Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, May 14, 2019

Nandy afunguka mipango ya ndoa na Ruge ilivyokuwa

adv1
Msanii wa muziki Bongo, Nandy ameweka wazi kuwa walipanga kufunga ndoa Machi mwaka huu na aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba.

Nandy ameeleza hayo wakati akihojiwa na Ayo Tv na kudai kuwa uhusiano wao ulikuwa wa siri kwa kuwa walikubaliana kulifanya suala hilo kuwa binafsi mpaka watakapokamilisha taratibu zote.

Amesema kuwa mara kadhaa alikuwa akikanusha kuhusu uhusiano huo kwa kuwa waliona hakuna haja ya kuweka wazi.

“Hatukupenda uhusiano wetu uendeshwe na mitandao, tulikuwa tunajaribu kutengeneza njia ya maisha yetu binafsi ili kufikia lengo letu. Hatukutaka life style  (mtindo wa maisha) ya mahusiano ya awali ya Ruge yajitokeze kwenye maisha yetu,”

Akizungumzia namna walivyoanzisha uhusiano wao Nandy amesema, “Nilikuwa napenda sana kumtumia kwenye mawazo yangu japo watu walikuwa wakimzungumzia kuwa mkali ila  alikuwa anapenda sana kunisikiliza na nilikuwa muwazi sana wa vitu vyangu hata vya ndani, nadhani ukaribu tuliotengeneza wa ‘kiboss’ na kiurafiki ndiyo ulitupelekea kuwa katika uhusiano,”.

Aidha Nandy amesema Ruge alikuwa ni zaidi ya mpenzi kwake aliishi naye kama baba na kaka yake na alikuwa akimshauri mambo mengi na mtu pekee aliyekuwa akimshauri katika mambo yake ya muziki na mambo binafsi hata wazo la kuwajengea wazazi wake nyumba lilitoka kwa Ruge.

“Katika kipindi ambacho Ruge alikuwa karibu na mimi na kunipa ujasiri ni wakati ambao video yangu na Billnass ilipovuja mitandaoni, nilikuwa sijazoea matusi ya mitandao ilinipa mawazo sana lakini alikuwa mshauri wangu mkuu.

“Baada ya ile video kusambaa yeye ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuonana na nilimpigia simu alivyopokea hata kabla sijaanza kuzungumza akaniambia najua kila kitu na tuko pamoja katika hili, tuliongea naye kwa simu alikuwa anatoka ofisini hadi akaja nilipokuwa hakukataa,” amesema.

Aidha Nandy amesema kitu kikubwa kilichomvutia Ruge kwake ni jinsi anavyomcha Mungu kwa kuwa mara kwa mara alikuwa akimsisitizia kwenda kanisani hata kama yeye alikuwa haendi.

“Mimi kilichofanya nimpende Ruge ni mkweli na jinsi alivyokuwa ananiongoza katika maendeleo, nakumbuka wakati naanza kuwajengea wazazi wangu aliniambia nataka fedha yote ya kujengea hiyo nyumba niichunge mwenyewe aliniambia anaweza kunisaidia lakini kuna leo na kesho inawezekana tukaachana au nisiwepo,” ameeleza Nandy.

Aidha Nandy amesema kwa kipimdi ambacho Ruge hayupo duniani kinampa wakati mgumu kwani kuna wakati anatamani amtumie hata ujumbe wa simu ila anashindwa kuendelea kupata ushauri wake lakini hata hivyo bado anaendelea kuzitunza baadhi ya jumbe alizokuwa akitumiwa na Ruge enzi za uhai wake.


Itakumbukwa kuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ltd. Ruge Mutahaba alifariki Dunia february 26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )