Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, October 23, 2018

Waziri Jafo Aimwagia SIFA Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza Kwa Kutekeleza Miradi Kwa Ufanisi

juu
Waziri wa nchi OR-TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo  ameipongeza Manispaa ya Ilemela kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo inayozingatia thamani ya fedha.

Pongezi hizo amezitoa akiwa kwenye ziara ya kikazi katika  Manispaa ya Ilemela kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alikagua jengo la utawala la Halmashauri, jengo la hospitali ya Wilaya, ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu pamoja na ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Buzuruga.

Sanjari na ukaguzi wa miradi hiyo aliongea na watumishi wa Manispaa na kuwasisitiza kufanya kazi kwa ueledi na  kujiamini huku akisisitiza suala la ukusanyaji wa mapato na kumtaka Mstahiki Meya wa Manispaa kuhakikisha anasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato hasa katika soko la samaki la Mwaloni kwani ndio chanzo kikuu cha mapato cha Halmahauri.

“Mna kila sababu ya kusimamia mapato katika soko la samaki,hakikisheni mapato yote ya soko    yanaingia vizuri na yanasimamiwa vizuri, sitaki kusikia soko la mwaloni linaharibiwa kuwa sio chanzo muhimu cha mapato ya Manispaa ya Ilemela”, Alisisitiza

Aidha amemtaka afisa mapato kuhakikisha anasimamia mapato na kama kuna wizi unaendelea basi ahakikishe anafunga mianya yote hasa katika soko la samaki na kuongeza kuwa anataka kuona mapato yanaongezeka na halmashauri inasonga mbele

Pia amewapongeza waheshimiwa madiwani kwa usimamizi wao mzuri na kuwataka kuendelea  kupambana katika kuisimamia manispaa pamoja na miradi  ya maendeleo ili Manispaa iweze kusonga mbele

Akiwa katika kituo cha Afya Buzuruga, ambapo alipata wasaa wa kuongea na wagonjwa waliofika kutibiwa, Mhe. Jafo amesema kuwa amefarijika kuona kuwa  Manispaa ya Ilemela  imefunga mifumo ya kielektroniki (GOTHOMIS) katika vituo vyote vya afya na zahanati na kuifanya  Halmashauri  hii kuwa ya kwanza ya mfano na hivyo ameziagiza Halmashauri zote  kukamilisha uwekaji wa mifumo ya hii.

Pamoja na hayo ameitaka Halmashauri kuhakikisha wanaitumia mifumo hiyo kwa lengo lililokusudiwa la ukusanyaji wa mapato kwa maslahi mapana ya Halmashauri na vituo vya afya huku akiwasisitiza watumishi kufanya kazi kwa ueledi.

Akihitimisha ziara yake ameahidi kuwa atahakikisha fedha za umaliziaji wa miradi zinaletwa ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati uliokusudiwa.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )