Showing posts with label diamond. Show all posts
Showing posts with label diamond. Show all posts

Monday, November 11, 2013

Diamond amchana Wema Sepetu.... Amwambia kuwa kama ana ndoto ya kuolewa na yeye basi anajidanganya


RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alifunguka kuwa kwenye maisha yake ya ndoa atakayoingia siku chache zijazo, aliyekuwa mchumba wake wakamwagana na kurejeana hivi karibuni, Wema Sepetu asitegemee kuolewa naye. 
 
Diamond ambaye ni staa wa Bongo Fleva aliyasema hayo mbele ya mwandishi wetu   Novemba 7, mwaka huu jijini Dar kufuatia kuulizwa anamchagua nani wa kumuoa kati ya Wema Sepetu na mchumba wake wa sasa, Penniel Mungilwa ‘Penny’.
 
Swali kwa Diamond liliibuka baada ya kuzagaa kwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii kwamba yu mbioni kumvisha pete ya uchumba mmoja wa mademu zake.
 
Swali hilo lilimfanya Diamond afunguke kwa kusema kwamba anachokijua yeye na ambacho kipo kwenye mikakati yake, mke wake mtarajiwa ni Penny.
 
“Najua wengi wanahisi mimi ninaweza kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kutokana na dini yangu kuruhusu lakini jambo hilo mimi silifikirii hata kidogo kwa kuwa kwenye maisha yangu nilishapanga nitaoa mke mmoja tu,” alisema Diamond.
 
Akaendelea: “Watu wanasema mengi juu yangu na Wema, wengi wao hawajui nafsi yangu inataka mwanamke yupi, ninachoweza kusema na watu wakasikia na kunielewa basi wajue kwamba Penny ndiye mke wangu, Wema asitegemee kuolewa na mimi.”

 
Diamond alikwenda mbele zaidi kwa kumwanika Penny kwamba ana sifa ya kuwa mke kwani ni mvumilivu sana na anaonesha upendo wa dhati kwake.
 
“Kwa maana hii basi hakuna mwanamke mwenye jina  kubwa wala sura nzuri zaidi ya Penny ninayeweza kumwita mke wangu. Najua kila mtu ana namna yake ya kuchagua ampendaye, ndiyo maana utaona watu wanasema hili mara lile, lakini hawajui nafsi yangu inataka mwanamke wa aina gani,” alisema Diamond na kuongeza:
 
Kama kuna demu anayejipa matumaini hayo basi asitegemee hata siku moja kwa sababu kuoa kwangu kutazingatia mke mwema na si bora mke, Penny pekee ndiye mwenye sifa za kuwa mke wangu,” alisema Diamond.

Credit-Global publisher
HABARI KAMILI..>>>

Thursday, July 18, 2013

DIAMOND "AWAPA MAKAVU" WATU WANAOCHUKIA MAFANIKIO YAKE....Inaonekana Diamond amechoshwa na haters wanaosubiri aanguke kimuziki na kumcheka...


Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameamua kutupia picha inayomuonyesha akianguka kutoka juu (angani) na kufikia chini kwa kichwa kwenye barabara ya lami. 


Picha hiyo ilisindikizwa  na maelezo yanayosema , "Najua hiki ndio mnachokisubiri, kwahiyo endeleeni kusubiri"...# Haters
HABARI KAMILI..>>>

Wednesday, July 17, 2013

"SIWEZI KUMUOMBA MSAMAHA DIAMOND KWENYE TWITTER"...PREZZO


Rapcellency, Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kwakuwa anaamini hakuna alichomkosea na ni jambo la kitoto.

Akiongea jana  mchana kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen, kinachoendeshwa Mzazi Willy M. Tuva, Prezzo amesema Diamond ndiye aliyemchokoza baada ya wasanii hao kutumbuiza mwanzoni mwa mwezi huu kwenye tamasha la Matumaini.

 Prezzo anadai aligundua kuwa Diamond alimponda kwenye magazeti ya Tanzania kuwa hamwezi kwa lolote kwenye muziki.


“Mimi sipendi kuwa na adui kwa sababu muziki unafaa kuleta muungano, sa me nikashangaa mbona huyu brother ananiingilia na huku sikumbuki kumkosea wala hatujawai kukutana ana kwa ana,” alisema Prezzo.


“Mtu yeyote anamjua Prezzo ni kama rattle snake, ukimchokoza you have to get prepared to be bitten.”

Rapper huyo aliendelea kudai kuwa alimpigia simu Diamond lakini hakupokea na ndio maana aliamua kumdiss kwenye Twitter.
 
“Jamaa hakupokea simu nikaona ah! Basi liwalo na liwe, nikadecide ku-air my views.”


Hata hivyo Prezzo amesema hawezi kumuomba msamaha Diamond kwenye Twitter kama anavyomtaka afanye.
 
“Unaona kwa saa hizi akianza kusema aende kwa Twitter aniombe msamaha, maisha huwa hayaendi hivo…kwa hivyo vitu vingine naona ni kama ni utoto unaingilia kati, kwani yeye kusema niombe msamaha kwa Twitter….niombe msamaha kwa kosa gani? Kusema ukweli,unajua mimini msema ukweli, mimi kuomba msamaha kwa Twitter naona kidogo ni utoto.”


Hata hivyo Prezzo amesema hataki beef na Diamond kwasababu anamheshimu na amemshukuru Willy Tuva kwa kujaribu kuwasuluhisha.
 
Source: Mambo Mseto (Radio Citizen), Ghafla Kenya
HABARI KAMILI..>>>

Tuesday, July 2, 2013

HAYA NDO MAMILIONI YA PESA ALIYOINGIZA DIAMOND KWENYE SHOW ZA MWEZI ULIOPITA ....

 

Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi.

Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.
 
Show ya nchini Comoro 22 June
Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38.
 
Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June
Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15.

Show ya Tigo Mwanza 30 June
Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10.
 
Kili Music Tour 2013
Tulipata taarifa kuwa Diamond atafanya show kwenye mikoa minne na kwamba amelipwa shilingi milioni 50 kwa show zote.
 
Show ya Matumaini 7 July
 kwenye hii show diamond ana zaid ya mil.10

Show ya Kenya 27 July
Kwenye show hii Diamond atashare stage na mastaa wa Nigeria, Ice Prince na Davido na hapa kama alivyosema kuwa katika show za nje ya nchi huwa hachukui chini ya dola 15,000. Kuna uwezekano hapa akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 20.
 
Kama una calculator basi unaweza ukapiga hesabu mwenyewe ni kiasi gani ameingiza kwa show za June na July. Kumbuka pia kuwa show zote hata za July tayari ameshasaini mkataba na ameshalipwa chake tayari. Kitu kama milioni 140 na usheee!!
 
Pia kumbuka ni balozi wa Cocacola na hulipwa kila mwezi kwa shughuli zinazohusiana na deal hiyo. Katikati wa mwezi July pia kuna uwezekano akawa na show zingine kibao.
 
“Siku zote ishi ukikumbuka, Maisha ni Vita, vita ambayo mwisho wake ni siku ya wewe kuingia kaburini, hivyo haupaswi kuchoka wala kukata tamaa.Heshima, Juhudi na Maombi ndio nguzo pekee zitazokusaidia wewe kushinda Vita hii… tambua Mwenyezi Mungu ndiye Muweza na Mpaganga wa yote,” anasema Diamond.
HABARI KAMILI..>>>

Friday, June 28, 2013

NAY WA MITEGO NA DIAMOND KUJA NA NGOMA MPYA..."SALAMU ZAO"


Baada ya kutamba na Muziki Gani, Diamond na Nay Wa Mitego wako mbioni kuachia ngoma nyingine hivi karibuni baada ya kupembua ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’.

Nay ameiambia mpekuzi kuwa kuna nyimbo tatu ambazo zipo tayari, Salamu Zao, Kwa Masela na Utakula Jeuri Yako, hawajajua ipi itaanza kutoka kwasababu kila mmoja yupo katika tour zinazoendelea. 


Wamesema wakikaa wakashauriana na wadau mbalimbali ndipo watakapoamua mzigo upi uingie mtaani kwanza.

“Kuna kazi ambazo zinakuja hivi karibuni ambazo nimefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi sijajua ni ipi ambayo itaanza kutoka lakini tutawaita wadau wachague ipi ianze kati ya ‘Salamu Zao na Kwa Masela’ ambazo zipo tayari na ‘Utakula Jeuri Yako’ nimefanya mwenyewe...


"Ilibidi tutoe nyimbo ambayo tumefanya na Diamond lakini mpaka sasa hivi hakuna maamuzi ya moja kwa moja tuitoe au kila mtu atoe ya kwake au tutaendelea na project yetu iliyoendelea, kwahiyo wadau wakae mkao wa kula,” amesema Nay.
HABARI KAMILI..>>>

Thursday, June 27, 2013

DIAMOND PLATNUMS KUPERFORM JUKWAA MOJA NA WAKALI WA NIGERIA NCHINI KENYA MWEZI UJAO

Ni ukweli ulio wazi kuwa star wa ‘Kesho’ Diamond Platnumz ‘anaweza’ kuwa msanii wa Tanzania anayefanya show nyingi zaidi kwa sasa na za gharama kubwa, baada ya kuwachanganya mashabiki wa Comoro na crew yake ya Wasafi weekend iliyopita sasa anategemewa kushare jukwaa moja na wakali kutoka Nigeria Davido na Ice Prince jijini Nairobi mwezi July.

Diamond Platnumz kipenzi cha mabinti ataungana na star wa Nigeria hit maker wa ‘Dami Duro’ Davido, Ice Prince, Victoria Kimani wa Kenya, na wakali wengine katika ‘Boombaataa Festival’.


Mtandao wa Ghafla umethibitisha ushiriki wa Diamond katika show hiyo kubwa ambayo hufanyika mara moja kwa mwaka nchini Kenya, yenye lengo la kuleta burudani ya utofauti kwa wanamuziki wa Afrika, fashion pamoja na utamaduni.

Show hiyo inategemewa kufanyika (July 27) mwaka huu Nairobi, Kenya.
HABARI KAMILI..>>>

Saturday, June 22, 2013

MIMBA YA PENNY NA DIAMOND YATOKA


TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja....

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
 
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.


Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.


Baada ya kupata habari hizo, mwandishig wetu alilimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:

Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?

Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine? 

Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.

Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
 
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.

Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine? 

Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

Credit: GPL
HABARI KAMILI..>>>

Tuesday, June 11, 2013

KUNDI LA MATAPELI WANAODAI KUTOA MIKOPO BILA RIBA WAVAMIA ACCOUNT ZA DIAMOND NA KUTOA UJUMBE HUU...


Kundi la matapeli wanaojiita Saving Foundation leo wameihack akaunti za Facebook na Twitter za Diamond na kuandika ujumbe unaoonekana kama umeandikwa na Diamond.
  
Amepigiwa  simu  Diamond ambaye hakuwa na taarifa zozote kumuuliza kama ni yeye ndiye aliyeandika na amekanusha kuandika ujumbe huo.

Ujumbe huo kwenye akaunti ya Facebook ya Diamond unasomeka:
Screenshot - 6_11_2013 , 6_16_56 AM
Matapeli hao pia wamewahi kutumia majina ya Zitto Kabwe na Ridhwan Kikwete kufanya utapeli huo.

Mtaalam mmoja wa masuala ya IT amedai  kuwa matapeli hao wamejipanga na wana mtandao mkubwa.
HABARI KAMILI..>>>

Wednesday, June 5, 2013

MAMBO 10 KUHUSU DIAMOND LIKIWEMO LA KUMILIKI ZAIDI YA BILIONI MOJA KATIKA ACCOUNT YAKE

1. Ana utajiri unaozidi shilingi bilioni 1.

2. Yupo kwenye mazungumzo na promoter wa Rwanda kufanya show moja ya uwanjani ambayo anaweza kulipwa dola 120,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 190.

3. Malipo ambayo hupokea kwa show zake nyingi za nje ya nchi hayashuki chini ya dola 25,000.

4. Tangia mwaka 2011 mwishoni akaunti yake haijawahi kushuka chini ya shilingi milioni 100.

5. Anamiliki nyumba kadhaa alizopangisha.

6. Wimbo Mawazo alimwandikia Jacqueline Wolper ambaye alikuwa mpenzi wake.

7. Kamwambie na Mbagala alimwambia mpenzi wake aitwaye Sarah aliyemkataa (Diamond) sababu hakuwa na uwezo.

8. Ukimwona alimwandikia Wema Sepetu baada ya kumsaliti.

9. Ili kuvunja mkataba na aliyekuwa meneja wake Papa Misifa, ilibidi amlipe shilingi milioni 18.

10. Ana timu (anayoilipa mshahara) ya watu zaidi ya 12 wakiwemo dancers, mtu wa mavazi, msaidizi wake, wapiga picha wawili nk.

Credit: bongo5
HABARI KAMILI..>>>

Thursday, May 23, 2013

DIAMOND ATIA AIBU YA MWAKA....KINGERZA CHAMUUMBUA TENA

KWANZA  NAANZA  KWA  KUMPONGEZA  SANA  DIAMOND maana  akiwa hajamaliza hata wiki mbili tangu atoke kwenye tour iliyofanikiwa ya Burundi na Congo, Diamond leo amesaini mkataba wa show nyingine kubwa ya kimataifa.

Kupitia Instagram, Diamond ameshare picha inayomuonesha akisaini mkataba wa show huku pembeni akiwepo mtu mwenye asili ya Asia ambaye huenda ndio promoter. 

Kilichowafanya  mashabiki wake  huko instagram  wavunjike  mbavu  ni Kingereza  alichotumia.....
"After I DONE did the Uk,Congo,Burundi…guess where next I’ll be headed.”...

Haijalishi  umekosea au upo  sahihi, ujumbe  umefika  kaka!!.  Waache  wacheke, wataacha  tu.

 Hata  hivyo, si vibaya pia  kutumia  lugha  yetu ya kiswahili  maana  ujumbe  hufika  vizuri  zaidi....Kingereza lugha ya  watu...ni ngumu..!!! 
HABARI KAMILI..>>>

Saturday, May 4, 2013

"HAKUNA ZAWADI KUBWA NILIYOPEWA NA MUNGU ZAIDI YAKO DIAMOND...NAKUPENDA SANA"......PENNY


Pengine  utundu  wa Diamond  ndo  kitu  pekee kinachowafanya  akina  dada  wamgombanie..Leo ni birthday ya Penniel Mungilwa na mpenzi wake Diamond Platnumz, amemwandikia maneno matamu.
 

“Sometimes I wish you could know how much you mean to me…its a lot’..fu***n a lot, I can’t even explain it.. It’s even more than money… sometimes I don’t even know how to col u, a wife, friend,sister,bedmate, partner.. Ooh God! I don’t know coz you are more than dat,”

“Siku zote umekuwa mwema, mkarimu,mpole,nidhamu na mwenye mapenzi tele juu yangu…. You always should keep this in your mind “I LOVE YOU SO MUCH”… Happy birthday Darling.”ameandika Diamond

Kwa maneno haya, hakuna msichana anayeweza kujizuia kulia kama akiambiwa na mpenzi wake.


 Baada ya kuona ujumbe huo ulioandikwa na Diamond kwenye Instagram, Penny amejibu:


“Baby u just made me cry!! Oh God Naseeb I luv u so much hubby…wallahi sina hata cha kujibu to make u understand How I appreciate ur sweet luv,God has given me so many things but bringing u in my life is the best gift I have received…U just made my day,years,a lifetym…I wont forget this…thank u hubby.”


HAPPY BIRTHDAY PENNY.
HABARI KAMILI..>>>

Friday, April 26, 2013

DIAMOND AWATAKA MADEMU WA LONDON WAJIPENDEKEZE ILI ACHAGUE WA "KUMKANYAGA"


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ anaendelea kutunisha akaunti yake baada ya kulamba shavu la shoo za kutosha nchini Uingereza ambapo ameahidi kurejea Bongo na mchumba rasmi atakayemtambulisha kwa mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’.
  
Mkali huyo wa ngoma ya Kesho alifunguka hayo juzikati kupitia website yake alipokuwa akizinadi shoo hizo atakazofanya kwenye majiji ya London na Reading, Uingereza ambapo aliwataka warembo hasa Wabongo waishio humo kupendeza ili achague mmoja atakayekuwa mchumba’ke.

Bila kujali mjadala utakaoibuka kwa kuwa tayari ana mchumba ambaye ni Penniel Mungilwa ‘Penny’, Diamond alifunguka: “Mashabiki wangu wa London na Reading kijana wenu nakuja kuweka historia kwa mara nyingine. Warembo mpendeze nakuja kuchagua mchumba mmoja wa kuja kumtambulisha kwa mama Diamond.”
HABARI KAMILI..>>>

Saturday, April 20, 2013

"HAKUNA MWANAMKE KWENDA KWENYE SHOW YA DIAMOND HUKO LONDON"......MANGE KIMAMBIBaada ya Diamond kusambaza clip ambayo inasikika Wema Akiongea nae ambayo Diamond Amesema kuwa Wema Alikuwa anajitongozesha...Mange Kimambi Ametoa Wito kwa wanawake wote walioko London Kutokwenda show ya Diamond akienda kufanya Show huko kwa vile alimzalilisha mwanamke mwanzao....


"Alafu bado utaona kunamijanamke huko London itavaa kabisa nguo na kujipaka ma makeup kwenye kumkatia Diamond viuno kwenye show... Ladies lets stand together...
tutadhalilishwa mpaka lini na hawa watu.....Embu tuonyeshe mfano hapa......HAKUNA MWANAMKE KWENDA KWENYE SHOW YA DIAMOND HUKO LONDON..
 
ATAKAE KWENDA NTUMIENI PICHA YAKE HUMU TUMJUE.......ILA GUYS Seriously huyu jamaa kavuka mipaka tumfanye mfano kwa wenzie" Mange Kimambi

HABARI KAMILI..>>>

Thursday, April 18, 2013

DIAMOND AFANANISHWA NA MWANAUME MSHAMBA, LIMBUKENI NA ALIYEKURUPUKIA MAPENZI UKUBWANI

KAMA USHAMBA NI SOMO BASI MFANO NI HUU HAPA!!!.

USHAMBA. Binafsi namshabikia sana huyu Msanii but I cant take it anymore!, Awali ya yote tuelewe kwamba kumdhalilisha mwanamke yeyote na kwa namna yoyote ni sawa na kumdhalilisha mama yako mzazi!,

Mambo ya kuanza kurekodiana kwenye maongezi yaliyo private na kuyasambaza binafsi naona ni kuvuka mipaka na Ushamba uliopitiliza,

DIAMOND unaimba nyimbo nzuri za mapenzi lakini sasa una-prove Ushamba juu ya Mapenzi yenyewe,kifupi hakuna mtu anayekulazimisha uwe na mrembo gani kimapenzi kwani wewe ni mtu mzima maliza wanawake wote duniani ikiwezekana tembea mpaka na Mamba wa kwenye Mabwawa,hiyo ni hiari yako, ila unapopeleka hewani sauti ya maongezi private na wema aidha kwa kutafuta kuongeza umaarufu,this is rubbish!!!,

Kwa haraka haraka ukimsoma diamond unagundua kuwa ni wale wanaume ambao hawakuwahi kubahatika kupendwa na wanawake wazuri,sasa wanapokuja kushika pesa au umaarufu ndio inakuwa siraha yao ku prove kwenye jamii kwamba hata nao wanaweza.

Yaani Diamond kushobokewa na madem wazuri kwake ni kama ngekewa ndiomaana anaingia kichwa kichwa.

PENNY usisahau kwamba huyu wema alikuwa rafiki yako na ukamchukulia Bwana,tena bwana mwenyewe ni huyu mtoto wa kiswazi ambaye Mapenzi yanampeleka puta!,anayedhihirisha ulimbukeni wake kwenye jamii.
 
Leo kwa ushirikiano wako na Diamond umemuanika msichana mwenzako kumdhalilisha,ok tia maji kichwa chako hii ni Bongo soon utanyolewa na tutaandika hapa hapa.

WEMA, Sasa ukae chini ujifunze kwamba mitoto ya Kiswazi mingi milimbukeni,wewe ni binadamu na hujakamilika basi jaribu kujikamilisha kwa kupunguza makosa,sina maana ya kwamba nakutetea wewe bali binafsi sipendezwi na KUDHALILISHWA KWA MWANAMKE YEYOTE!

KIOO CHA JAMII :
Hapa hakuna kioo,ni heri kuzamisha sura kwenye tundu la choo ukiamini kwamba utaiona taswira yako kuliko kuwapa dhamana wasanii malimbukeni. 
Credit: Sheria ni Msumeno
HABARI KAMILI..>>>

Monday, April 15, 2013

"HIVI MAMBO YA DIAMOND INA NINI MPAKA INAGOMBANIWA???.....DIAMOND NAOMBA PENZI LAKO NA MIMI NIJIONEE"...HILDA NDEMA

 Katika  hali  ya  kushangaza, binti  mmoja  maarufu  kwa  jina  la  Hilda  amejitokeza   hadharani  kupitia  facebook  yake  na  kudai  kuwa  yupo  tayari  kugawa  penzi  kwa  diamond  hata  bure  ili  naye  ajionee  kinacho wafanya  wanawake  wenzie  wamgombanie...

Huu  ni  ujumbe  wake

"Hey tsup..!! Diamond  nipe  penzi  lako  nionje  kinachofanya  kila  mwanamke  akung'ang'anie  na  kukutaka..

nataka  kujua  ni  ufundi  ama  una  mashine  kubwa  au spe*m zako  zina almasi???.. c'moon plutnumz  give me a chanche to one nite

Wema,Wolper,Uwoya,Aunt Ezekiel ...haiwezekani....Mwanaume unacho cha ziada siyo bure...

Nahitaji any time na popote.nitakuvulia chupi bila hofu.take my body right now bro..."
HABARI KAMILI..>>>

Wednesday, April 10, 2013

"JAPOKUWA SIJAONA MSANII ANAYENIFIKIA KWA HELA NINAYOPATA KWENYE RINGTONE LAKINI UKWELI NI KWAMBA WASANII TUNANYONYWA"...DIAMOND


Suala la wasanii kunyonywa na makampuni ya simu kwenye mauzo ya ringtone linamuuma kila msanii, hata Diamond ambaye ndiye msanii anayeingiza fedha nyingi zaidi kuliko yeyote Tanzania katika biashara hiyo.


Jana kupitia Instagram, aliandika kilio chake:

Dah! hivi kweli Serikali imekosa majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya biashara ya ringtones..!? Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu kwa Mda mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi, kisha wanatudump baada ya kufanikiwa kwenye uchaguzi wao, bila kujali thamani na Mmhango wetu kwao.

Hata hivyo kuna watu wanaoamini kuwa Diamond hapaswi kulalamika kwakuwa ndiye msanii anayefaidi zaidi matunda ya muziki Tanzania.

Mmoja wa followers wake aitwaye Princestepp aliandika: Hupaswi kulaumu wewe maanake kati ya wasanii wachache walioweza kula hela za watanzania chini ya ya serikali ya rais wetu Kikwete ni wewe acha unafiki wasanii wengine ambao hawajapata fursa kama yako walaumu vipi sasa?

Diamond alijibu: Mi nimekula pesa na bado nakula pesa kwa juhudi zangu za kujituma jukwaani na kufanya show nzuri, sio kuwa naitwa kupewa pesa za ringtones nah! Napewa show…. So nikiwa kama mfano mzuri kwa wasanii lazima niwe mstari wa mbele kupigania haki za wasanii kiujumla. 

Aliongeza, “Mi napigania haki zetu upande mwingine wananiona snitch.. wakati mi naamini katika wasanii wote japo nadhulumiwa lakini hakuna hata anayefikia hela nnayolipwa kwa rintones.. ila naona haiwezekani kwanini watufanye wajinga watu wapewe haki zao.”
HABARI KAMILI..>>>

Sunday, March 31, 2013

"MI NAJITUMA KWA BIDII..Q-CHIEF ANAKAA NA KUVUTA BANGI HALAFU ANADAI NATUMIA NYOTA YAKE....NAOMBA ANIKOME"...DIAMOND


Hii  ni  kauli  ya  msanii Diamond kuhusu Q chief: mi nafanya kazi, mazoezi na dancers, nahangaika kutafuta sare, kuandika nyimbo nzuri, wakati nafanya yote hayo we unakula unga, halafu unakuja kusema nasafiria nyota yako, nisafirie nyota ya mla unga? mi staki, staki, agombane na wakubwa wenzake kina dully mi aniache na wadogo wenzangu staki...?
HABARI KAMILI..>>>

Saturday, March 23, 2013

" MIMI NI MTI WENYE MATUNDA MILELE....SIOGOPI KUPIGWA MAWE"... HUU NI UJUMBE WA DIAMOND


MSANII wa muziki wa bongo fleva Diamond Platinam ameendelea kujinadi kupitia mitandao ya kijamiii huku akiteka hisia za mashabiki wake kwa kutuma baadhi ya picha zinazomuonyesha akiwa jukwaani akifanya 'makamuzi' pamoja na kutuma ujumbe wa kujipongeza kwa kazi anayoifanya

Kupitia mtandao wake wa 'Instagram' msanii huyo alituma ujumbe uliosomeka hivi "Mimi ni mti wenye matunda milele siogopi kupigwa mawe"

Ujumbe huo ulionekana kuteka baadhi ya mashabiki wake huku wengine wakituma ujumbe za kumpongeza kwa kuwa na imani hiyo huku akionyesha kutoteteleka kwa jambo lolote linalomkabili ambalo linaonyesha kutaka kumdondosha kimuziki

Maneno ya ujumbe huo pia umeonekana kutumiwa katika nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la 'Muziki gani' ambayo wameshirikiana na msanii Ney wa Mitego


Credit: PRO-24
HABARI KAMILI..>>>

Thursday, March 14, 2013

DIAMOND AMTIA MIMBA PENNY NA KUAMUA KUMZAWADIA GARI LA MILIONI15


Kupitia segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto wake mtarajiwa.

Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa sasa ni mjamzito.

Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”

Alipoulizwa kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu “siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “
HABARI KAMILI..>>>

Wednesday, March 13, 2013

Huyu Ndio Msanii Anaye Ongoza Kulipwa Hela Nyingi Kutokana na Ringtones za SimuMwanzilishi wa kampuni ya Push Mobile inayohusika na uuzaji wa miito ya simu, ringback tone (RBT) amesema Diamond ndiye msanii wa Bongo Flava anayeingiza fedha nyingi zaidi.

Shamte ametoa taarifa hiyo jana alipokuwa akizungumza kwenye kongamano la mchango wa technolojia ya habari na mawasiliano ICT kwenye tasnia ya muziki nchini katika kituo cha ubunifu wa technolojia hiyo cha KINU jijini Dar es Salaa

"That boy is hot, you have no idea how much money he makes from RBT, I handle that account true story,” alisema Rashid. Alipoombwa ataje ni kiasi gani Diamond anaingiza kutokana kuuzwa kwa nyimbo zake, Rashid alisema, “lots… let’s just say he is happy.” Lakini Shamte alisema kama angekuwa na umaarufu kama Diamond alionao angeingiza fedha nyingi zaidi kuliko sasa.

“If I was hot like Diamond trust me I would be rich and I would not need to have anybody manage me or anything, I would put up a website, I would put snippets of all of my tracks because I can’t really make any money from radio, I would dump a bunch of songs onto radio, I will make sure you can stream a little bit of it but if you want all of it, I will make you pay me 200 using M-Pesa, if you want to download it I will make you pay me a hundred using M-Pesa.”
HABARI KAMILI..>>>