Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, February 4, 2019

VIDEO: Serikali Yatoa Ufafanuzi Madai Ya kununua korosho chini ya bei elekezi ya sh. 3,300

Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya watu wa kada mbalimbali, akiwemo mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali kuwa korosho inanunuliwa chini ya Sh3,300 kinyume na agizo lililotolewa na Rais John Magufuli.

Naibu waziri wa Kilimo, Omar Mgumba ametoa ufafanuzi kuhusu bei ya korosho leo  February 4, 2019 akibainisha kuwa korosho inanunuliwa kwa Sh3,300 kwa kilo moja, kwamba maagizo ya Rais hayajakiukwa.

Mgumba amesema kiasi cha Sh3,300 kwa korosho daraja la kwanza, daraja la pili ndio hununuliwa kwa Sh2,640.

Mgumba alikuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe aliyetaka kujua kwa nini wanunuzi wa korosho wamekiuka agizo la Rais Magufuli na kuanza kulipa chini ya kiwango ambacho hakikuelekezwa.

==>>Tazama hapo chini
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )