Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 23, 2018

Naibu Waziri: "Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018 haizuii watu kufanya tafiti"

juu
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Ashatu Kijaji amesema marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya mwaka 2018 hayana lengo la kuzuia watu, taasisi au vyuo kufanya utafiti.

Dk.Kijaji ametoa kauli hiyo jana jijini Dodoma katika Maadhimisho ya siku ya Takwimu Afrika.

Alisema kuwa madhumuni makubwa ya marekebisho na uridhiaji wa Mkataba wa Takwimu wa Afrika ni kuhakikisha kuwa zinazalishwa takwimu ambazo zinazingatia viwango.

“Niwatoe wasiwasi wananchi na wadau mbalimbali kwamba marekebisho haya yana lengo jema na hayana lengo la kuzuia kufanya tafiti,”alisema.

Kadhalika, alisema Wizara hiyo ipo katika hatua ya kuandaa kanuni za utekelezaji wa marekebisho hayo na wadau watashirikishwa ili kuwe na uelewa wa pamoja wakati wa utekelezaji wa sheria hiyo kwa maslahi mapana ya Taifa.

ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )