Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, September 19, 2019

Aliekuwa Rais wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu Waondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.....Mahakama Yasema Dhamana Yao Iko Wazi

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa dhamana aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu Kaburu baada ya kuondolewa mashitaka ya utakatishaji fedha.

Dhamana hiyo ni kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh.Mil 30, ambapo hatua hiyo inatokana na washitakiwa hao kukutwa na kesi ya kujibu katika mashitaka 8 isipokuwa mawili ya utakatishaji fedha.

Hata hivyo washitakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 20, 2019 kwa ajili ya washitakiwa hao kuanza kujitetea akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zachariah Hans Pope.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amesema jukumu la kuthibitisha shitaka kwa washitakiwa ni la upande wa mashitaka, pia kwa kosa moja moja na sio kwa kutegemeana.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )