Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, March 20, 2019

CHADEMA Wazungumzia Kumkosa Maalimu Seif...Waahid Kumpa Ushirikiano

Chadema imesema ilitamani kumchukua aliyekuwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, lakini hawakufikia makubaliano, hata hivyo wameamua kushirikiana naye katika chama chake kipya cha ACT Wazalendo.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, naibu katibu mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum  Mwalimu amesema licha ya kumkosa Maalim Seif na kundi lake wataendelea kushirikiana naye kwa kuzingatia mkutano wa vyama vya upinzani uliofanyika Zanzibar Desemba 2018.

"Hakuna pigo Maalim Seif kutokuja kwetu japo kweli tulimtaka, kama kaenda kwa wenzetu ni sawa tu, ni kama hajaolewa mtoto wako kaolewa mtoto wa Baba mdogo ni mulemule, tena kama kaolewa na tajiri utashindwa kuomba chakula?" - Amesema Salum Mwalimu .

Kuhusu nguvu ya Chadema Zanzibar, Mwalimu amesema chama hicho kitaendelea na programu zake, lakini hakitapambana na ACT-Wazalendo.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )