Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, March 26, 2018

TANGA RAHA- Sehemu ya Arobaini na Moja( 41 )

juu
 AGE………………18+
WRITER…………EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA

Radi nyingi zikaanza kutawala kwenye anga huku mawingu mazito ya mvua yakikusanyika kwa kasi.Ndani ya dakika kadhaa mvua kubwa iliyoongozana na radi kali ikaanza kunyesha.Nikatafuta sehemu ya kujibanza pembezeni ya ukuta ili kuacha mvua ipite
Nikiwa nimeuegemea ukuta niskastukia nikikabwa shingo kwa nguvu na mkono ulio tokeza kwenye ukuta nilio uegeme huku mkono huo ukiwa na kucha ndevu za kutisha

ENDELEA
Cha kwanza kukiwahi ni kuishika shingo yangu kwa haraka na kuanza kuminyana na kiganja hiki kilicho ikamata shingo yangu,nikafanikiwa kujinasua kwenye kiganja,kitendo cha kugeuka nyuma nikakikuta kikimalizikia kuingia ndani ya ukuta.Nikataka kuondoka ila ujasiri mkubwa ukauvaa mwili wangu,nikarudi nyuma hatua chache na kuiangalia jinsi nyumba hii ilivyo kuanzia juu hadi chini.Ni nyumba inayoonekana kujengwa miaka mingi ya nguma,kwani hata kuta zake ni zile zilizo jengwa kipindi cha ukoloni.Nikiwa ninaendelea na uchunguzi wangu wa macho nikaanza kuzisikia sauti za watu wakingong’oneza ndani ya ukuta ambao nilikuwa nimeuegemea.

Kila ninapojaribu kuitafsiri hii lugha siipatii jibu kwa maana,kinacho zungumza hakieleweki ila watu hao wanazungumza kwani wanaonekana wanamambishano ya wao na wao.Nikazunguka upende wa pili wa nyumba na kukuta milango na madirisha vikiwa vimefunga,gafla taa zilizokuwa zinawaka nje zote zikazima gafla na kiza kinene kikatawala kila eneo,huku mvua iliyo andamana na radi zikiendelea kurindima kwa kasi ya ajabu.Nikaanza kuondoka taratibu,hatua chache kutoka nyumba ilipo nikasikia jina langu likitajwa ndani kwa sauti ya juu na kunifanya nigeuke nikiwa na mshangao mkubwa

Nikatamani kurudi nyuma ila nikaanza kuondoka,kila ninapopiga gatua moja mble ndioyo sauto ya mtu anaye liita jina langu huku akilia ikizidi kuongezeka.Nikayaziba masikio yangu na kwenda mbele zaidi ila nikajikuta saut inayo niita ikizidi kongezeka.Wasasiwasi mwingi ukaanza kunitawala,niakageuka na kuanza kurudi sehemu ilipo nyumba,hadi ni nafika mlango ukafunguka na wala sikumuona mtu aliye ufungua mlango zaidi ya giza nene lililo tawala ndani ya nyumba.

“Njoo”
Sauti ambayo ilikuwa ikiniita ikaanza kuniiomba niingie ndani.Nikajitazama kuanzia juu hadi chini na kuanza kupiga hatua za taratibu na kuingia ndani,gafla mlango ukafunga kwa nyuma na nikaanza kuhisi vitu vikianza kunishika shika mwilini mwangu.Sikuwa na budi zaidi ya kuanza kupiga mayowe ya kuomba msaada,ujanja wote ukaniishia.Gafla taa za chemli zipatazo nne zikawaka kwenye kona zote za chumba.Sikuamini kuona watu wengi wakiwa wamerundikana kwenye nyumba hii ambayo kwa ndani haina vyumba kama nyumba nyingine.Watu ambao wapo humu ndani wanavuja damu kwenye miili yao

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )