Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, February 21, 2019

Wilaya Ya Dodoma Mjini Yakamilisha Kusaini Ulipaji Wa Fidia Wa Zaidi Ya Shilingi Bilioni 300 Kwa Wananchi Waliopitiwa Na Mradi Wa Umeme Jua

adv1
Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe.Patrobas Katambi amesema kuwa tayari ofisi yake imeshaidhinisha na kusaini juu ya ulipaji zaidi ya Tsh.Bilioni 300 kwa wananchi wa Michese Dodoma ambao wamepitiwa na mradi mkubwa wa Umeme jua.
 
Akizungumza  na  waandishi wa habari  jijini Dodoma jana   Februari 20,2019  Mhe.Katambi amesema kuwa tayari wananchi wa kijiji cha Michese walishafanyiwa uthamini na nyaraka zote zilishafika ofisini.
 
Aidha Mhe.Katambi amewataka wananchi kuhakiki akaunti zao za kibenki ili kuhakikisha wanalipwa bila dosari yoyote.
 
“Kwa wananchi wa huko Michese ambapo kuna mradi mkubwa wa umeme tayari wananchi wale walishafanyiwa uthamini na nyaraka zao zilishafika kwangu na nilishasaini ”

Katika hatua nyingine Mhe.Katambi amesema kuwa tayari ulipaji wa fidia kwa wananchi wa Chawa umeshaanza ambapo Tsh.Bil.5.7 Zimelipwa na zitafika mpaka  Tsh.Bil.9,kwenye kiwanja cha ndege Tsh.Bil. 3.7 zilishalipwa ,eneo la Mtumba ulipaji ulishaanza  huku  wakala wa majengo Tanzania [TBA ]wako katika mchakato wa kuhakiki  majina kwa watu ambao bado  hawajalipwa.
 
“Ninapozungumza mpaka sasa hivi huko Chawa wananchi wameshaanza kulipwa Bil.5.7  zitafika mpaka bil.9 sidhani kama kuna malalamiko ya ulipaji,ni taarifa tu mnanipa ya kwamba niendee kufuatilia kasi iendelee kwa wale ambao walionekana wanadosari lakini wale ambao hawana dosari ulipaji unafanyika mara moja.”
 
MWISHO.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )