Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 13, 2019

Ebola Yaua Uganda, Tanzania Yatoa Tamko

adv1
Kijana aliyekuwa na umri wa miaka mitano ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa Ebola, hii ikiwa ni kesi ya kwanza ya maradhi hayo hatari kuthibitishwa nchini Uganda.

Duru za habari zimearifu kuwa, kijana huyo alikuwa akitibiwa katika kituo kimoja cha afya mjini Kasese, katika mpaka wa magharibi wa Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Jana jioni, Shirika la Afya Duniani WHO bila kutoa maelezo ya kina, lilithibitisha kesi ya kwanza ya ugonjwa huo nchini Uganda.

Haya yanaripotiwa chini ya mwezi mmoja baada ya Uganda kutangaza kuwa imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola usiingie nchini humo ukitokea nchi jirani ya DRC, hasa kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kumiminika nchini Uganda.

Hii ni katika hali ambayo siku chache zilizopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema karibu robo ya watu walioambukizwa Ebola huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yumkini hawajui kwamba wanaugua ugonjwa huo hatari.

Tayari Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, imeshatoa taarifa kwa wananchi wake kuchukua tahadhari za ugongwa huo.

“Tumepokea kwa tahadhari ya uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda. Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikichukua hatua za utayari (preparedness) za kukabiliana na ugonjwa huu. Wananchi wasiwe na hofu. Tutatoa taarifa kwa umma siku chache zijazo.” Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )