Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 12, 2019

Wafanyabiashara Mikoa ya Kanda ya Kaskazini Kutumia Bandari ya Tanga

adv1
WAFANYABIASHARA wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wameonesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kupitisha shehena ya mizigo yao baada ya kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa bandari hiyo.

Wameonesha nia hiyo kwenye mkutano wa siku moja baina ya uongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na wafanyabiashara na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Meneja wa Bandari ya Tanga, Percival Salama alifafanua kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake, imeboresha miundombinu na mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo.

Alisema kuwa kutokana na maboresho hayo taratibu za uchukuaji wa mizigo zinatumia muda mchache tofauti na awali kutokana mamlaka zote za serikali zinazohusika na bandari zipo kwenye jengo moja.

“Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi bandari ya Tanga ni nzuri, salama kwa mizigo na ni ya uhakika kwa vile tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi, miundombinu, utendaji kazi na Tehama,” alisema na kuongeza:

“Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu”.

Katika kusogeza huduma zake kwa wateja wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, alisema tayari uongozi wa Mkoa wa Arusha kupitia Mkuu wa Mkoa huo, Mrisho Gambo umetoa eneo lenye ukubwa wa ekari 500 la Malula katika Wilaya ya Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.

“Wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro mtakuwa hamna haja ya kuja hadi Tanga kuchukua mizigo, mtakuwa mnasubiri mizigo yenu huko huko Arusha sisi tunawaambia gharama zetu tu mnalipia moja kwa moja na sisi tutajuana na Shirika la Reli( TRC) ambao tunategemea ukarabati wa reli ukikamilika uwatumie wao,” alisema.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Lydia Mallya aliwasihi wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa. Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Shirima alisema waliikimbia Bandari ya Tanga na kuhamia Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na urasimu uliokuwa unafanywa na taasisi za serikali zilizokuwa zinahusika na utoaji wa mizigo, jambo ambalo lilikuwa linachelewesha mizigo.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima(TCCIA) Mkoa wa Arusha, Walter Maeda aliongeza kuwa wafanyabiashara wa Arusha wanafahamu kuwa kikwazo kikubwa katika Bandari ya Tanga ni taasisi za serikali katika kuchelewesha mizigo ndiyo maana waliachana nayo.

“Sisi tuliikimbia bandari ya Tanga na kuamua kutumia Bandari ya Mombasa kutokana na nenda rudi zilizokuwa zinafanywa na TRA,TFDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa), TBS (Shirika la Viwango) kwa kweli walikuwa hawana ushirikiano mzuri hali iliyotuletea taabu sisi wafanyabiashara,” alisema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )