Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 13, 2019

Kijaji Awataka Watendaji TRA kuwa Karibu Na Wateja Wao

adv1
Na Peter Haule, WFM, Dodoma
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amewataka Mameneja wa TRA wa mikoa na Wilaya  nchini kote kusimamia vema ukusanyaji wa kodi za majengo na kuhakikisha kuwa viwango vinavyotozwa ni vile vilivyoko kisheria.

Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo mjini Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi Mheshimiwa Yahaya Masare, kwamba Mamlaka ya Mapato mkoani Dodoma imempelekea ankara ya kodi ya jengo na kumtaka alipe shilingi laki moja badala ya shilingi elfu 10 zilizoainishwa kisheria kwa majengo ya kawaida.

Dkt. Kijaji ambaye alifika kwenye makazi ya Mbunge huyo, katika Mtaa wa Uzunguni Jijini Dodoma, alibaini kutokuwa na mawasiliano ya kutosha kati ya TRA  na wateja wake jambo lililosababisha malalamiko ya mteja huyo na kuagiza Mameneja wa TRA mikoa na wilaya kuhakikisha wanawafikia wateja badala ya kuwaachia kazi viongozi wa mitaa peke yao.

Awali, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mhe. Yahaya Masare  alimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji kwamba alishitushwa na hatua ya TRA mkoa wa Dodoma kumpelekea ankara hiyo yenye kiwango kikubwa cha madai wakati anafahamu vema sheria ya kodi ya majengo iliyopitishwa bungeni imeainisha viwango vya kodi kwa kila jengo lililoko katika maeneo ya mijini na vijijini

Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma Bi. Kabula Mwemezi, amekiri kuwepo kwa kasoro ya ankara waliyompatia Mbunge huyo na kujitetea kwamba hali hiyo ilitokana na taarifa walizonazo zinazohusu wateja wote wanaomiliki majengo na kwamba suala hilo limepatiwa ufumbuzi

Bi Mwemezi aliwataka wateja wenye malalamiko kuhusu ankara walizo letewa kutoa taarifa kabla hawajalipa ili waweze kupatiwa suluhisho.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )