Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, October 12, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 99 na 100 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA     
Nikachukua simu nyingine ya Cajoli, akanikabidhi na funguo za gari lake kisha nikaondoka. Safari ya kuelekea katika hoteli ya Mkonge hoteli haikuchukua muda mrefu nikafika, nikasimamisha gari kwenye maegesho, simu ya mfukoni mwangu ikaita ikanibidi kuitoa simu na kuipokea huku nikiwa nimesimama pembeni ya gari langu.
“Dany umefika”   
Niliisikia sauti ya Cajoli akizungumza kwenye simu, ila kabla sijajibu nikahisi kitu kizito kikinigandamiza kichwani mwangu huku nikisikia sauti nzito ya mwanaume ikiniamrisha kwamba nisigeuke nyuma la sivyo atanichangua ubongo wangu.

ENDELEA
“Dany”   
Sauti ya Cajoli ikaendelea kusikia kwenye simu ikiniita jina langu, sikuweza kumjibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya na kusikiliza amri ya mtu huyu aliye simama nyuma yangu.
“Rudi nyuma”
Alizungumza tena, nikafanya kama anavyo hitaji, taratibu nikaanza kurudi nyuma kwa hatua ndogo ndogo.
“Ingia kwenye gari”
 
Mtu huyo alizungumza na kunifanya niingie kwenye gari jengine ambalo lipo pembeni ya gari ambalo nimekuja nalo na ninahisi huyu mtu aliweza kuniona kipindi ninashuka kwenye hili gari  langu.
Nikautazama mlango wa gari hili ulio funguliwa, taratibu nikaingia, jamaa wa nje akafunga mlango na taa iliyopo ndani ya gari hili ikawashwa. Pembeni ya siti ambayo nimekaa nikamkuta John akiwa anatabasamu.
“Vipi DANY?”
John alizungumza akiwa amejawa na furaha nyingi usoni mwake. Jambo ninalo jiuliza ni jinsi gani ambavyo Jonh amweza kufahamu sehemu mimi nilipo wakati nilitoroka hospitali nchini Kenya pasipo kuweza kumuambia mtu yoyote.
 
“Safi tu”
“Naona hospitalini uliondoka kinyume na makubaliano yetu?”
“Nikuulize swali?”
“Yaa kuwa huru tu”
“Huwa sipendi kuishi kwa kufwata amri ya mtu yoyote kwenye maisha yangu. Ndio maana mipango yote ninayo kwenda kuifanya ninahitaji kuifanya mimi peke yangu”
“Hhaaaa Dany unanihitaji mimi, unahitaji msaada wangu pasipo mimi utaumia kwa maana watu unao kwenda kupambana nao sio wadogo, ni watu ambao wameishika hii nchi”
 
“Sikia broo ninajiamini kwa kile ninacho kwenda kukifanya so ninakuomba usiingilie mipango yangu sawa”
Nilizungumza kwa kufoka, cha ajabu John hakuonyesha kukasirishwa na maneno yangu, akabaki akiwa anatabasamu tu.
“Dany wewe bado ni mdogo sana, usihitaji kuumia peke yako. Tupo kaka zako tuna uwezo wa kukusaidia, tupe nafasi ya kukusaidia”
 
“Jibu ni hapana, wewe ufahamu ni machungu gani ambayo ninayo kwa mauaji ya familia yangu”
“Dany kila jambo halihitaji kutumia hasira. Kila jambo linahitaji utulivu, jambo la muhimu kwa hivi sasa ni kuhakikisha kwamba unatumia akili kubwa kuliko kutumia hasira. Wewe ni professional training agent so huwezi kutumia hasira kwenye mission ambazo unataka kuzifanya”
“Ninajua ni nini ninacho kifanya, ninakoomba uniache niondoke”
 
“Ok sihitaji kukubana ila ukihitaji msaada wangu, chukua hii kadi yangu ina namba zangu za simu”
Nikaangalia bussines card ambayo ananipatia John, nikaichukua kisha nikashuka kwenye gari. Mlinzi wa John akaingia kwenye gari na kuondoka eneo hili na kuniacha nikiwa nimesimama nikilisindikiza gari hilo kwa macho jinsi linavyo ondoka katika eneo hili. Simu yangu ambayo bado ipo mkononi mwangu ikaita tena wala sikufahamu ni muda gani ambao Cajoli alikata simu.
“Ndio”
“Dany upo Salama mume wangu?”
“Yaa nipo salama, kuna mambo nilikuwa ninayafanya”
“Lile gari limeosha ondoka hapo hotelini na lipo katika barabara ya kuelekea Raskazoni”
 
“Nimekupata, ila sio mbali kutoka hapa”
“Yaa sio mbali, ukilifukuzia unaweza kuliwahi”
“Sawa”
Kwa haraka nikaingia kwenye gari, nikaliwasha. Nikarudi nyuma kwa haraka, nikaliweka sawa na kuondoka eneo la hoteli kwa mwendo wa kasi. Nikatazama pande zote za barabara kuhakikisha hakuna gari linalo tokea upande wowote wa barabara nikaingiza gari langi barabarani na kuanza kuelekea barabara ya raskazoni walipo elekea Yudia na watu wake. 

Kwa mwendo wangu wa kasi, nikafanikiwa kuliona gari hilo, taratibu nikachomoa bastola yangu tayari kwa mashambulizi ninayo kwenda kuyafanya. Nikazidi kuongeza mwendo hadi nikalikaribia gari lao, nikalipia kwa kasi kisha nikafunga breki za gafla huku gari langu nikihakikisha linaziba barabara. Dereva wa gari la Yudia akafunga bereki na kusimamisha gari lake mita chache kutoka lilipo gari langu. 

Kwa haraka nikashuka huku bastola nikiwa nimeishika kwa mikono yangu  yote miwili kwa ukakamavu. Nikapiga rasiai moja kwenye tairi la mbele la gari lao na kulifanya lishuke chini kwa upande huo wa tairi. Nikaanza kutembea kwa kunyata huku nikiwa ninajiamini sana, kitu kilicho anza kunipa mashaka ni pale nilipo ona mashambulizi yangu hayajibiwi. Nikiwa nimelikaribia gari mlango wa upande wa dereva ukafunguliwa, akashuka bibi wa kizungu, huku akitetemeka mwili mzima. 
 
“Lala chini”
Nilimuamrisha huku nikiendelea kutembea kwa mwendo wa tahadhari, nikaufungua mlango  wa siti za nyuma, sikuona mtu yoyote kwenye gari. Siti ya mbele kuna mtoto mdogo wa kiafrika akiwa ameinama kwenye siti huku amejikausha kimya akiogopa kitu kinacho endelea.
Nikazunguka nyuma ya gari, namba za usajili za gari ni zile zile nilizo zikremisha.
“Fu**kkkkkkk”
Nilizungumza kwa hasira huku nikirudi kwenye gari langu. Nikaingia kwenye gari na kumpigia simu Cajoli
“Vipi umefanikiwa?”
“Hapana gari ni lenyewe ila wahusika sio”
Nilizungumza huku nikuliweka sawa gari langu, nikaondoka eneo la ktukio na kumuacha bibi kizee wa kizungu akiwa amelala chini kifudi fudi.
 
“Imekuwaje?”
“Hata mimi sielewi imekuwaje, ngoja nirudi nyumbani tu”
“Sawa”
Nikakata simu na kuiweka pembeni, nikiwa maeneo ya Bombo darajani, nikapishana na gari mbili za polisi zikielekea kwa kasi katika eneo ambalo ninahisi ndipo kulipo tokea mlio wa risani. Moja kwa moja nikaeleka nyumbani kwa Cajoli, nikapiga honi mlinzi akafungua geti nikaingiza gari na kulisimamisha sehemu nilipo litoa. Cajoli aliye simama mlangoni kwa haraka akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu, tukaingia ndani huku tukiwa tumeshikana mikono.
 
“Mbona muda ule nilisikia sauti ya kiume tofauti na yako kwenye simu?”
“Kuna watu ambao wanahitaji mimi kufanya kazi nao”
“Kivipi?”
“Nina historia ndefu sana kwenye maisha yangu, kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nitakavyo kuwa nikikuambia mambo kadhaa kuhusiana na mimi”
“Sawa Dany ila walikuteka?”
Cajoli aliuliza huku machozi yakimlenga lenga.
“Hapana hawakuniteka, ila ni mazungumzo ya hapa na pale. Hivi unafahamu raisi anakuja lini Tanga?”
“Raisi anakuja kesho kutwa, ana ziara ila sijajua  anazifanyia wapi?”
 
“Inatosha siku moja”
“Kivipi?”
“Kumuua raisi”
Cajoli akakaa kimya huku akifikiria kitu cha kunishauri.
“Dany ila kitu unacho taka kukifanya ni cha hatari sana”
“Natambua ila nahitaji kufanya hichi, hii ndio nafasi yangu mimi ya pekee katika kutimia adhima yangu. Natambua Cajoli unanipenda, ila ninakuomba usinizuie katika hili ambalo ninahitaji kulifanya”
“Sawa Dany mimi ninakuruhusu kwa moyo mmoja, japo hujaniadisia mengi ila kwa mauaji yale niliyo yaona kwenye familia yako ni vyema ukalipiza kisasa ila niahidi kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Naomba uhakikishe unabaki salama salimini”
 
“Kwa hilo Mungu yu pamoja nami”
“Kuna rafiki yangu, anamiliki ghala la silaha, asubihi nitawasiliana naye na tunakwenda kwake, utachagua silaha yoyote utalayo ihitaji katika kazi yako”
“Sawa nitashukuru sana katika hilo”
Cajoli taratibu akaanza uchokozi wa mapenzi ambao mwanaume yoyote atakaye fanyiwa ni lazima atasisimka hususani jogoo wake. Taratibu tukajikuta tukizama kwenye dibwi kubwa la mapenzi. Nikamuinamisha Cajoli kwenye sofa la hapa sebleni, nikakishika kiono chake vizuri na kuanza kula kitumbua chake, safari hii nikahakikisha ninampa haki kubwa ambayo sidhanikama nitampa tena, kwa maana kazi ambayo ninaiendea sidhani kama nitarudi hai. 
 
Kelele za Cajoli  zikaendelea kusambaa hapa sebleni, sikulijali hilo nilicho kijali ninampa heshima madhubuti. Waarabu weupe taratibu nikaanza kuwasikia wakitoka kwa mbali, sikutaka kuwamgwaga nje kama nilivyo fanya kwenye mtanange wa mwanzo. Wote nikawamwagia ndani
“Ohooooo”
Cajoli akatoa mguno ulio endana na pumzi nyingi, kila mmoja jasho jingi linamwagika usoni mwake kwa maana shuhuli sio ndogo.
“Asante sana Dany, s** zako ni tamu, yaani ninazisikia zinavyo tembea mwilini mwangu”
“Kweli?”
 
“Yaa na nipo kwenye danger zone, Mungu akitujali tukipata mtoto, itazidi kuwa furaha kwenye maisha yangu”
“Kama ikiwa hivyo ninaomba umtunze mwangu na kumfundisha maadili yaliyo mema”
“Kwa nini unazungumza hivyo, sema tutamtunza na kumlea katika maadili yaliyo mema. Dany ukimaliza hiyo kazi ninakuomba tuondoke Tanzania, twende tukaishi Dubai”
“Dubai?”
“Yaaa Dubai ndio nyumbani kwetu, japo nimezaliwa Tanzania, ila asili ya wazizi wangu ni Dubai”
“Mungu abariki katika hili”
“Nibebe”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya kudeka, nikanyanyuka kwenye sofa nililo kalia. Nikainama kidogo akanipandia mgongoni mwangu. Nikambeba kama mtoto mdogo na kuingia naye chumbani. 

Tukaoga kwa pamoja na kurudi chumbani. Usiku huu, ninaweza kusema ni usiku ambao ninalala kwa amani kwenye maisha yangu, hisia zangu zinawaza mambo mengi juu ya kazi ambayo ninayo kwenda kuifanya. Cajoli kwa uchovu wa shuhuli niliyo mpatia, usingizi uliwahi kumpitia akiwa amekilaza kichwa chake kifuani mwangu. Taratibu nikamsogeza na kichwa chake na kililaza kwenye mto. Nikashuka kitandani na kuchukua Laptop  yake aliyo iweka kwenye meza ya kioo iliyopo humu ndani. Nikaiwasha kwa bahati nzuri haina namba za siri, wazo likanijia kichwani mwangu, nikaingia kwenye mtandao wa N.S.S ambao ndio ofisi nilizokuwa ninafanyia kazi.
Ili niweze kupata habari za ndani kabisa katika huu mtando unao husika na kikosi cha ulinzi wa taifa, inabidi kuingiza namba za siri ambazo siku zote huwa wafanyakazi wa kitengo hichi wao ndio wanafahamu. 
 
‘Nikiingiza namba yangu itakuwa ni shida kwangu’
Niliwaza akilini mwangu, nikijaribu kutuliza kichwa kuhakikisha ninakumbuka namba za K2, japo inaniwia ugumu  katika kukumbuka namba zake ila nikazidi kuumiza kichwa na kukituliza kuhakikisha ubongo wangu unakumbuka namba za siri za K2.
Kwa bahati nzuri nikafanikiwa kukumbuka namba zake za siri, kwa haraka nikaziingiza kwenye sehemu mbayo inamuhitaji mfanyakazi kuweza kuingiza namba hizo za siri. Akaunti ya K2 ikafunguka, jambo lililo nifanya nishushe pumzi nyingi, kwa maana nilihisi nimekosea kile nilicho kiingiza.
 
Nikaanza kusoma taarifa zilizopo kwenye mtandao wao, nikaona pia ziara ya K2 kuja mkoa wa Tanga. Atafanya mkutano wa hadhara wa kuwahutubia wananchi wa mkoa huu wa Tanga katika kiwanja cha Tangamano. Nikaona mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye kitengo hichi huku mkuu wao kwa sasa akiwa ni Babyanka. Nikaendelea kusoma taarifa za kutafutwa kwangu, japo sasa hivi sitangazwi kwenye vyombo vya habari ila kwenye mtandao wao nipo na wananitafuta kimya kimya kwa maana hadi sasa hivi hawana taarifa kwamba nipo hai au nimekufa.
Hadi inafika alifajiri, bado ninaendelea kusoma taarifa zao. Cajoli akaamka na kunikuta nikiwa nipo kwenye sofa.
“Umeamka mapema mume wangu?”
“Yaaa umelalaje?”
“Leo nimelala vizuri sana, sijawahi kulala usingizi mtamu kama huu kwenye maisha yangu”
“Kweli?”
“Ndio mume wangu”
 
Cajoli akashuka kitandani taratibu na kunifwata hadi sehemu nilipo kaa. Akanikalia kwenye paja la mguu wa kulia huku akinikumbatia.
“Nakupenda sana Dany wangu”
“Nakupenda pia, tujiandae twende kwa rafiki yako”
“Sawa, ila ngoja nikuandalie kifungua kinywa, tule ndio twende sawa mume wangu?”
“Poa mke wangu”
Cajoli akatoka chumbani, nikaendelea kusoma taarifa katika mtandao wetu, kuna baadhi ya wafanyakazi wamefariki dunia na wengi wao ninawafahamu. Cajoli akarudi chumbani akiwa na sahani aliyo weka kifungua kinywa pamoja na glasi iliyo jaa juisi. Tukapata kifungua kinywa, kisha tukaingia bafuni na kuoga haraka haraka. Tukajiandaa na kuondoka nyumbani.
“Rafiki yako anaishi wapi?”
 
“Maeneo ya Kange kule”
“Sawa”
Hatukuchukua muda mwingi tukafika maeneo ya Kange, tukasimama nje ya geti. Cajoli akapiga honi na geti likafunguliwa, tukaingia ndani ya nyumba hii ambayo inaonekana ni ya kawaida sana. Tukakaribishwa na rafiki yake huyo ambaye ni msichana wa kike.
“Huyu ndio boyfriend wangu niliye kuwa ninakuambi kwenye meseji”
“Ohoo Dany karibu sana kwangu”
“Asante sana”
“Dany huyu ni wajina wangu anaitwa Cajoi naye”
“Yaa tumefanana majina tangu utotoni tulikuwa tunafanya kazi kwa pamoja”
“Nashukuru kukufahamu”
“Alafu shem kama sura yako sio ngeni sana kwangu”
“Yaa najua hilo, utakuwa umeniona sehemu”
Tulizungumza huku tukiingia ndani.
“Twendeni huku”
 
Tukaingia kwenye moja ya chumba ambacho kina ngazi za kushuka chini, tukaingia kwenye chumba kilichopo chini ya ardhi. Cajoli akasukuma mlango huu mzito ambao umetengenezwa kwa chuma tu. Tukaingia kwenye chumba ambacho nikikubwa, na kimejaa silaha za kila aina.
“Dany jisikie huru kuna silaha na mabomu ya kila aina, hata ukihitaji bomu la nyuklia ninaweza kukupatia”
“Nyuklia?”
“Yaaa njoo ulione”
Cajoli huyu akafunua moja ya turubai lililo funika moja ya meza, nikaona bomu la nyukila ambalo endapolitalipuka sehemu yoyote linaweza kuua mamilioni ya watu na wengi wao hawana hatia kwenye maisha yao.

AISIIIII……….U KILL ME 100                                                                                               

“Hili bomu si zuri sana kwa kazi ambayo unahitaji kwenda kuifanya shemeji yangu”
“Yaa sio zuri, ila nitahitaji silaha kadha ambazo ninaweza kukamilisha hii kazi yangu”
“Chumba chote sasa ni mali yako kuwa huru”
“Shukrani”
Nikiaanza kuzunguka ndani ya chumba hichi huku nikichagua bunduki ambazo ninaona zinaweza kwenda kunisaidia kwa kazi iliyopo mbele yangu. Kwenye moja ya kabati nikaona nguo nyeusi zikiwa zimening’inizwa vizuri.
“Hizi nguo ni vipi?”
”Hizo ni nguo ambazo huwa nina shonesha mwenyewe. Kwa watu ambao wanahitaji nguo za kufanyia kazi basi inakuwa ni rahisi kwa wao kuchukua nguo kutoka kwangu”
“Ninaweza kuzijaribisha?”
 
“Ndio unaweza shemeji yangu”
Nikazitoa kwenye kabati na kuziweka kwenye meza iliyopo humu ndani. Taratibu nikaanza kuvua nguo zangu, ikambidi shemeji kugeuka na kunipa mgongo. Nikazijaribisha nguo hizi, unaweza ukasema kwamba ziliandaliwa kwa ajili yangu kwa maana zimenikaa vizuri mwilini mwangu.
“Shem hizi nguo uliandaa kwa ajili yangu nini?”
Shemeji Cajoli akanigeukia na kunitazama, akaachia tabasamu pana huku akinitazama usoni mwangu. “Wajina umemtoa wapi huyu mwanaume?”
“Kwa nini?”
“Mzuri sana”
“Utani sasa huo wajina”
“Shosti ninakuambia, unatakiwa kuwa makini kumlinda mumeo si unajua wanawake wenyewe wa sasa shida tu, wanajitongozesha wenyewe”
“Hilo nalo neon wajina”
“Shem kuna bullet proof jakets zipo kwenye hilo kabati la pili unaweza kuwa na hata mmoja”
“Asante shemeji yangu”
Nikafungua kabati la pili na kukuta majaketi ya kuzuia riasai yakiwa yamepangwa vizuri. Nikachukua moja nikalijaribisha. Likanikaa vizuri mwilini mwangu.
“Kila kitu kipo vizuri, nipatieni begi ninaloweza kuweka zana zangu”
 
“Usijali katika hilo”
Cajoli akatoka na nikabaki na mpenzi wangu.
“Dany unauhakika na hichi unachokwenda kukifanya?”
Cajoli aliniuliza kwa sauti ya upole huku akinitazama usoni mwangu.
“Yaa am sure kwa kile ninacho kwenda kukifanya”
“Ila nimeanza kupata hisia mbaya katika hili”
“Hisia gani?”
“Sifahamu ni hisia gani, ila sipo vizuri katika hili ambalo umeamua kwenda kulifanya”
“Baby nisikilize, najua nilazima utakuwa na wasiwasi mwingi katika hili, ila tambua ya kwamba ninafanya hivi kwa ajili ya familia yangu. Ninafanya hivi kwa ajili ya kutengeza amani ya maisha yangu. Amani ya familia yangu ambayo ninakwenda kuitengenza mimi na wewe. Unahitaji niendelee kuishi kwa kukosa amani na kuandamwa na wabaya wangu hadi kwa wanangu ambao nitapata kutoka kwako?”
 
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, hadi Cajol naye akaanza kumwagikwa na machozi usoni mwake.
“Nafanya haya yote kwa ajili yako na wanangu. Nilipo fikia panatosha kabisa, sihitaji kukupoteza wewe. Sina mama, sijui ni wapi alipo baba yangu, sifahamu kama yupo hai au laa. Nimebaki mnyonge kwenye dibwi ambalo sidhani kama ninaweza kutoka. Kwa nini na mimi nisilipize kisasi nikiwa na nguvu zangu, au una hitaji waje walipize watoto wetu?”
“No Dany”
Cajoli alizungumza na kunikumbatia kwa nguvu, taratibu tukajikuta tukianza kunyonyana midomo yetu kwa hisia kali sana huku machozi yakiendelea kutiririka kwenye nyuso zetu.
“Mmmghgg”
Tulisikia sauti ya Cajoli nyuma yetu, tukaachiana na kumtazama.
 
“Shem begi hili hapa”   
Shem Cajoli akanikabidhi begi kubwa jeusi, wote watatu tukaanza kusaidia kuingiza silaha ambazo nimezichagua, huku bunduki moja ikiwa ina uwezo wa kupiga risasi kwa umbali mrefu sana. Kazi haikuwa ngumu sana, baada ya muda mfupi tukawa tumemaliza kuingiza silaha zote kwenye begi huku nyingi zikiwa ni bastola na magazine zake.
“Jamani tupateni hata chakula cha mchana hapa kwangu?”
“Shem inabidi nikafanye maandalizi mapema kuhakikisha kwamba kazi yangu haiendi vibaya”
“Ila shem, kazi ambayo unakwenda kuifanya mbona kama ni kubwa sana huoni kama inaweza kuleta matatizo kwako”
“Bora wajina umenisaidia kuzungumza”
Cajoli alizungumza kwa sauti ya unyonge sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Mimi ninawaomba muwe wapole na watulivu, kikubwa ni kuniombea kwa mwenyezi Mungu, ili kazi yangu iweze kutimia”
“Sawa shem, ila ukihitaji msaada wangu ninaomba unijulishe”
 
“Hapana shemeji, kazi hii sihitaji iweze kuingia kwenye maisha ya mtu mwengine. Nyinyi kikubwa mbacho munatakiwa kuweza kukifanya, ninawaomba muweze kuniombea kwa mwenyezi Mungu aweze kunifanikisha katika hili”
Maneno yangu yakawafanya Cajoli na mwenzake kukaa kimya, hapakuwa na mtu aliye weka kipingamizi kutokana na msimamo wangu nilio uamua kwa jambo hili. Tukaagaana na shem Cajoli na kuondoka nyumbani kwake huku begi la silaha  nikiwa nimeliweka siti ya nyuma. Njia nzima wote tupo kimya, akili yangu ina kazi ya kuwaza ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya kuhakikisha kwamba ninaweza kumuua K2 na watu wake.
“Dany”
Cajoli aliniita kwa sauti ya upole na kunifanya nitoke kwenye dimbwi la mawazo, nikamtazama, kwa ishara ya macho akanionyesha mbele yetu. Nikaona askri barabarani wakiwa wanasimamisha magari yanayo ingia jiji la Tanga huku kizuizi chao wakiwa wamekiweka maeneo ya majani mapana, maeneo ya kiwanja cha ndege cha mkoa wa Tanga.
 
“Tulia usiwe na wasiwasi”
“Sasa wakikagua hili begi huku siti ya nyuma”
“Usiwe na wasiwasi Cajoli wewe tulia tena jifanye unazungumza kiarabu mimi nitakuwa mtafsiri wako, hao polisi ukizungumza nao kiarabu basi hawato elewa”
“No Danu hiyo hilo halitokuwa wazo zuri kwetu wanaweza kunisumbua na kuanza kuhitaji maswala ya passport”
“Ok wewe tulia wala usionyeshe wasiwasi wowote”
“Sawa”
Taratibu Cajoli akasimamisha gari pembeni kama polisi wa usalama barabarani alivyo hitaji afanye hiyo. Polisi akatembea hadi sehemu gari lilipo na kumfanya Cajoli kushusha kioo cha upande wake taratibu,
“Habri zenu wakuu”
“Salama tu kaka”
“Naomba driving leseni”
Cajoli akafungua kipochi chake kidogo na kutoa leseni yake na kukabidhi askari, akaisoma kwa dakika moja kasha akamrudishia. Akasoma kazi kadhaa zilizo bandikwa kwenye kioo cha mbele, alipo jiridhisha akarudi kwenye kioo.
 
“Safari njema waheshimiwa”
“Shukrani na wewe kaka”
Cajoli akafunga kioo cha gari na tukaendelea na safari yetu. Tukafika nyumbani, nikafungua mlango nyuma wa gari nikatoa begi lenye silaha. Moja kwa moja nikaingia ndani huku nikimfwata Cajoli kwa nyuma.
“Njoo chumba hichi”
Cajoli alizungumza, tukaingia kwenye chumba ambacho kina vitu vichache ikiwemo meza kubwa.
“Nenda kaandae chakula, leo ninahitaji kula chakula chako mke wangu”
“Sawa, ila upo sawa Dany?”
“Yaa am, fine “
Sure”
 
“Yaa nina uhakika, kuwa na amani mke wangu, wewe ndenda kaandae chakula”
“Sawa  honey”
Cajoli akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu akaondoka ndani ya chumba hichi. Nikaanza kupanga sila zangu, huku nyingine nikizifuita vumbi kuhakikisha kwamba utendaji wake wa kazi unakuwa sawaia. Kazi hii ikanigarimu zaidi ya lisaa limoja, nilipo hakikisha kwamba silaha zimekamilika kuwa sawa. Nikaanza kupanga ni ipi nianze nayo katika kuifanya kazi yangu. Nianyanyuka na kutoka katika chumba hichi, nikaingia jikoni na kumkuta Cajoli akiendelea kupika chakula.
“Bado hujamaliza?”
“Yaa bado sijamaliza, vipi wewe umesha maliza?”
“Kwa kiasi fulani, laptop ipo wapi?”
“Pale ulipo iacha asubuhi”
 
Nikatoka jikoni na kuingia katika chumba cha kulala, nikaichukua laptop na kuridi nayo kwenye chumba chenye silaza zangu za maangamiuzi. Nikaingia kwenye mtandao wa NSS, kuangalia kama kuna habari yoyote mpya. Sikukuta habari yoyote mpya tofauti na zile nilizo zikuta jana usiku.
Niafungua video ambayo sikuifungua kati ya video tatu zilizopo kwenye memory card aliyo nipatia Linda. Maandishi ya rangi nyekundu yakaonekana kwenye video hii ynayo someka kwa kusema.
 
‘Magaidi wakubwa Afrika na mitandao yao’
Picha ya kwanza ikaonekana K2, huku pembeni kukiwa na malezo yake, umiliki wa kundi kubwa la wasichana ambao kazi yao ni kuua pale wanapo tumwa kufanya kazi hiyo. Wakaonyeshwa watumishi wake wakuu ambao wa kwanza ni Livna Liva wa pili ni mama yangu mzazi, jambo lililo nifanya nibaki nimekodolea macho video hii,  hadi ikanilazimu kuisimamisha na kuyasoma maelezo ya mama.
 
Mama yangu anaonyesha ni gaidi aliye ingia kwenye mfarakano na bosi wake ambaye ni K2. Chanzo kikubwa cha K2 na mama kuingia katika mgogoro mkubwa ni swala zima la kugombania madaraka huku kila mmoja akijona yeye ndio mwenye nguvu kubwa zaidi ya mwenzake.
K2 na mama walikuwa marafiki wa muda mrefu tangu walipokuwa jeshini, ila mama aliacha jeshi na kuingia kwenye maswala ya uongozi huku K2 akifanikiwa kuingia katika kitengo cha NSS. Hawa wote wawili wamehusika sana kwenye kifo cha raisi wa kwanza wa kike Tanza ambaye ni bi Rahab na nafasi hiyo ikachukuliwa na kaka wa K2.
 
Historia hii kidogo ikaanza kunipa mwanga wa mambo ambayo nyuma yalikuwa yanatokea pasipo mimi kuweza kuelewa ni kitu gani ambacho kinaendelea.
‘Nahitaji uniletee kichwa cha K2 hapa’
Maneno haya ya mama yakajirudia kichwani mwangu, kwa hapo awali nilihisi mama anazungumza hivyo kutokana na ukatili ambao K2 alinifanyia kwa kunifunga kwenye gereza la giza pasipo kosa la aina yoyote. Nilihisi labda ni wivu wa mapenzi juu yangu kumbe kuna jambo ambalo linaendelea nyuma yake.
Historia kwa ufupi kati ya mama na K2 ikaishia hapo, nikaendelea kutazama magaidi wengine ambao wanafanya kazi na K2 jambo linalo nishangaza watu wote walipo chini ya K2 hakuna mwanaume hata mmoja, wengi wao ni wamama ambao sijawahi kuwaona hata siku moja kwenye maisha yangu.
 
“Dany chakula tayari honey”
“Sawa”
“Tuje kula huku au nikiandae mezani?”
“Twende tu tukalie mezani”
Nikazima laptop na kuelekea mezani kwa ajili ya chakula. Cajoli akaninawisha mikono kisha na yeye akanawa. Taratibu tukaanza kula ndizi nyama alizopika.
“Dany”
“Mmmm”
“Ninakuomba unapo kwenda huko uhakikishe unarudi salama mume wangu.”
“Usijali, ila kuna kazi ambayo ninahitaji kuifanya tofauti na hii ambayo nilipanga kuifanya”
“Kazi gani tena!!?”
“Kuudondosha mtandao wa K2, kwa maana hata nisikisema kwamba nimuue yeye, bado nitakuwa suijaipata amani ambayo ninaitafuta”
 
“Huo mtando wewe una ufahamu?”
“Ndio nina ufahamu, kupitia hawa watu wake, ndivyo jinsi nitakavyo kuwa nikimdhohofisha hadi itafikia kipindi atakosa nguvu, na akikosa nguvu ya madaraka basi kwangu itakuwa ni rahisi sana kumuangamiza”
Cajoli akashusha pumzi nyingihuku akinitazama usoni mwangu. Akaonekana ni mtu mwenye furaha ambayoa anaizuia kuionyesha usoni mwake.
“Ila kesho nitakwenda kwenye viwanja hivyo kusoma mazingira, nahitaji kumuona K2 jinsi alivyo livyo kwenye sura ya uraisi”
 
“Utakwenda na silaha”
“Yaa ni lazima kwenda na silaha kuhakikisha ninajilinda”
Siku nzima ikapita nikiwa ninapanga mipango yangu ya kimya kimya wala sikuhitaji kumshirikisha Cajili kwa kila kitu. Asubuhi ikawadia, huku moyo wangu ukiwa imejawa na shauku kubwa ya kuhakikisha kwamba ninahakikisha kwamba leo ninaondoka na roho ya K2. Nikachukua bastola zangu mbili nikazificha kwenye soksi za miguuni mwangu. Nikavaa jaketi la kuzuai risasi kisha juu yake nikavaa na sweta lenye kofia.
“Cajoli ninakuhitaji ubaki ndani, tazama Tv kuangalia kinacho tokea sawa baby”
“Ila Dany nakuomba usifanye kinyume na kile ambacho umekipanga”
“Usijali katika hilo nitahakikisha kwamba sifanyi ujinga”
“Sawa mume wangu, ninakupenda”
“Ninakupenda pia”
“Utatumia gari?”
“Hapana, nitapanda pikipiki”
“Una pesa ya kutosha?”
“Ndio”
 
Tukakumbatiana na Cajoli kisha nikatoka nje. Nikatoka nje ya geti nikatembea hadi mtaa wa pili, nikamkodisha dereva bodaboda, nikampa maelekezo kueleka hadi katika viwanja vya Tangamano ambapo hapo K2 atakuwepo. Dereva akafanya kama nilivyo muagiza, nikafika katika viwanja hivi viliyo jaa watu wengi pamoja na askari huku walinzi wa raisi wakiwa wamezagaa kila mahala. Nikaingia kwenye gorofa moja linalo tazamana na uwanja huu wa Tangamamo. Nikaanza kupandisha kwenye ngazi kueleka juu, huku nikiwa makini sana, kwa naana huuwa ninajua walinzi wengine kwa mara nyingi huwa wanakaa juu ya magorofa wakiwa na bunduki zao maalimu za kupiga risasi masafa marefu yote hiyo ni katika kuimarisha ulinzi wa raisi.
 
Nikaingia kwenye mlango wa juu kabisa katika goroa hili
ambao niliukuta ukiwa umerudishiwa tu. Nikamuona askari mmoja wa kikosi cha NSS, akiwa amejificha shemu na bunduki yake ya aina kama hiyo.
 
Kwa mwendo wa kunyata na kwa uamakini sana nikamsogelea, nikachomoa bastola yangu kwenye soks ya mguu wa kulia. Kwa kutumia kitako cha bastola nikampiga nacho kwa nyuma na kumfanya adondokee pembeni.
Nikachukua mawasiliano yake aliyo yavaa sikioni, nikayavaa mimi vizuri, kila kitu ambacho wanapeana taarifa askari wote wa NSS katika eneo hili ninayasikia. Nikalala katika sehemua mbayo alikuwa amelala akikagua maeneo ya chini ya gorofa kwa kutumia darubini yake ambayo imefungwa kwenye bunduki hii.
 
“Zimebaki dakia mbili raisi kufika kiwanjani”
Nilisikia taarifa hiyo kutoka kwa sauti ya kike ambayo nina ifahamu sana, kwani ni Babyanka. Nikashusha pumzi nyingi huku bunduki nikiwa nimeinyooshea barabarani sehemu ambayo gari za raisi zitasimama. Gari nyeusi tatu zinazo fanana zikazimama kwenye sehemu maalumu zilipo andaliwa raisi kushuka. 

Walinzi wa rais anao tembea nao kwenye gari wakashuka kwa wingi huku wakiwa makini kuhakikisha raisi akishuka kwenye gari anakuwa salama. Mlizi mmoja akafungua mlango wa nyuma wa gari ya katikati. Nikamuona raisi akishuka taratibu kwenye gari huku akiwapungia mikono wananchi wake walio anza kumshangilia kwa furaha sana.
 
Nikamvuta taratibu K2 kwa kutumia darubini ya hii bunduki. Nilipo hakikisha msalaba mwekundu ninao uona kwenye hii darubini umekaa vizuri kichwani mwake, taratibu nikaikoki bunduki, huku nikishusha pumzi nyingi. 

Nikamuangalia K2 jinsi anavyo furahi na wananchi huku akiwapa mikono ya hongera. Gafla mwili mzima ukaanza kunitetemeka huku jasho jingi likinimwahika mwili mzima. Nikajaribu kuhakikisha kwamba ninajikaza kumuweka K2 katika tageti yangu, ila ninashindwa kabisa. 

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi, taratibu nikajaribu kunyanyuka ila nikashindwa kabisa na kujikuta nikiiangusha bunduki pembeni na kulala chali, huku nikitazama juu na kuona jinsi dunia inavyo zunguka kwa kasi jambo ambalo kwenye maisha yangu sikuwahi kuliona hata siku moja.

==>>ITAENDELEA KESHO
chn
ap
Loading...
taboola dsk
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )