Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, October 4, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Awatimua wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita.....Ni baada ya jana Kuwacharaza vikobo Wanafunzi 14

adv1
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, jana October 4 alichalaza bakora wanafunzi 14, katika Shule ya Sekondari Kiwanja iliyopo Chunya mkoani Mbeya kwa madai ya kukutwa na simu za mkononi jambo ambalo ni kinyume na na utaratibu wa shule

Asubuhi ya Leo Ijumaa, RC  Chamila  amefika tena  katika shule hiyo   na kuagiza wanafunzi wote wa kidato cha 5 na 6  warudi nyumbani hadi Oct 18,2019   kwa kosa la kuchoma Bweni.

RC Chalamila ameeleza sababu ya kuwarudisha wanafunzi hao makwao ni kutokana na kile kinachodaiwa, waliteketeza kwa moto mabweni yao baada ya walimu wao kuwanyang'anya simu, ambapo amewataka warudi, Oktoba 18, huku kila mmoja akipaswa kulipa kiasi cha Shilingi 200,000 na wale waliokamatwa na simu za mkononi, ameamuru walipe  kiasi cha Shilingi 500,000 na warudi shuleni wakiwa na wazazi wao.

"Mliochoma Mabweni, nawaambia kama mna hamu na mnawashwa kuchoma vitu, mkachome nyumba za wazazi wenu. Kuanzia sasa nafunga form 5 na 6, mnaondoka kwenda kwenu, na ikifika saa 4 bado mnang'ang'a hapa, mtakung'utwa kichapo cha kufa mtu na Walimu mnaowafundisha mtaenda likizo kidogo na ninyi wote mtakuja na laki 2 na waliokamatwa moja kwa moja na simu mtakuja na laki 5 na wazazi juu.

"Kwa hiyo Mkuu wa Shule, Afande RPC, Afande OCD, sitaki kuona form 5 na 6, wataondoka watarudi hapa tarehe 18. Na nyie form 4 kama kuna watu watafanya fujo, nitawatimua hata kama mitihani ni kesho, nafuta darasa zima.  - RC Chalamila

Akizungumzia suala la kuwachapa viboko wanafunzi hao 14, Chalamila amesema kuwa yeye ndio bosi wa Mkuu wa shule katika mkoa na hivyo anaowajibu wa kutoa adhabu kwa wanafunzi wote wanaoonesha utovu wa nidhamu shuleni.

"Jana niliwacharaza viboko watoto, wengine wamenijadili kwenye mitandao wakihoji Mkuu wa Mkoa anatoa wapi mamlaka haya. Bosi wa Mkuu wa Shule ni Mkuu wa Mkoa. Sasa kama Mkuu wa Shule anaruhusiwa kuwachapa, basi mimi (Mkuu wa Mkoa) natakiwa niwacharaze sana."- RC Albert Chalamila

Aidha RC Chalamila ameongeza kuwa hakuna mwanafunzi yeyote atakayeruhusiwa kuhama shule,hadi pale atakapokuwa amekamilisha kulipa kiasi hicho cha pesa na kuuagiza uongozi wa shule, kuhakikisha ujenzi wa mabweni hayo unaanza mara moja pindi pesa hizo zitakapoingizwa kwenye akaunti ya shule.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )