Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, June 13, 2019

Serikali Kuendelea Kutekeleza Mikakati Ya Kupiga Vita Utumikishwaji Dhidi Ya Watoto

adv1
Serikali imekua na mikakati mikubwa ambayo imesaidia kuwatoa Watoto katika suala zima la utumikishwaji katika kazi na mazingira mbalimbali. 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu 
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Bungeni kuhusu maadhimisho ya siku ya kupiga vita utumikishwaji dhidi ya  

Watoto. Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa  na Dkt. John Pombe Magufuli imekua ikichukua hatua mbalimbali dhidi ya  tatizo hilo. 

“Jamii inatakiwa kutambua maana ya utumikishwaji wa Watoto na kazi  hatarishi zinazowakabili ili kuwa walinzi wa watoto,” alisisitiza Mhagama. 

Aliongeza kuwa Watoto hawatakiwi kutumikishwa bali wasaidiwe kutimiza  ndoto zao kwa kuwaandaa kuwa raia wema na wajenzi wa Taifa la kesho. 

Alieleza juu ya Sheria na mikakati mbalimbali inayosimamia haki za Watoto ikiwemo Sheria ya elimu ambayo inataka Watoto wote kupata fursa ya  elimu, Sheria Na. 1 (2009) ambayo inalinda haki na ustawi wa mtoto,  Sheria Na. 6 (2004) ya Ajira na Mahusiano Kazini inelezea mazingira  ambayo mtoto hatakiwi kutumikishwa kazi ambazo hazipo kwa mujibu wa taratibu.

Pamoja na hilo alielezea pia juu ya mpango ya taifa wa kupiga vita ukatili  dhidi ya Wanawake na Watoto ambao umesaidia katika kuwaondoa Watoto kwenye mazingira hatarishi na Mpango Mkakati wa taifa wa kupambana na  ajira dhidi ya Watoto. 

“Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia viwango vya kazi na imekuwa ikisisitiza  waajiri kufuata sheria za kazi kwa kutowahusisha Watoto katika   mazingingira hatarishi au kwenye kazi zisizo na staha ambazo zinafanya   Watoto waingie kwenye utumikishwaji,” alisema Mhagama 

Aidha, Waziri Mhagama alitoa wito kwa jamii kuwapa Watoto kazi   zinazozingatia umri, ukubwa wa kazi na zinazolinda afya yao. 

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )