Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, September 28, 2019

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Amteua Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania Prof. Benno Ndulu Kuwa Mshauri Wake Wa Masuala ya Kiuchumi

adv1
Rais Cyril Ramaphosa  wa Afrika Kusini amemteua Prof. Benno Ndulu kuwa miongoni mwa watu 18 wanaounda Baraza la kumshauri Rais huyo katika masuala ya uchumi litakaloanza kufanya kazi kuanzia Oktoba 01, 2019

Baraza hilo lililotangazwa jana na Rais Ramaphosa litakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha uhusiano mzuri na uthabiti katika utekelezaji wa sera ya uchumi na kuhakikisha kuwa Serikali inaweza kujibu mabadiliko ya hali ya uchumi

Baraza linajumuisha viongozi wa ndani na nje ya Afrika Kusini watakaotoa mawazo ya kiuchumi, wakimshauri Rais na Serikali kwa upana zaidi, kuwezesha maendeleo na utekelezaji wa sera za uchumi zinazochochea ukuaji wa umoja

Pamoja na Prof. Benno Ndulu, wengine ni Prof. Mzukisi Qobo, Prof. Dani Rodrik, Prof. Mariana Mazzucato, Mamello Matikinca-Ngwenya, Dkt. Renosi Mokate, Dkt. Kenneth Creamer, Prof. Alan Hirsch, Prof. Tania Ajam, Dkt. Grové Steyn, Wandile Sihlobo, Dkt. Liberty Mncube, Prof. Fiona Tregenna, Prof. Haroon Bhorat, Ayabonga Cawe, Prof. Vusi Gumede, Dkt. Thabi Leoka na Prof. Imraan Valodia


Prof. Benno   Ndulu alikuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania tangu 2008 hadi 2018 baada ya Rais John Magufuli kumteua Profesa Florens Luoga kushika nafasi hiyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )