Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, June 23, 2018

Bomu Lalipuka Waziri mkuu mpya wa Ethiopia akihutubia

adv1
Mlipuko mkubwa umetokea katika mkutano wa waziri mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed.Inaarifiwa kwamba watu 83 wamejeruhiwa huku 6 wakiwa katika hali mahututi.

Kiongozi huyo ameondolewa eneo hilo haraka na kwa muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake katika mkutano alioandaliwa kuiunga mkono serikali yake.

Maelfu walikuwa wamekusanyika katika bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa.

Abiy amelitaja shambulio hilo kama "Jaribio ambalo halikufanikiwa la vikosi visivyotaka kuiona Ethiopia imeungana".

Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamepelekwa katika kituo cha afya kilicho karibu na bustani hiyo kupokea matibabu.

Abiy aliichukua nafasi ya waziri mkuu Ethiopia baada ya kiongozi aliyekuwepo Hailemariam Desalegn aliopjiuzulu ghafla mnamo Februari

Yeye ni kiongozi wa kwanza kutoka jamii ya Wa Oromo ambayo imekuwa ikiandamana dhidi ya serikali kwa takriban miaka mitatu ambapo mamia ya watu walifariki.

Inaaminika Abiy anaungwa mkono pakubwa miongoni mwa vijana wa Oromo pamoja na makabila mengine.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 42 alizaliwa katika mji wa Agaro huko Oromia na anatoka katika familia iliyochanganyika waislamu na wakristo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )