Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 10, 2018

Mahakama yashindwa kutoa hukumu ya Mbunge CHADEMA

adv1
Mahakama ya wilaya ya Mbozi imeshindwa kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Mbunge wa jimbo hilo, Ndg. Pascal Haonga (CHADEMA) baada ya kudaiwa kwamba mchakato wa hukumu haujakamilika kulingana na uzito wa kesi.

Hukumu hiyo imeahirishwa na Hakimu Mfawidhi, Nemes Chawi  anayeendesha kesi hiyo ambapo amepanga kuifanyia maamuzi Kesi hiyo namba 117 ya mwaka 2017 Agosti10.

Katika kesi hiyo Haonga na  Katibu wake Wifred Mwalusanya na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kalasha, Mashaka Mwampashi wanakabiliwa na mashitaka matatu ikiwa ni pamoja na kufanya vurugu wakati wa uchaguzi na kuwazuia askari polisi kutekeleza majukumu yao tukio walilolifanya  Agost 28, 2017.

Naye  Wakili upande wa utetezi Bonifasi Mwabukusi ameishukuru Mahakama kwa uamuzi huo na kuamini kuwa mahakama itatenda haki.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )