Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 6, 2019

Wasanii Kutembelea mradi wa reli ya kisasa (SGR) Aprili 07/2019

adv1
Wasanii takribani 300 nchini Tanzania wanatarajiwa kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro.

Akizungumzia safari hiyo jana, Msanii wa filamu nchini ambaye pia ni mratibu wa msafara huo Bw. Steve Nyerere amepongeza uongozi wa shirika la reli (TRC) kwa kuwapa fursa wasanii na kutambua mchango wao katika jamii.

Steve Nyerere alimpongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kwa kufanikisha safari hiyo ambayo itawahusisha waimbaji wa muziki wa bendi, Bongo Fleva, Taarab, Singeli, Wigizaji wa Filamu , Bongo Movie, Komedi , Wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

Safari hiyo itaanza saa moja asubuhi kwa treni ya (TRC) kutoka Kamata jijini Dar es salaam na kupitia maeneo yote ambayo mradi huo unatekelezwa huku wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa mainjinia wa shirika la reli  na wale wa kampuni ya Yapi Merkezi wanaojenga reli hiyo ya kisasa.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )