Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Rais Magufuli kuzindua Mahakama Zinazotembea(Mobile Court) Kesho

adv1
Na Erick Msuya – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli (Kesho February 6) anatarajia kuzindua Mahakama zinazotembea (Mobile Court) Jijini Dar es Salaam ikiwa ni mpango mkakati wa Mahakama wa kumaliza mlundikano wa kesi.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashauri wa Mahakama ya Tanzania, Eva Nkya uzinduzi huo utafanyika katika sherehe  za siku ya Sheria kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mpango huo wa Makahama zinazotembea umekuja kufuatia maombi ya Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma kwa Rais Ikulu January 29 mwaka huu Jijini Dar Es Salaam wakati akiwaapisha Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ombi lililohusu kuimarisha miundombinu ya Mahakama,kuongeza Mahakama zinazotembea (Mobile Court) na kuongeza rasilimali Watu.

Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi hao Ikulu Jijini Dar es Salaam ,Rais Magufuli alisema wazo la kuwa na Mahakama hizo zinazotembea ni wazo jema na la ubunifu katika kushughulikia kero za wananchi hususan katika upatikanaji wa haki. 

Mpaka sasa nchini Tanzania tuna mahakama za Mwanzo 960, kata zaidi ya elfu 3 ambazo hazina mahakama, serikali imeona si vyema kukaa kusubili majengo ya mahakama mpaka kujengwa kwa kipindi kirefu, hivyo kuanzishwa kwa magari haya yatakuwa mkombozi kwa wananchi waishio katika kata zisizo kuwa na mahakama.

Dhana ya mahakama zinazotembea ni mahususi kwa kuwapunguzia gharama wananchi wa tanzana,kuwapunguzia muda wa kwenda mahakamani, kuwapa uhuru wa kuweza kufanya shughuli zao na kuwapa elimu wananchi juu ya haki zao za msingi katika mahakama.

Mpaka sasa serikali imeshanunua magari mawili yenye uwezo wa kusikiliza mashauri ya wananchi kwa aslimia 100, na kwa awamu hii ya kwanza wameanza na Mahakama ya mwanzo na Mahakama ya Wilaya hivyo kadri siku zitakavyozidi serikali inatalajiwa kuongeza magari mengine kutokana na mwamko wa wananchi.

Magari hayo ya Mahakama zinazotembea zinatarajia kuanza katika mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza hii yote kutokana na wingi wa mashauli, uchache wa mahakama na idadi ya watu hasa waishio Dar es Salaam katika maeneo mbalimbali katikaikoa tajwa .

Mbali na kusikiliza kesi, mahakama hizi zinatoa elimu kwa umma na kuelimisha wananchi juu ya kupata huduma za mahakama,  kufanya usuluishi kwa jamii na kuhusika kwenye oparesheni  maalumu za kiusalama  endapo zikitokea.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )