Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, February 21, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Kumi ( 10 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

 Simu yangu ikaingia meseji na namba iliyoleta meseji hiyo imeandikwa PRIVETE.Taratibu nikaanza kuisoma meseji hiyo
{NIPO NJE NAKUFWATILIA KILA HATUA NA HUYO MALAYA ZENA ULIYE NAYE NDANI KWAKO NITAMUUA UKISHUHUDIA}
Nikatamani ardhi ipasuke nidumbukie.Nikazidi kuchanganyikiwa pale Madam Zena aliponiaga anataka kuondoka ili akawahi kipindi chake cha kufundisha baada ya mapumziko ya saa nne asubuhi

ENDELEA
 “Madam ninakuomba usiondoka please”
“Kwa nini Eddy wakati nimesha kuleta hadi nyumbani?”
“Na penda tu leo unipe  kampan yako ya kukaa hapa kwangu nakuomba”

Madam Zena akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha akatoa simu yake na kupiga kwa mtu ila sikujua ni nani
“Sir Barongo”

“Nakuomba unishikie vipindi vyangu kaka yangu kama huto jali kidogo nimepata dharura”
“Nashukuru kaka yangu haya Mungu akipenda kesho”
Madam Zena akakata simu kisha akairudisha kwenye begi lake na kuniangalia huku aikitabasamu
“Sasaa hapa ninaweza kukaa kwa amani….Ehee mgonjwa una CD gani nzuri nzuri za movie”
“Kwa CD tu hapa utakesha”
Madam Zena akachukua makasha ya CD yaliyopo chini ya meza ya kioo na kuanza kuangalia kasha moja hadi jengine hadi akakuta kasha lililoandikwa PIRATE ON BLACK SEE akaitoa CD yake na kuiweka ndani ya deki kisha akarudi kwenye sofa na kukaa.Madam Zena akaanza kuguna baada ya CD hiyo kuanza kwani imeshamiri mambo ya kikubwa yanayo onyeshwa live bila chenga
“Sir Eddy hivi hizi CD unazitolea wapi?”
“Kwa nini?”
“Huwa ninazitafuta ila sizipati”
“Kuna maeneo ya pale forozi karibu na benki ya NMB kuna jamaa best yangu anaziuza”
“Bei gani?”
“Elfu tatu”
“Basi kuna vijana walinipitishia wakaniuzia kwa elfu ishirini”
“Dooo wamekutapeli hao”

“Tena wamenitapeli sana kwani CD lenyewe lina scratch kama nini”
“Basi nitakutafutia”
Madam Zena akaendelea kutazama CD huku akionekana kunogewa kwa jinsi watekaji wa meli katika CD hiyo wakipeana mambo matamu,Nikatazama Wallet yangu na kukuta  nina pesa ya kutosha.
“Zena ngoja nikanunue chakula cha mchana”
“Haupiki?”
“Sijisikii kupika”
“Lakini mimi si nipo ninaweza kupika”
“Utapika siku nyingine ila nakuomba kama mtu yoyote akigonga usimfungulie hadi usikie sauti yangu”
“Sawa ila ni kwanini?”
“Watu wa mtaa huu ni wasumbufu sana na wamesha anza kunizoea vibaya”
“Sawa au unaogopa vimanzi vyako vitakuja?”
“Sina manzi wala nini wewe fanya kama nilivyo kuambia……………Nikuletee kinywaji gani?”
“Kwanza unakwenda kununua nini….”
“Alafu sikukuuliza nikuchukulie chakula gani?”
“Mimi niletee chipsi yai na kuku nusu nikipata na castel mbili baridi utakuwa umeifanya siku yangu ikawa powaaa”
“Powa nitafanya hivyo ila na wewe fanya kama nilivyo kuagiza usije ukafungua mlango”

“Sawa Eddy nimekuelewa”  
Nikatoka chumbani kwangu na Madam Zena akaufunga mlango wangu kwa ndani lengo langu ni yeye kuweza kuwa katika hali ya usalama kwani kuna watu wameanza kunipa vitisho kwa njia ya meseji.Nikamsalimia bibi kizee mwenye umri kwa makadirio yangu unao fika miaka 70 hivi.Aliyekaa nje ya nyumba ya jirani na ninapo ishi
“Marahaba mjukuu wangu.Hujambo baba”
“Sijambo haya mimi ninapita”
“Sawa…..ila kijana nakuomba mara moja”
Nikamsogelea sehemu aliyokaa na akanionyesha sehemu ya kukaa huku macho yangu yakilichunguza eneo la hapo kwani mtu aliye nitumia meseji alidai yupo maeneo haya huku akijua nipo na nani ndani kwangu
“Kijana unaitwa nani?”
“Ninaitwa Eddy”
“Ahaaa Eddy mjukuu wangu inavyoonekana wewe ni mgeni hapa Tanga?”
‘Ndio”

chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )