sheria zinatungwa nje ya bunge na ndani ya bunge kwa hiyo anzeni mchakato mkiona kuna ukakasi tunashirikiana ili mkulima wa chini anufaike na yeye”
 
Mhe.Mgimwa amefafanua mkulima wa chini amekuwa akihangaika kulima yeye mwenyewe bila usaidizi wowote  lakini inapofika wakati wa mavuno  serikali inamwingilia na kumpangia namna ya kuuza au kutouza mazao Yake  kutokana na mfumo mbovu na kandamizi wa sheria zilizopo za tangu ukoloni .
 
“Mkulima anapokwenda kulima shamba hana confilict na mtu yeyote  aidha akodi shamba au alime shamba lake,ikifika wakati wa kuvuna anataka kuuza serikali inakuja kumwambia hakuna kuuza nje ya nchi,sawa si sawa.

"Kwa  hiyo  hakuna sheria yoyote inayomlinda mkulima zaidi ya kumnyonya na kumgandamiza,hivyo kuna uhitaji mkubwa wa marekebisho ya sheria wadau wa kwanza wa kuangalia mapendekezo ya sheria ni ninyi wadau na wataalam  wa kilimo pekee sisi bunge ni kupokea mapendekezo,kujadili na kutunga sheria”
 
Katika hatua nyingine Mgimwa amemtaka mwandaaji na mratibu wa kongamano hilo la wakulima  ,Mshauri wa Masuala ya kilimo Tanzania, Profesa David Nyange kuwa na utaratibu wa kuwashirikisha  wakulima wenyewe wa hali ya chini  na si kama ilivyo  kwa sasa  ambapo wamekuwa wakishiriki wasomi pekee  huku pia  akitaka mpango wa program wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili[Agricultural Sector Program ][ASDP-2] kuwa na mpango wa kuweka ripoti kwamba imefikia wapi katika utekelezaji wake huku serikali ikiwa na mpango wa kuwekeza  Sh.Trilioni 14 .
 
“Wataalam mpo wengi sana kuliko hata watu waliokusudiwa.mkutano huu ungependeza ungekuwa na wakulima wengi,wavuvi wengi,pamoja na wafugaji.Lakini liangalieni nanyi watu wanaobadilishana mawazo sio tunaowalenga”.
 
Kwa upande wake Mshauri wa Masuala ya Kilimo hapa nchini Prof.David Nyange amesema maazimio ya mkutano huo watayachambua zaidi na kuyafikisha katika sehemu husika huku Mtaalam mwingine wa masuala ya kilimo ambaye kwa sasa ni Katibu tawala mkoa wa Kagera Prof.Faustine Kamzora akisema kuwa  Tanzania haiwezi kuondokana na umasikini bila kuongeza tija.

Mkutano huo wa siku tatu umehudhuriwa na wataalam na viongozi mbalimbali wa asasi za kiraia na kiserikali miongoni mwao ni pamoja na makamu mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge,kilimo,mifugo na maji Dokta  Christopher Ishengoma,Mhadhiri chuo kikuu cha kilimo-SUA Dokta Sizya Lugeye ,mkurugenzi wa mradi SOYA NI PESA kupitia taasisi ya CATHORIC RELIEF SERVICE Bi.Neema Mrema  na wengine wengi na kaulimbiu ni mchango wa sekta ya kilimo katika kuhamasisha kukuza viwanda.
 
MWISHO.

tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )