Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, September 3, 2019

PICHA: Radi Yaua Ng'ombe 22 Kigoma Wenye Thamani ya Mamilioni ya Pesa

adv1
Ng'ombe  22 wenye thamani ya Tsh.Million 12 wamekufa baada ya kupigwa na radi katika Kijiji cha  Kaziramihunda, Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakati vijana wanaowachunga wakitoka kuwanywesha maji.

Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala  amewataka Wananchi kuwa wavumilivu kwakuwa ni mipango ya Mungu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Martin Ottieno,amesema kuwa tukio hilo lilitokea  Septemba 1, 2019, majira ya jioni wakati Ng'ombe hao wakitoka kunyweshwa maji kijiji jirani, ambapo ghafla ilinyesha mvua kubwa iliyopelekea tukio hilo.

''Ni kweli tukio hilo limetokea na kulikuwa na makundi mawili ya Ng'ombe, kundi la kwanza lilikuwa na Ng'ombe 16  na mmiliki wake anaitwa Abdul kasungu na kundi la pili kulikuwa na Ng'ombe  6 wanaomilikiwa na Filbert Chibedese na walikuwa wanatoka malishoni, ghafla mvua ikaanza kunyesha, radi ikatokea na kuua mifugo yote 22'' amesema Kamanda Ottieno.

Aidha imeelezwa kuwa katika tukio hilo,  hakuna madhara yoyote  yaliyotokea kwa binadamu, hususani waliokuwa wanachunga hiyo mifugo.


 
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )