Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, April 8, 2019

Maandamano ya ACT- Wazalendo Yapingwa Marfuku....Polisi Wasema Atayeandamana Atapigwa Hadi Achakae

adv1
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amezuia maandamano ya vijana wa ACT-wazalendo yaliyopangwa kufanyika kesho jijini humo wakilenga kulishinikiza Bunge kuondoa azimio la kutoshirikiana na CAG. 

“Tunazo taarifa pia kuna Chama cha ACT Wazalendo wanasema na Vyama vingine wanakusudia kufanya maandamano tarehe 9, kumshinikiza Spika kufuta azimio la Bunge la kutofanya kazi na CAG, wakiingia barabarani watapigwa watachakaa”-Amesema Muroto 

Muroto amesema kazi za Bunge zinahojiwa ndani ya Bunge na si nje ya Bunge hivyo amewataka wananchi wa Dodoma kuendelea na kazi zao kama kawaida kwani hakuna maandamano yoyote yatakayofanyika.

Licha ya zuio la polisi vijana hao wamesema wataendelea na maandamano kwani ni haki yao.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )