Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, April 1, 2018

Kauli ya CHADEMA Baada ya Halima Mdee Kukamatwa na Polisi Leo

juu
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kimeamua kumpelekea daktari wa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee ili aweze kumcheki na kuwathibitishia Jeshi la Polisi kuwa Halima ni mgonjwa na wala hakuwa na nia ya kukimbia kuripoti Polisi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

"Halima Mdee bado anashikiliwa na Jeshi la Polisi wa kituo cha 'Centro' Jijini Dar es Salaam mpaka hivi sasa japokuwa amewaeleza ukweli kwamba ametoka kwenye matibabu na kuwaonesha vyeti vyote vya hospitali lakini bado wanaendelea kumshikiria", amesema Mrema

Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "mpaka sasa hivi hatua tulizozichukua ni kumpeleka daktari wake ili aende kumcheki na kuwathibitishia Polisi kuwa Halima kweli ni mgonjwa pia wanasheria wa chama wataelekea kituoni hapo muda si mrefu".

Halima Mdee ni miongoni mwa viongozi wa Chadema wanaotuhumiwa na Jeshi la Polisi kufanya maandamano yasiyokuwa na kibali kipindi cha uchaguzi mdogo wa marudio katika jimbo la Kinondoni
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )