Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts
Showing posts with label habari za kitaifa. Show all posts

Thursday, April 17, 2014

Mwanafunzi wa chuo cha IFM akamatwa na Bangi kilo 50


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia abiria wa tatu waliokuwa wakisafiri na Basi la New Force kutoka Kahama kuelekea Jijini Dar es Salaam.Wanaoshikiliwa ni Kevin Prospar(aliyekaa pichani kulia),Joseph Charles (aliyekaa kulia) na John Joseph(aliye kaa katikati)
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime kushoto akikagua bangi iliyo kamatwa.
Basi la New Force lililokamatwa likiwa limebeba abiria waliokuwa na bangi likiwalimeshililiwa kwa muda Makao ya Polisi Mkoa wa Dodoma.
 *********
By Geofrey Adroph via Pamoja Pure blog -- Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watu watatu kwa kosa la Kupatikana na bhangi kiasi cha Kilogramu 133.5 yenye thamani ya Ths. 20,025,000/= bei ya mitaani (street value).
 
Watuhumiwa hao wamekamatwa mnamo tarehe 16/04/2014 majira ya 7:30 mchana eneo la Stendi Kuu ya mabasi katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma. 

Watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bhangi katika mabegi baada ya kupanda basi kutokea Kijiji cha MANONGA – TINDE Mkoani SHINYANGA kwenda jijini Dar es Salaam katika basi namba No. T.931 CGU mali ya kampuni ya NEW FORCE linalofanya safari zake kutokea Kahama kwenda jijini Dar es Salaam. 
 
Watu hao walifahamika kwa majina ya:-
  1. CALVIN S/O PROSPER SALEKA, miaka 23, kabila Mchaga, Mwanafunzi wa chuo cha Institute of Finance Management (IFM) cha Dar es Salaam, mwaka wa pili, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 51kgs.
  2. JOHN S/O JOSEPH, Miaka 31, kabila Msukuma, mkulima na mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam, alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito wa 42.5kgs.
  3. JOSEPH S/O CHARLES BATONI, Miaka 22, kabila Msukuma, mkulima na mkazi wa Shinyanga. alikamatwa akiwa na mabegi mawili ya bhangi yenye uzito 36.5kgs
Watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa za raia mwema aliyewatilia mashaka na kutoa taarifa Polisi. Mbinu waliyotumia kusafirisha ni kuhifadhi katika mabegi makubwa ya nguo na kufunga kwa mifuko ya nailoni kisha kusaga vitunguu na kuweka katika mabegi hayo pamoja na kupulizia manukato (perfume) ili kuondoa harufu wasiweze kugundulika kirahisi.

Tukio lingine katika kijiji cha Central Kiteto Tarafa ya Mlali Wilaya ya Kongwa zilikamatwa lita 300 za Pombe haramu ya Gongo nyumani kwa Salumu s/o Chamagulu ambaye alikimbia baada ya kuona Polisi na tunaendelea kumtafuta.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David A. Misime – SACP, anawapongeza kwa dhati raia wema wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuendelea kudhibiti madawa ya kulevya na Pombe ya Moshi inayoharibu vijana wengi.
HABARI KAMILI..>>>

Magazeti ya leo Alhamisi ya tarehe 17 April 2014

 
 
 
 
 


 

 

 

 

 

 

 

 

 


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Magazeti  ya  leo  Alhamisi  ya  tarehe  17  April  2014

HABARI KAMILI..>>>

Bunge maalumu la Katiba kuendelea leo licha ya baadhi ya wajumbe ( UKAWA ) kususia kikao hicho jana jioni


Vikao vya Bunge Maalum la Katiba vitaendelea tena leo kwa kujadili sura ya 1 na ya ile ya 6 ya Rasimu ya Katiba licha ya baadhi ya wajumbe kususia kikao hicho jana jioni na kutoka nje ya ukumbi kwa kile walichodai ni kuchoshwa na matusi, dharau na ubaguzi .

Kauli ya kuendelea kwa kikao leo ilitolewa usiku wa jana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Federick Werema  kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha jioni cha Bunge hilo, wakati aliposimama kutoa hoja ya kutengua Kanuni za Bunge Maalum la Katiba ili kuongeza muda wa kujadili sura hizo, kutoka 3 hadi siku saba.

Kabla kutengua, Werema alisema mizaha katika Bunge hilo haina tija, hivyo kususia kwa baadhi ya wajumbe hakuzuii kuendelea kwa majadala huo.

“Ninawaomba waliokubali kuendelea na mjadala huu tuwahi kesho,” alisema Jaji Werema.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samia Suluhu Hassan aliwataka wajumbe hao kuwahi mapema saa 3:00 asubuhi ili kuendelea na kikao.

Kuhusu ombi la mwongozo kutoka kwa mjumbe wa Bunge hilo, Mwigulu Nchemba kuhusu kitendo na hatima ya wajumbe waliosusia kikao na kutoka nje, Makamu Mwenyekiti huyo alisema itajulikana baaada ya Kamati ya Uongozi wa Bunge Maalum la Katiba kukutana.
HABARI KAMILI..>>>

Taarifa ya TAHADHARI ya mvua kubwa katika Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na Dar es Salaam.


Taarifa kwa Umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa.

Taarifa Na.
201404-02

Muda wa Kutolewa
Saa 10:00 Alasiri

Saa za Afrika Mashariki
Daraja la Taarifa:
Tahadhari

Kuanzia:
17
Aprili, 2014

Tarehe
Mpaka:
18
Aprili, 2014

Tarehe

Aina ya Tukio Linalotarajiwa
Vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24,

ukanda wa pwani.


Kiwango cha uhakika:
Wastani (70%)
Maeneo yanayotarajiwa
Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na mikoa ya Tanga, Pwani na

kuathirika
Dar es Salaam.

Kuimarika kwa ukanda wa mvua Inter-tropical convergence zone

Maelezo:
(ITCZ)” ambao umeambatana na ongezeko la unyevunyevu na


kuwepo kwa ‘Easterly Wave’.

Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari pamoja na

Angalizo:
mamlaka zinazohusika na maafa, wanashauriwa kuchukua tahadhari


stahiki.

Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa

mrejeo kila itakapobidi.


Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
HABARI KAMILI..>>>

Wednesday, April 16, 2014

Wajumbe wa Bunge la Katiba toka vyama vya upinzani leo jioni waligoma na kutoka nje ya Ukumbi wa Bunge.....Hizi ni picha za tukio hilo

 Wajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikaoWajumbe wa Bunge  Maalum la Katiba ambao wanaunga mkono mfumo wa  Serikali za tatu wakitoa katika Ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma baada ya kususia kikao
***********

Wajumbe karibu wote wa vyama vya upinzani wanaoshiriki Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma, wametoka nje ya kikao cha leo jioni, wakipinga kitendo cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye wajumbe wengi ndani ya bunge hilo, kuwaburuza.
 
Wakati akitoa mchango wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliliambia Bunge kuwa wanashangazwa na kitendo cha CCM kutaka kutumia wingi wao, kutengeneza katiba ambayo hailingani na mawazo ya wananchi, kama yalivyowasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
 
Alisema kitendo kilichofanywa na Waziri wa Nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi, kwenda katika kanisa na kusema wanaotaka muundo wa serikali tatu wanataka kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kiislamu ni uchochezi unaoweza kuligawa taifa na hata kusababisha machafuko.
 
Alisema pia wanashangazwa na Rais Kikwete kupokea na kusaini rasimu hiyo, lakini akaja bungeni na kuipinga kwa nguvu kubwa.
HABARI KAMILI..>>>

VIDEO: Sikiliza mchango wa Profesa Lipumba uliopelekea wajumbe wa UKAWA kususa na kutoka nje ya bunge la Katiba leo jioni

Audio na Video za mchango wa Prof. Ibarahim Lipumba alioutoa Bungeni siku ya Jumatano, Aprili 16, 2014 na kutamatia kwa baadhi ya wajumbe kutoka nje ya Bunge Maalum la Katiba ipo hapo chini baada ya mchango huo kwa maandishi ifuatavyo:-
Mhe. Mwenyekiti gazeti la Mwananchi la tarehe 14 Aprili 2014 limeandika kuwa “Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge), William Lukuvi ameanza kampeni kanisani kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa Serikali ya Muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.”

Mhe. Lukuvi aliyasema haya katika Kanisa la Methodist, Jimbo la Dodoma alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika ibada ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa askofu. Hoja kama hiyo pia ilizungumzwa na Rais Kikwete wakati akilihutubia bunge Maalum tarehe 21 Machi 2014.
 

Ni kweli katika Rasimu ya Katiba taratibu imara za Mapato ya Serikali ya Shirikisho hazijawekwa vizuri. Serikali hiyo haina Mamlaka ya Mapato. Baada ya Rasimu ya kwanza kutolewa tatizo hilo nililichambua kwa kina katika mada niliyowasilisha katika Baraza la Katiba la TCD. Makala hii imetumiwa sana na Wajumbe wa Bunge hili. Hata hivyo wajumbe hawa hawanukuu ufumbuzi uliopendekezwa katika mada hii.


Baraza la Katiba la TCD chini ya Uenyekiti wa Augostin Lyatonga Mrema ulipendekeza muundo wa serikali tatu na utaratibu wa uchangiaji wa mapato toka serikali washirika kwa kadri mapato yanavyokusanywa na serikali washirika.


Zaidi ya asilimia 90 ya gharama za Shirikisho siyo mpya. Gharama za Rais wa Muungano za hivi sasa zitahamia kwa Rais wa Shirikisho.


Ikiwa tutakuwa na uwazi na uwajibikaji gharama hizo zitakuwa ndogo kuliko za sasa. Gharama za JWTZ, Polisi, Uhamiaji, Mambo ya nje zitahamia Serikali ya Shirikisho. 

Zote hizi siyo gharama mpya
Kwa sababu ya uzoefu wa “Akaunti ya Fedha ya Pamoja” na Tume ya pamoja ya Fedha, Rasimu ya Katiba haina pendekezo la kuwepo kwa chombo kinachoshirikisha serikali tatu kujadili na kukubaliana mgao wa mapato ya serikali za washirika kugharamia serikali ya Muungano.


Tume imependekeza ushuru wa bidhaa kuwa chanzo cha mapato ya kodi ya serikali ya shirikisho.Ni vyema mapato ya kugharamia serikali ya Muungano yakachangiwa na mapato ya serikali mbili.


Katiba itamke wazi serikali za washirika zitachangia sehemu ya mapato yao yote kwenye serikali ya Muungano. Kuzuia migongano ni vyema tukafikia muafaka wa asilimia ngapi ya mapato ya serikali yaende kwenye shughuli za Muungano.


Kwa kutumia uchambuzi wa gharama za Muungano uliofanywa na Tume ya Pamoja ya Fedha, gharama za Muungano ni asilimia 20 ya mapato ya Muungano. Katiba inaweza kutamka kuwa kiasi kisichopungua asilimia 20 ya mapato yote ya serikali za Washirika yatawasilishwa katika mfuko wa serikali ya Muungano kwa kadri mapato hayo yanavyokusanywa.


Izingatiwe kuwa kwa utaratibu huu bado mshirika mwenye uchumi mkubwa atakayechangia sehemu kubwa ya gharama za Muungano.
Katiba itamke kuwa Bunge la Shirikisho litatunga sheria ya kuweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa sehemu yake ya mapato yanayokusanywa na serikali za Washirika yanawasilishwa kwenye mfuko wa Serikali ya Shirikisho.


Mamlaka ya kukusanya mapato inaweza kusimamiwa kwa pamoja kati ya serikali ya shirikisho na serikali za washirika ili kuhakikisha kuwa mapato yanayokusanywa na kuyawasilisha kwa serikali ya Washirika na serikali ya Muungano kwa uwiano uliokubaliwa.


Miaka ya 1960 na 1970 Mamlaka ya kukusanya mapato ya Afrika Mashariki ilikusanya kodi za mapato, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa Kenya, Tanganyika na Uganda na kuziwasilisha kwenye serikali husika.
 

Sera za kodi zilitungwa na nchi husika lakini kodi za nchi hasa ushuru wa forodha zilifanana.
 

Kama CCM ingekuwa na nia njema utaratibu wa kukusanya kodi na kugawa kwenye serikali ya shirikisho na serikali za washirika siyo rocket science ni jambo ambalo linaweza kuwekwa vizuri ndani ya katiba. Katiba ya muungano kama katiba mama ijenge misingi mizuri ya usimamizi wa fedha za umma na ukusanyaji wa kodi.

Mhe. Mwenyekiti, Rasimu ya Katiba imeletwa na Tume ya Rais ili tuijadili na kuipitisha. Rasimu hii siyo ya CUF, siyo ya CHADEMA, siyo NCCR Mageuzi, siyo ya Wapemba. Ni Rasimu ya Tume ya Rais Kikwete.
 

Katika hotuba yake katika kanisa la Methodist Mhe. Lukuvi pia alisema “Serikali tatu zikipita ni wazi kuwa hata makanisa yatafungwa kwani nchi haiwezi kuwa na amani tena.”
 

Lukuvi alisema Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu.
 

Baadaye alipotakiwa kufafanua kauli yake, Lukuvi alisema alichokizungumza kanisani hapo ni mawazo yake binafsi ambayo yanafanana na Watanzania wengi, akiwamo Rais Jakaya Kikwete.
 

Mhe. Mwenyekiti je lengo la serikali mbili ni kuwadhibiti Wazanzibari wasianzishe dola ya Kiislam kama alivyoeleza Mhe. Lukuvi? Baada ya hotuba ya Mhe. Lukuvi “Askofu Bundala alisema kanisani hapo kwamba ili kudumisha Muungano ni vyema Katiba ya Zanzibar ifutwe ili iwepo moja ya nchi moja ambayo inadumisha Muungano.”
 

Mchakato wa kupata katiba mpya unapaswa kuwa wa maridhiano, Vipi Waziri anayemuwakilisha Waziri Mkuu anaenda kanisani na kusema Wazanzibari wanaotaka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka Serikali ili wapate nafasi ya kujitangaza kuwa ni nchi ya Kiislamu.
 

Kama hamuitaki Rasimu ya Katiba ya Tume ya Rais kwa nini mmetuleta hapa kwa gharama kubwa. Tunaambiwa Bunge limekarabatiwa kwa shilingi bilioni 8.2. Je ni utaratibu wa 10 percent uliohamasisha kutumia fedha nyingi huku serikali ikiamini kuwa Rasimu ya Katiba haifai kabisa.
 

Mjadala umekuwa wa matusi na siyo wa kujenga hoja. Kauli za kibaguzi zimetolewa dhidi ya Wapemba, dhidi ya Waarabu, dhidi ya Wahindi. Wajumbe wa Bunge Maalum wanashangilia kauli za kibaguzi. Tunaanza kupanda mbegu ya intarahamwe wa Tanzania. Kauli za kibaguzi ni kinyume cha maadili na tunu za Watanzania.
 

Kwa utaratibu wa kanuni 33 (7), Baada ya taarifa ya kamati namba moja hadi namba kumi na mbili kuwasilishwa, taarifa hizo zitajadiliwa kwa kipindi kisichozidi siku tatu. Baada ya mjadala kamati ya uandishi inapaswa kuanda vifungu vya sura hizo mbili ili vipigiwe kura na wajumbe wa pande mbili za muungano. Hilo halitafanyika.

Kufuatana na Ratiba, Bunge Maalum litaendelea hadi tarehe 25 Aprili bila kupiga kura na kufanya maamuzi ya vifungu vya sura hizi mbili kinyume na kanuni. Bunge linaahirishwa hadi Agosti bila kufanya maamuzi ili kuwapa nafasi CCM watafute theluthi mbili ya pande zote za Muungano kwa njia yeyote ile.


Tunaopigania katiba ya wananchi hatuwezi kubariki uchakachuaji wa maoni ya wananchi. Wakati umefika tuwaache CCM muendelee na vioja vyenu kwani hamtaki kuandika katiba inayotokana na mawazo ya wananchi badala yake mnahamasisha chuki dhidi ya Wapemba, Wahindi na Waarabu na kupandikiza uhasama wa kidini. 
 
Msikilize hapa( audio ):


Video  za  matukio  hayo
HABARI KAMILI..>>>

Muasisi wa CHADEMA, mzee Edwin Mtei alaani kitendo cha Tundu Lissu kumtukana Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere


Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu. 
 
Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972. 
 
Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
 
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke: 
 
Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao. 
 
Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.
 
Edwin Mtei
HABARI KAMILI..>>>

Hati ya Makubaliano ya Muungano yawasilishwa Bungeni.


Makamu mwenyekiti wa bunge maalum la katiba, Samia Suluhu Hassan amesema amepokea hati ya makubaliano ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyothibitishwa kisheria.
 
Hati hiyo imefikishwa bungeni hapo baada ya mjumbe wa bunge hilo, Tundu Lissu kuomba hati hiyo ioneshwe hadharani siku mbili zilizopita.
 
Waziri wa nchi ofisi ya rais, Stephen Wasirra alieleza kuwa ametimiza ahadi yake aliyoitoa awali kuwa hati hiyo ingefikishwa bungeni ndani ya siku mbili.
 
Katika hatua nyingine, wajumbe wa bunge hilo maalum la katiba leo wameendelea na majadiliano kuhusu sura ya kwanza na ya sita ya rasimu ya katiba huku suala la muundo wa serikali za muungano likichukua nafasi kubwa.
HABARI KAMILI..>>>

Alichosema bungeni Mh. Wassira kuhusu Tundu Lissu

 
April 16 2014 saa saba kasoro mchana makamu mwenyekiti wa bunge la katiba hapa Dodoma aliwasha kipaza sauti na kuzungumza kuhusu matangazo mawili yaliyomfikia, moja la wageni na la pili ni la hati ya muungano ambayo hatimae imepelekwa bungeni baada ya kuzungumziwa sana na Wajumbe mbalimbali hasa wanaotaka uwepo wa serikali tatu waliosema hati hiyo haipo.
 
Makamu Mwenyekiti alisema ‘nimepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy na sasa nampa dakika mbili Mh. Wassira atoe maelezo ya hati hii’
 
Mh Wassira akaanza:
1. Juzi nilisimama katia bunge hili na kusema kwamba hati ya muungano iliyokua inapigiwa kelele sana, ipo katika hali nzuri na ndani ya siku mbili itafikishwa bungeni.
  1. Sisi wote tumeapa na mwisho wa kiapo chetu tukasema ewe Mungu nisaidie, Mungu wa madhebu yote ni Mungu wa ukweli na uongo ni kazi ya shetani, wamegawana kabisa Mungu wa ukweli na Shetani wa uongo.
  2. Baada ya hati kupatikana jana Tundu Lissu na wenzake wamekutana wakazungumza kwamba sasa tusema sahihi ya Karume sio sawa, tunaipeleka wapi Tanzania? yani kila siku uongo unataka utawale Tanzania na ukweli upuuzwe?
  3. Watanzania tujihadhari sana na Mawakala wa shetani maana Mungu anatumia Wanadamu kufikishia ujumbe wake kwa Wanadamu wengine na Shetani anatumia Wanadamu pia, lazima tukwepe mamlaka ya shetani na Mawakala wao.
  4. Mh. Tundu Lissu amewakashifu waasisi wa taifa Mzee Karume na Mwl. Nyerere Mungu awaweke mahali pema, anasema ni madikteta na waongo…. mimi nasema heshima ya viongozi wetu waasisi hailindwi na vyama, italindwa na Watanzania wote, wajibu wa kulinda heshima yao ni wa wote.
  5. Hatuzuii mtu kusahihisha sera lakini huwezi kusema viongozi wetu wale walikua ni waongo na Madikteta, hatuna haki ya kuwakashifu, namwambia rafiki yangu Tundu Lissu, ulinzi wa heshima ya viongozi hawa ni wa Watanzania na utalindwa kwa gharama yoyote.
>>MillardAyo
HABARI KAMILI..>>>

Mafuriko jijini Dar.....Idadi ya waliofariki yafikia 41


Mafuriko  yaliyotokea Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki yamesababisha vifo vya watu 41.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema vifo 25 vimethibitishwa. Ameagiza polisi kufanya uchunguzi zaidi kubaini watu wengine ambao hadi sasa hawaonekani waliko.
 
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa, eneo la Ilala, vilitokea vifo 11 ingawa inahisiwa watu wengine wawili hawaonekani. Kinondoni vifo ni saba huku wengine 14 wakidaiwa kuzikwa bila polisi kupata taarifa na Temeke vifo saba.
 
Sadiki alitaka uchunguzi wa polisi ufanyike kila familia zilizokumbwa na msiba, hususani Kinondoni kuthibitisha kama vifo hivyo 14 vilitokana na mafuriko.
 
Kuhusu kurudi katika makazi yao kwa wakazi wa Jangwani alitaka watumie busara kwani kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.
 
Alisema serikali haiwezi kubomoa nyumba husika kwani inasubiri uamuzi wa mahakama kutokana na kuwepo kwa kesi iliyofunguliwa dhidi yake.
HABARI KAMILI..>>>

Jeshi la Polisi latangaza kitita cha Sh. Milioni 10 kwa mtu atakayesaidia kukamatwa kwa watu waliolipua bomu juzi jijini Arusha katika baa ya Night Park

 
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI),Isaya Mngulu
 *****
Jeshi la Polisi nchini limetangaza zawadi ya Sh. milioni 10 kwa atakayewezesha kukamatwa kwa  watu waliotumia mabomu kulipua  baa ya Night Park mwishoni mwa wiki iliyopita.

 Katika mlipuko huo, watu 17 wameripotiwa kujeruhiwa kati ya hao, waliobaki wodini kuendelea na matibabu ni nane baada ya wengine kuruhusiwa.

Wanaondelea na matibabu ni  Evance Maleko, Evarist Richard, Petro James, Christian Zakaria, Pius Shayo, Antelus Ishengoma, Sudi Ramadhani na Mariam Hansi aliyeko hospitali ya Selian.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Isaya Mngulu, alisema uchunguzi uliofanywa na jeshi hilo umebaini kuwa bomu lililolipuliwa Aprili 13, mwaka huu, saa 1:30 asubuhi kwenye baa hiyo, ni la kutengenezwa kienyeji.

Mngulu alisema wataalamu wa mabomu waligundua bomu lingine lililokuwa kwenye mkoba ulioegeshwa kwenye kiti katika baa ya Washington,  pembeni mwa baa hiyo.

“Bomu hili tumeligundua baada ya tukio hili kutokea na saa sita usiku tukaligundua, lakini halijalipuka na tunalo kwa ajili ya kuchunguza tujue limetengenezwa kwa kutumia vifaa gani,” alisema.

Alisema hata  bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji, jambo lililowafanya waelewe hata hilo lililolipuka ni la kienyeji.

Mngulu alisema kutokana na kukithiri kwa matukio hayo nchini kwa sasa, ni vema wananchi na hasa wale ambao wapo maeneo ya mkusanyiko, wakachukua tahadhari za uhakika, kwani siyo vema kumwamini hata rafiki yako.

“Ni vizuri ukajiridhisha alichobeba rafiki yako kwenye mkoba na ukitilia wasiwasi bora utoe taarifa polisi na siyo kukaa kimya hadi madhara yakatokea,” alisema.

Alitoa rai kwa wamiliki wa kumbi za starehe, makanisani, misikitini na maeneo ya mikusanyiko kujitahidi kuweka kifaa cha CCTV ili kuwezesha kubaini wahalifu pale uuhalifu unapotokea.

Alisema hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na kwa kuwa wana kifaa cha CCTV kilichofungwa Night Park, wana hakika muhusika atapatikana.

Alisema matukio ya milipuko ni mengi kutokea nchini kwa sasa na yanatokea maeneo mbalimbali na siyo Arusha peke yake, isipokuwa wote wanaokamatwa na milipuko hiyo kama Dar es Salaam na Tanga ni vijana wadogo ambao hawajawahi hata kupita jeshini.

Kuhusu Sikukuu za Pasaka, alisema kila mkoa umepewa maelekezo kwa Kamanda wa Polisi kutumia mbinu zao zote na vifaa walivyonavyo kama farasi na mbwa ili kulinda usalama wa ibada za sikukuu hizo
HABARI KAMILI..>>>