Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, April 7, 2019

Waziri Mkuu Amuwakilisha Raisi Dr John Magufuli Katika Kumbu Kumbu Ya Miaka 25 Ya Mauji Ya Kimbari Rwanda

adv1
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano ambavyo ni tunu walizoachiwa na waasisi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Aprili 7, 2019) katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya Kimbari iliyofanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika kumbukumbu hizo, amewasisitiza Watanzania kudumisha amani na utulivu.

Awali,Waziri Mkuu alijumuika na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo la Gisozi lililopo jijini Kigali.

Baada ya kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu za mauaji hayo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitoa maelezo ya kina kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Rwanda 1994.

Viongozi wengine waliohudhuria kumbukumbu hizo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Ulusegun Obasanjo.

 (mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa .mwenye Tai nyekundu akiwa na viongozi wa mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 katika wakitoa heshima katika eneo la kumbumbu ya mauji ya kimbari Waziri Mkuu  yupo Kigali Rwanda akimuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri wa mambo ya Nje wa Rwanda Balozi Richard Sezibera .aliye mpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigali alipo wasili leo Aprili 7/2019 alipo fika kumuwakilisha  Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 Kkulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Ernest Mangu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dr John Magufuli katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994

PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )