Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 11, 2019

Mfungwa Aliyesamehewa na Rais Magufuli Agoma Kutoka Gerezani

adv1
Merad Abraham ambaye ni miongoni mwa wafungwa 70 waliosamehewa na Rais Magufuli jana Disemba 9, amekataa kuondoka katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya akidai hana mahala pa kwenda huku akijijeruhi usoni kwa jiwe kwa nia ya kutaka arejeshwe Gereza la Ukonga Dar es Salaam.

Meradi ambaye alifungwa kwa kesi ya kubaka alihukumiwa kutumikia kifungo cha miaka 30 jela, Juni 20, 2000 na alitakiwa kumaliza kifungo Juni 20, mwakani.
 

Mfungwa huyo alijijeruhi baada ya mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila kuondoka  katika gereza hilo baada ya kushuhudia  wafungwa 70 kati ya 259 wa gereza hilo wakikamilisha taratibu za kutoka.

Abraham alirejeshwa katika gereza hilo licha ya kujijeruhi na kusubiri utaratibu wa kutoka


adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )