Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, February 5, 2019

Watumishi wa Umma 827 Wapata Mafunzo Nje ya Nchi

adv1
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Watumishi wa Umma 827 kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wamepatiwa mafunzo nje ya Tanzania mwaka 2017/18 ili kuwapa uelewa, ujuzi na maarifa mapya ya kumudu majukumu yao katika kutekeleza malengo ya Taifa.

Hayo yameelezwa leo, Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kuteuliwa, Mhe. Janeth Masaburi juu ya mpango wa Serikali wa kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo ndani na nje ya nchi kwa watumishi wa Umma ili kuwajengea uwezo na kuleta tija kwa Taifa.

“Serikali imeimarisha ushirikiano wa wadau mbalimbali wa maendeleo hususani Australia, India, Japan, China, Indonesia, Jamhuri ya Watu wa Korea ambapo kupitia wadau hao watumishi 827 walipata fursa za mafunzo ya muda mfupi na mrefu katika nchi hizo,” amesema Dkt. Mwanjelwa.

Aidha, amesema katika mwaka 2016/17 washirika hao walitoa nafasi za mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa watumishi 654.

Amesema, Serikali katika kutambua umuhimu wa kuwapatia mafunzo Watumishi wa Umma ili kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi ilitenga shilingi 54,470, 327,822 kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya ndani na nje ya nchi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2018/19 jumla ya shilingi 39,839,347,632 zimetengwa kwa ajili hiyo.

Sera ya Menejimenti na Ajira ya Mwaka 1999 na marekebisho yake ya mwaka 2008 Kifungu 4.8, Sera ya Mafunzo katika Utumishi wa Umma ya Mwaka 2013 Kifungu 4.2 na Kanuni ya Kudumu za Utumishi wa Umma za mwaka 2009 kifungu G.1 (Vifungu vidogo 7, 9, 10, 11) zinasisitiza kuhusu umuhimu wa kila mwajiri katika utumishi wa Umma kuandaa na kutekeleza Mpango wa Mafunzo wa mujibu wa tathimini ya mahitaji ya mafunzo (Training Needs Assessment).
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )