Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, September 13, 2019

Waziri Wa Kilimo Hasunga Aicharukia Tume Ya Taifa Ya Umwagiliaji Atoa Maagizo Mazito

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameipa wiki moja Tume ya Taifa ya umwagiliaji kutengeneza mikakati ya kutengeneza mabwawa ya kukinga maji ya mvua ili kuwasaidia wakulima kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kukua.

Mhe Hasunga ameyasema leo tarehe 13 Septemba 2019 katika ukumbi wa ofisi ndogo za wizara ya kilimo Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye kikao kazi na watumishi wa Tume huyo.

Waziri Hasunga amesema kuwa wizara hiyo ina matarajio ya kutumia fursa ya mradi mradi wa umeme wa maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (RHPP) utakaozalisha megawati 2115, kea ajili ya kilimo cha umwagiliaji ambapo inatajwa kuwa kuna zaidi ya Hecta 150,000 zinazofaa kea ajili ya umwagiliaji.

Mhe Hasunga amewataka watendaji hao wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuhakikisha kuwa wanampatia mipango na mkakati wa namna gani baada ya umeme kuzalishwa katika eneo lile, yale maji yatatumika yote katika umwagiliaji na hecta zote zile zianze uzalishaji.

‘’Ninawapa wiki moja hakuna muda mwingine wa kufanya hivyo kwa sababu niliwapa mienzi minne hamjafanya hivyo’’ Alisema Mhe Hasunga

Aidha, Waziri Hasunga ametoa siku tatu kumpatia taarifa za utendaji kazi wa miradi ya umwagiliaji katika mikoa minne yaani Tabora, Katavi, Rukwa, na Songwe iwapo kuna miradi inayofanya kazi na isiyofanya kazi.

Kilimo cha umwagiliaji kimekuwa kikisisitizwa na serikali kwani ni kilimo kisichotegemea mvua hivyo kuwa na matarajio ya kuvuna mazao kwa wingi.

Umwagiliaji ni mtindo wa kilimo wa kupeleka maji kwa mimea shambani pasipo mvua ya kutosha, hutumiwa katika maeneo yabisi au wakati mvua ni kidogo. Katika nchi baridi unatumiwa pia kwa kusudi la kulinda mazao dhidi ya jalidi.

Ni kilimo ambacho kinasaidia sana, kwa mfano nchi ya Misri tangu zamani inategemea mto Naili katika shughuli zake za umwagiliaji wa mazao.

MWISHO
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )