Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, April 16, 2019

Katibu Mkuu CHADEMA Aitwa Kujieleza Mahakamani

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtaka Katibu Mkuu CHADEMA , Dk Vicent Mashinji kuieleza mahakama kwa nini ameshindwa kuhudhuria kesi yake iliyopo mahakamani hapo.

Dk Mashinji ambaye ni mshtakiwa wa sita katika kesi ya kufanya mikusanyiko isiyo halali, inayowakabili vigogo tisa wa chama hicho, ameshindwa kufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa yupo kwenye kesi nyingine iliyopo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea mkoani Ruvuma.

Dk Mashinji ametakiwa kufika mahakamani hapo Aprili 17, 2019  na kuieleza mahakama hiyo sababu za yeye kushindwa kufika mahakamani hapo, wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka.

Dk Mashinji na wenzake wanakabiliwa na makosa 13 likiwemo la kula njama, ambapo wote wanadaiwa kuwa, Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam waliku─║a njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko la kutawanyika.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )