Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, April 21, 2018

Aliyekuwa mpenzi wa Masogange, afunguka siri kubwa

adv1
Msanii wa filamu bongo Rammy Galis ambaye alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Agnes Masogange aliyefariki hapo jana, ametoa siri ambayo wengi walikuwa hawaijui kuhusu maisha ya Agnes.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Rammy Galis ameandika ujumbe akionesha kuhuzunishwa na kifo cha mrembo huyo ambaye alibarikiwa na Muumba kwa urembo wake, na kusema kwamba walipokuwa kwenye mahusiano aliwahi kucheza filamu yake ambayo kama ilitabiri kifo chake, kwa kuigiza kufa mwisho wa kisa hiko kilichopewa jina la 'hukumu'.

“Tulikesha usiku na mchana ili ucheze filamu yetu kwa hisia, ukasema hii iwe kumbukumbu yako kama niliwahii hata kwenye kazi zako kukusaidia, sasa kwanini filamu yetu tulitunga jina liitwe #hukumu? ilikuwaje story ya filamu mwisho unafariki? kwani tulikua tunatungia iwe kweli hukumu yako? Mungu ndio hakimu wa viumbe vyote katika dunia , umeondoka ghafla sanaa , na hii pia ni funzo umeniachia”, ameandika Rammy Galis akiambatanisha picha ya wawili hao pamoja.

Kutokana na kauli hii ya Rammy Galis, tunaweza sema Masogange naye amepitia kifo ambacho muigizaji nguli wa filamu za bongo Steven Kanumba alifariki, kwa kuigiza kifo kwenye filamu yake ya mwisho, na kweli kabla ya filamu kutoka alipatwa na mauti.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )