Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 8, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 168 na 169 )

juu
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
   
“Laiti kama wangeweka bomu basi hii ingekuwa shabaha yangu ya pekee kuhakikisha kwamba K2 anakufa”
“Ni kweli, ila kama mtu mmoja simuoni katika walinzi wake ikiwa wasichana wengine nimewaona”
“Nani?”
“Livna Livba”
Hata kabla sijatazama vizuri, mlango wa hapa sebleni ukafunguliwa. Sote tukajikuta tukigeuka nyuma, tukamuona Martin akiingia humu ndani ila uso wake ukivuja damu na ametulia sana, akaingia na Winy naye jicho moja limemvimba, nikaishika bunduki yangu vizuri huku nikipiga hatua moja mbele. Martin akatingisha kichwa akishiria kunikataza kusogea mbele kwani kufanya hivyo inaweza kuwa hatari kwangu, kwani sifahamu ni nani aliyopo nyuma  yao.
   
ENDELEA   
Taratibu tukaona viatu vyeusi vya kijeshi, hatukamaliza hata sekunde moja, sura ya Livna ikasimama mbele yetu huku mikononi mwake akiwa ameshika  bastola mbili huku amewanyoshea Winy na Martin kwenye vichwa vyao.
“Halooo Dany”   
Sauti ya Livna haijabadilika kabisa, hata sura yake ni ile ile kabisa.
“Pigeni magoti nyinyi wajinga”
Livna alizungumza kwa kwa ukali, taratibu Winy na Martina wakapiga magoti chini jambo lililo anza kuniumiza akili yangu kwani siwezi kufanya chochote kibaya kwani kitahatarisha maisha ya hawa watu wawili ambao ni muhimu sana kwangu hususani Martin.
“Vijana wako bwana waliingia vibaya kwangu, sikuwa na jinsi zaidi ya kuwafanya hivi japo huyu mseng** hapa alikuwa ni mume wangu”
 
Livna alizungumza huku akimpiga teke la mgongo Martin.
“Sikuja hapa kukukamata ila nimekuja hapa kukusaidia”
“Kunisaidia?”
“Ndio kukusaidia, natambua kiu yako ni kumuua K2 si ndio?”
Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku nikimtazama Livna, taratibu akazichomeka bastola zake kwenye kiuno chake na kuanza kutembea hadi sehemu lilipo sofa na kukaa taratibu.
“Martin unatakiwa kujifunza zaidi maswala ya kupigana, na wewe dada nawe hivyo hivyo”
Uwepo wa Livna humu ndani ukazidi kunishangaza na hata maneno yake yanazidi kunishangaza. Kupigwa kwa Martin na Winy kwangu wala sishangai sana kwani hata mimi nilisha wahi kukutana na kipigo chake nilipo kuwa na Mariana kwenye meli nilipo kuwa ninatoroka nchini Tanzania.
 
“Mbona muna shangaa shangaa vipi nimekuwa kituko eheee”
“Martin mumefanya nini sasa?”
Nilimuuliza Martin huku nikimtazama usoni mwake.
“Samahani mkuu, nilitamani kuonana naye ndio yakatokea haya”
“Kwa nini mumemleta hapa?”
“Dany acha kumkoromea mwenzako. Mshukuru Martin amenishawishi sana kuweza kuungana nawe”
“Livna huwezi kuungana nami ikiwa uliweza kusaliti baba yangu na akafa, leo hii utaungana nami kivipi?”
 
“Baba yako alienenda tofauti na makubaliano yetu na pia K2 ameenenda kinyume na makubaliano yetu je wewe utaenenda kinyume na makubaliano yetu”
“Makubaliano yapi?”
“Moja nahitaji kizazi changu cha wasichana nilio wafunza mafunzo maalumu kubaki kama walivyo na sinto hitaji kuona kuna mkuu yoyote anaye hitaji kujimilikisha kikosi hicho kama alivyo fanya baba yako eti kisa anapesa. Na pia K2 ndivyo anavyo fanya, anawatumikisha wasichana wangu, wanajitolea maisha yao pasipo yeye kufahamu ni thamani gani hao wasichana walivyo na hata akifa msichana mmoja kwangu ni hasara kubwa inayo niumiza sana”
 
 “Mimi kikosi chako sina kisasi nacho na laiti wakihitaji kuendelea kumkumbatia K2 nitahakikisha kwamba ninawaua nao”
“Kuwaua unaweza, na mimi nitakuua kwa maana sishindwi kukuua Dany. Ila bado hujakomaa kwenye vita ambayo ungehitaji kuufanya kwani kumuua msichana wangu basi ineyagarimu maisha yako”
 
Livna alizungumza kwa kujiamini sana. Ili maisha yako yasiende bure nikaamua kukupa hii ofa, ili uweze kulipiza kwa yale yaliyo tokea kwa baba yako na familia yako kwa uzima”
“Una jambo jingine?”
“Ndio ninalo kwa nini nikose. Hakikisha kwamba unanipa orodha ya maadui zako wote sawa”
“Umezungumza ya kwako ngoja na mimi nizungumze yangu. Moja ofa yako nimeikubali. Mbili ukijaribu kunisaliti, nitakuaa, kwa maana Dany wa miaka ile si wa miaka hii ya sasa. Tatu maadui wangu ni watatu na ikiwezekana nitahitaji kabla ya masaa ishirini na nne yajayo wawe wamesha ondoka duniani sawa.”
 
“Sawa hilo ni jambo raisi. Oya bado hamjanyanyuka tu”
Martin na Winy wakanyanyuka, Babyanka akaanza kuwapa huduma ya kwanza kwani nyuso zao zimebadilika kwa kipigo walicho weza kukipata huko walipo toka.
“Jamani ninaombeni maji ya kunywa?”   
Livna alizungumza huku akikaa vizuri kwenye hili sofa. Babyanka akafungua friji na kutoa chupa ndogo ya maji ya kinywa na kukamabidhi Livna.
 
“Kuna sababu nyengine ya kumsaliti K2 zaidi ya hiyo ambayo umeniambia?”
“Sababu zipo ila ni ndogo ndogo sana”
“Kama?”
“Kujiachukulia tu wasichana nao wahitaji kwenye kikundi changu, kuto kuwalipa vizuri pia ni jambo ambalo kidogo limenifanya moyo wangu kila siku niwe na maumivu”
“Kweli?”
Nilimuuliza Livna huku nikiwa nimekazia macho usoni mwake.
“Ndio”
“Kwa nini ulishindwa kumuua ikiwa anaenenda kinyume nawe?”
 
“Sipendi kuua, na kikosi changu nilikiunda kwa sheria ya kulinda wale watakao lipa pesa kwa ajili ya sisi kuwalinda”
“Ilikuwaje K2 akachukau madaraka ya katika kikosi chako?”
“Baba yako na K2 ndio walikuwa walezi wa kile kikosi, walitoa pesa zao nyingi sana. K2 akamgeuka baba yako baada ya kuzidiwa kwa kutoa matumizi, akaamua kumuua, kwa kutumia watu wake wa karibu sana. Sasa yeye ndio akabaki kuwa na nguvu katika kikosi, ila mimi ndio niliachia kikosi hichi na muanzilishi tangu nikiwa mdogo sana.”
“Muanzilishi wa hicho kikosi ni nani?”
“Huwezi kumfahamu ni mama mmoja wa Kijapani na yeye ndio aliye nipatia mafunzo ambayo leo hii ninaweza kuwapatia wezangu”
“Sawa, sasa ninasikiliza mbinu zako ambazo tunaweza kuzitumia kumuangamiza K2, raisi Donald Bush na mke wa raisi bi Hawa Donald?”
“Hao wawili nao wameingia kwenye kumi na nane zako?”
“Ndio”
 
“Ilikuwaje?”
“Hupaswi kufahamu?”
“Basi kwa hao wawili nitajitoa kwa maana siwezi kufanya kazi pasipo kujua huyo ninayetakiwa kumuhudumia amefanya jambo gani kwako”
“Hawa alikuwa mke wangu”
“Ndio  uliye funga naye ndoa, kwa maana kidoleni una pete ya ndoa?”
“Hapana”
“Kwa hiyo alikuwa hawara?”
“Nilipokonywa na raisi huyo baada ya kunipeleka katika mission ambazo ni hatari kubwa. Moja ilikuwa ni kuvuruga kikundi cha Al-Shabab nchini Somalia na nilifanikiwa kukisambaratisha, mbili ilikuwa ni kukisambaratisha kikosi cha Boko haramu nchini Tanzania”
 
“Kweli Dany umebadilika vikosi vyote hiyo viwili uliweza kuvisambaratisha?”
“Niliweza kwenye Al-Shabab, ila kwenye hicho kikosi cha Boko  haramu nilikuwa jeneral wao, baada ya kuona nimesalitiwa na raisi Donald Bush. Nilimsamehe kwa kumchukua mke wangu, ila hakuona kama msamaha wangu una tija akatuma makomandoo wake waniangamize ila nilifanikiwa kuwaua. Nilipata mke mwengine niliye funga naye ndoa, wakaona haitoshi, mke wake akatuma watu wakamuua mtoto wa mke wangu isitoshe wakakisambaratisha kikosi kizima”
 
“Duuu kweli wanahaki ya kuuwawa. Si uliwasamehe kabisa baada ya kuchukuana wao?”
“Ndio”
“Hata kama ni mimi ningewaua”
“Natamani hata kwenda kuwaua leo nasikia wamelala hapo Serena Hoteli?”
“Nani kazungumza?”
Nikamtazama Winy ambaye tayari amefutwa futwa damu usoni mwake.
 
“Hapana hapo Serena wamelala wapambe wake tuu ila raisi na mke wake wapo katika manuari ya jeshi la Marekanani na huko si rahisi kwa mtu yoyote kuweza kuwafikia na kuwaua”
“Mmmmm”
“Ndio hivyo, ukihitaji kumua raisi wao labda kwneye hizo ziara zake anazo anza kesho”
“Anazianzia wapi?”
“Anaanza kutembelea daraja la Kigaoni kukagua kagua mradi huo”
“Sawa na ni saa ngapi?”
“Majira ya asubuhi tu”
“Dany”
 
Babyanka aliniita huku akinitazama, nikamsogelea sehemu alipo kaa kwenye kiti.
“K2 amekipata kichwa cha jamaa yake, na ujumbe ulio andikwa ameusoma tayari?”
Babyanka alizungumza huku akiirudisha video hiyo aliyo irekodi nyuma kidogo.
“Mbona analia K2?”
Livna aliuliza huku akisimama pembeni yangu.
“Tumemchinja mume wake.”
“Eheheee Dany umechokoza moto, mama anakwenda kuvaa gwanda leo”
 
“Shauri yake mkuki kwa nguruwe ndio mtamu ila kwa binadamu ni mchungu sana”
“Mmmm, sasa ilikuwaje mkamchinja jamaa yake?”
“Tulimkamata”
“Mkuu”
Martina aliniita, nikamgeukia na kumtazama.
“Hiyo ndio nafasi ya kwenda kumuua K2 kwa maana hapo amechanganyikiwa tayari”
“Hapana musimue sasa hivi”
“Kwa nini?”
“Kama unahitaji kumpata Donald na mke wake, hakikisha kwamba humuui K2, waue kwanza hao wawili kisha huyo ndio atafwatia na kifo chake kitakuwa ni cha taratibu”
Livna alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Poa hapa kikubwa ni kupango wa kumuua Donald na watu wake”
“Usijali upo na injini ya kazi hapa, kesho dunia nzima unakwenda kuandika historia ya kugopesha wengi”
Masaa yote yaliyo salia tukayatumia katia kupanga mipango ya kuhakikisha kwamba raisi Donald na Hawa tunawaua huku Livna akiahidi kuongeza wasichana wake wanne ambao anawaamini na wana mfunzo ya hali ya juu anayo amini kwamba ni lazima maraisi hawa wataisoma namba.
 
Hadi kuna pambazuka kila kitu kikawa tayari katika mpango wake, wasichana wa Livna Livba nao  wakawa wamesha fika hapa nyumbani kwa Winy huku wakiwa na mavazi maalumu ambayo wanayatumia walinzi wa Marekani wanao mlinda raisi wao. Nikakabidhiwa suti nyeusi pamoja na jaketi maalumu ya kuzuia risasi ambayo nimeivaa nyuma kwanza kabla ya kuvaa shati langu juu. 
 
Nikavalishwa sura ya bandia ambayo imetengenzwa kwa haraka na mmoja wa wasichana wa Livna mara tuu baada ya kuniona. Sura hii uzuri wake ninaweza kuivaa na si hadi nifanyiwe upasuaji  maalumu(oparesheni).
Kikosi cha watu tisa kikakamilia huku sote tukiwa tumevaa vifaa maalumu vya kuweza kuwasiliana sisi kwa sisi, nikasimama kwenye kioo na kujitazama vizuri, kwa sura niliyo ivaa kusema kweli nimebadilika na si rahisi kabisa kwa mtu kuweza kunitambua. Kitambulisho changu pia kina sura hii, na ukikutana nami ni rahisi sana kuamini kwamba mimi ni mlinzi wa raisi wa Marekanani. Martin, Babyanka na Winy nao wakakabidhiwa vitambulisho vyao kwa ajili ya kwenda kuianza kazi hii.
“Dany ataenda na mimi. Husna utaenda na Winy pamoja na Martin, Babyanka utachukua walio salia”
Livna alipanga majukumu hayo huku tukkiwa tumesimama kwa mfumo wa duara.
 
“Sawa”
“Tukumbuke, mwanachi asife katika hii kazi hapa anaye takiwa ni raisi Donald na mke wake. Tuhakikisheni kwamba tunawaleta eneo hili wakiwa hai na sote tulindane kwenye hii oparesheni”
Livna alizidi kusisitiza huku akitutizama kwenye nyuso zetu.
“Sawa mkuu”
“Jamani nashukuru kwa umoja wenu, hii kazi ni ya kuhatarisha maisha yetu. Na nyote mumefanya kwa ajili ya kunisaidia. Endapo hatuto rudi kwa idadi hii basi ninaimani kwamba tutaonana kwenye dunia nyingine ambayo hakuna mtu aliye wahi kwenda”
Nilizungumza kwa sauti ya upole kwani kusema kweli katika hili swala laiti ningekuwa peke yangu basi siwezi kabisa kufanya hivyo.
 
“Usijali ninaimani sote tutarudi salama, na hakuna hata kati yetu atakaye kufa. Twendeni tukawatandike makalio yao sawa”
Livna alizungumza kwa msitizo ambao unampa hamasa kila mmoja eneo hili.
“Sawa mkuu”
Tukapeana mikono kisha sote tukaaanza kutoka sebleni hapa, kila mmoja akiwa na silaha za kutosha, na kila mtu anajua ni wapi ameingiza silaha hizo. Tukaingia kwenye magari manne yanayo tumiwa na walinzi wa Kimarekani ambayo yamekuja na wasichana wa Livna.
Safari ikaanza taratibu, tulipo fika barabarani gari zikatawanyika na kila gari likapita njia yake ila lengo kubwa ni kufika Kigamboni. Simu ya Livna ikaanza kuita mfukoni mwake, taratibu akaitoa na kuipokea.
 
“Muheshimiwa raisi”
Nikamtazama Livna huku nikiendelea kuendesha gari.
“Ziara imebadilishwa?”
Nikajikuta nikupunguza kasi ya mwendo wa gari.
“Ahaaa inaanzia hapo SPF Tower?”
“Sawa mkuu basi nitaimarisha ulinzi hapo”
Livna akakata simu yake na tukaanza kupeana taarifa watu wote juu ya ziara ya maraisi hawa kubalishwa. Ikatulazimu wote mpango kubadilika haraka inavyo wezekana. Mimi na Livna tukawa wa kwanza kufika katika magorofa haya mawili ambayo ni marefu sana kwenda juu na urefu wake ni sawa na mita 147  kwenda juu.
 
“Sijui wanafika saa ngapi hapa”
Nilizungumza huku nikiendelea kutazama ulinzi ulio imarishwa hapa. Hapakuwa na mtu wa kutukagua kwa maana tunavitambulisho.
“Watafika, siwezi kumpigia K2 simu na kumuuliza inaweza kumpa wasiwasi.”
“K2 alisha wahi kufahamu mahusiano kati yangu mimi na wewe?”
“Hapana hakuwah kufahamu”
“Ahaa sawa sawa”
 
“Tuelekee juu, kwa maana huku ndipo wanapo kagua kagua”
“Wanaanza gorofa gani kwa maana yapo haya mawili hapa?”
“Hili tulilopo ndio wanaanza”
“Babyanka na timu yako hakikisheni munakaa gorofa namba mbili.”
“Sawa”
Baada ya kutoa maelekezo hayo kupitia kinasa sauti maalimu nilicho kivaa, tukaanza kuingia ndani ya hili gorofa ambapo ndio mara yangu ya kwanza kuingia humu ndani. Baada ya lisaa ving’ora vikaanza kusikika, nikasimama kwenye moja ya dirisha na kuchungulia chini nikaanza kuona gari za raisi K2 zikifika katika hili eneo, walinzi wakazidi kuimarisha ulinzi.
“Jaribu kuizuia asira yako utakapo muona K2, tunaye muhiraji leo ni Donald na Hawa sawa Dany”
 
“Nimkuelewa”
Baada ya dakika tano mbeleni gari za raisi wa Marekani nazo zikafika katika eneo hili. Walinzi wote wa Marekani nao wakasogelea gari hili ambalo ni refu, wakamfungulia raisi mlango akashuka huku akipunga mkono. Taratibu nikaona gauni jekundu likianza kutoka ndani ya gari hili, kisha akashuka Hawa huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake, macho yangu nikayashusha hadi tumboni mwake nikaona ujauzito wake ulio nifanya nipatwe na uchungu mwingi sana hadi nikatamani kuanza kufanya mashambulizi nikiwa huku huku juu nilipo.
 
AISIIIII……….U KILL ME 169

“Dany tutafeli, unamuonaje malaya tu huyo na unakuwa na hasira kiasi hichi?”
Livna alizungumza huku akitazama mikono yangu jinsi inavyo tetemeka kwa hasira ambayo kusema kweli haina kipimo.
 
“Nahitaji kuwaua sasa hivi?”
“Piga picha ukiwaua sasa hivi kuna midomo mingapi ya bunduki kwa hawa watu na unahisi mwili wako unaonekana vipi. Utafanywa chujio kwa risasi acha ujinga”
Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo hukua kinishika mkono wangu wa kulia ambao unazidi kutetemeka kwa hasira kali niliyo nayo.
“Tulia nitakuonyesha hii kazi jinsi inavyo fanywa”
“Sawa”
Tukaanza kutembea tembea kwenye gorofa tuliyopo huku tukiendelea kujifanya ni walinzi wanao imarisha ulinzi ila hatuna chochote katika hili.
 
“Hivi unahisi ni kwa nini niliamua kutembea na wewe?”   
“Sijakuelewa?”
“Yaani unatambua kwa nini nimeamua kuongozana nawe kwenye hii oparesheni hii?”
“Sijajua?”
“Kwa sasabu ninakujua vizuri Dany, unafeli kila misheni kwa ajili ya hasira za hapo kwa hapo, ukimuona adui sijui unakuwaje kuwaje. Na isitoshe humu ndani kuna watu wana ujuzi hadi wakuwasoma watu miguu yao jinsi  inavyo tembea wakikuona tembea yako haieleweki lazima wakudandie, sasa piga picha wakikustukizia na jinsi unavyo tafutwa watakufanya nini”
 
Livna alizungumza kwa sauti ya chini, tukasimama pembeni ya lifti inayo fika katika gorofa hili, wakaanza kutoka walinzi kisha akafwatia K2, alipo muona Livna akamkonyeza kama ishara ya urafiki. K2 na walinzi wake wakelea kwenye moja ya sehemu maalumu iliyo andaliwa humu ndani na hapa ndipo maraisi watakapo kutana ili kuanza kukagua gorofa hili lenye huduma mbalimbali.
Waandishi wa habari nao wakazidi kuwa bize kuhakikisha kwamba wanapata picha nzuri kwa raisi ajaye kupitia lifti hii. Tukiwa hapa gafla umeme ukakatika na giza totoro likatawala humu ndani, kelele zikaanza kutawala huku walinzi wakihakikisha kwamba wanamlinda K2 kwani kukatika kwa umeme hili jambo halikuwepo kwenye ratiba yao.
 
“Show time baby”
Livna alizungumza huku akinishika mkono, tutakasimama kwenye lifti hii na kwa haraka Livna akaanza kuifungua milango hii miwili, ambayo haikumpa tabu sana. Mara kwa mara macho yangu yanatazama sehemua lipo kuwa K2 ila kutokana na giza pamoja na wingi wa watu sikuweza kumuona.
“Tunashuka chini unaone lifti ile kule”
Livna alizungumza kwa nguvu huku akinionyesha lifti  iliyo kwama kwa mwanga wa simu yake nikaweza kuiona na lifti hii ndipo alipo raisi Donald pamoja mke wake pamoja na walinzi.
“Ile ni gorofa namba mbili  inabidi kushuka kwa hii kambi”
“Nimekupata”
Akaanza Livna kushuka kwa kasi na hii kamba ngum ili tengenezwa kwa nyanya ndogo dongo za chuma na zimaesukwa sehemu moja na kuifanya kama hii kuwa nene na ngumu sana.
 
Nikachomoa bastola zangu mbili na kuzifanya kama vishikizo katika kamba hii kwani nikishuka chini kwa kutumia viganja vyangu pekee, nikifika hadi lifi ilipo ni lazima viwe vimechubuka. Nikashuka kwa kasi sana hadi nikafika sehemu ilipo lifti.
Tukaanza kusaidiana na Livna katika kufungua mfuniko ulipo juu  ya lifti. Tulipo hakikisha  kwamba umefunguka Livna akamulika ndani na simu yake.
“Muheshimiwa raisi tupo kwa ajli ya kukutoa hapa salama wewe na mke wako”
Livna alizungumza, nikapata nafasi ya kuchungulia ndani, nikawaona walinzi wa raisi Donald wakiwa wamezielekezea bunduki zao kwa Livna.
 
“Sawa”
Livna akaingia kupitia uwazi huo, na mimi nikaingia pia kupitia katika uwazi huu. Cha kushangaza sijamkuta Hawa ila sikuhitaji kuonyesha tofati yoyote katika hili.
“Hii ni gorofa namba mbili, tusaidiane kufungua huo mlango na tumtoe raisi humu ndani”
Livna akawapa maelekezo vijana wa raisi Donald Bush.
“Sawa madam”
Tukaanza kusaidiana kufungua mlango hadi ukafanikiwa kufunguka, tukakuta lifti hii ipo katika usawa wa gorofa ya pili na ya tatu huku kukiwa na uwazi mdogo wa kupita katika  gorofa namba mbili kwani ndio ilikuwa inapanda kwenda juu.
“Unaweza kupita hapo muheshimiwa?”
 
“Ndio”
Wakaanza kupita walinzi baadhi, nikafwatia na mimi, kisha akafwatia raisi Donald, Livna na walinzi wengie wawili wa mwisho. Sote humu tunategemea mwanaga wa tochi wa simu ya Livna. Tukaanza kukimbia kwa haraka kwenye kordo hii kubwa huku kando kando  kukiwa na maduka makubwa ya simu ambayo sihitaji kuyatilia maanani.
“Mke wangu alielekea bafuni kidogo”
“Usijali muheshimiwa raisi tutampata tu. Yanka umesikia hiyo”
“Ndio”
Tuliisikia sauti ya Babyanka kupitia vinasa sauti ambavyo katika watu tulipo hapa tumevaa mimi na Livna tu na hata hawa walinzi wake wamevaa vinasa sauti vyao wanavyo wasiliana na wa watu wao. Tukaanza kushuka ngazi kuelekea chini huku raisi Donald Bush tukiwa tumemuweka katikati.
 
“Winy gari ziandaliwe kwneye magesho ya chini kabisa”
“Sawa”
“Raisi anaondoka na msafara mwingine?”
Mlinzi  mmoja wa raisi aliuliza huku  tukiendelea kushuka kwneye gorofa hii kwa kasi.
“Ndio, akiondoka na usafiri wake shambulizi lilizo pangwa kufanywa hapa ni lazima atashambuliwa kwenye gari”
“U…ume….sema shambulizi binti?”
Raisi Donald Bush aliuliza huku akihema sana kwani kasi tunayo mpeleka unaweza kuifananisha na wana riadha.
“Ndio muheshimiwa raisi”
“Nani huyo anaye hitaji kufanya shambulizi?”
“Ni Dany muheshimiwa”
 
“DANY…….Mwanaharamu mkubwaa, nitoeni hapa jamani akinikamata ataniua huyu”
“Usijali muheshimiwa upo salama, nitakulinda hadi dakika ya mwisho wa maisha yangu”
“Mke wangu, mke wangu jamani muokoeni”
“Yanka umefanikiwa kumpata mke wa raisi Donald?”
“Ndio tunaeleka naye kwenye maegesho ya magari”
“Muheshimiwa raisi mke wako utamkuta kwenye meegesho ya magari”
“Ila nyinyi ni kina nani, kwa maana mazungumzo yenu munayafanya nyinyi wenyewe?”
Mlinzi mwengine aliuliza 
 
“Sisi ni kikosi maalumu cha dharura alicho kiunda raisi K2”
“Ataunda vipi kikosi maalumu pasipo kushirikisha ofisi yetu?”
“Sisi ndio watu wa pekee tunayo ijua hii nchi, isitoshe muheshimiwa raisi amekuja kipindi ambacho nchi inamtafuta gaidi anaye itwa Dany, ninaimani unamfahamu na kama haumfahamu basi utakuwa umemsikia”
Livna aliendelea kujibu maswali ya hawa walinzi wa karibu wa raisi kiufasaha na laiti kama wangejua Dany mwenyewe nipo karibu yao wala wasinge dhubutu kabisa kunyanyua miguu yao.
“Tunahitaji kudhibitishiwa hilo na muheshimiwa raisi K2”
“Acheni ujinga nyinyi, tupo kwneye hatari nyinyi munataka kudhibitishiwa ili iweje, mule ndani ya lifti si mulikuwa mumechanganyikiwa na mukakosa la kufanya hadi huyu binti  akafika, eheeeeee?”
Raisi Donald Bush  aliuliza kwa kufoka huku akihema sana.
“Ila muheshimiwa raisi ni jukumu letu kukulinda kwa maisha yetu yote”
 
“Mimi ndio raisi wa Mareknani ninaye kupa amri wewe. Msikilizeni huyu binti  anacho kisema kuazia hivi sasa, nina imani kwamba nyote hakuna anye mjua Dany zaidi yagu, na kifupi Dany ni yule aliye isambaratisha kambi ya Al-Shabab, sasa piga picha akikutana na sisi sasa hivi nani atakate pona eheee?”
“Samahani mueshimiwa raisi”
Mlinzi huyu ikambidi kukaa kimya tu kwani ndio hivyo raisi amesha zungumza na ahitaji maoni mengine yoyote kusikia. Tukafika katika mlango wa kutokea nje, wote tukajibanza huku tukitazama nje, nikaona gari mbili tulizo kuja nazo zikiwa kwenye eneo la maegesho.
“Jamani tunatakiwa kuwa makini, hapa ni sehemu ya maegesho hatujui adui yupo wapi, kwa hiyo tunatakiwa kuwa makini sana”
“Sawa”
 
Baada ya Livna kuzungumza hivyo tukaanza kutoka katika eneo hili kuelekea lilipo gari, tukaanza kusikia kishindo cha kwanza cha mmoja wa walinzi wa raisi akianguka chini. Sote tukajibanza kwenye moja ya gari.
“N..nini jamani?”
“Shiiiiii…….”
Livna alimnyamazisha raisi kwani tayari woga umesham mtawala, hata mimi mwenyewe sijui ni kitu gani kinacho endelea. Hatukaa sawa mlinzi mwengine akaanguka chini huku  akitoa ukeleke. Nikataka kushambulia sehemu nilipo muona.
“Dany ni sisi tunakuona tumevaa night vision glass”
Niliisikia sauti ya Winy akizungumza jambo lililo nifanya niwe mpole na kuishusha bastola yangu chini. Kwani huu ni mpango ambao ninaimani Livna ameupanga ili kuwapagawisha raisi Donal Bush. 
“Hei, mumemuona mshambuliaji?”
Mmoja wa walinzi  alizungumza.
 
“Yaa yupo eneo lile”   
Kitendi cha mlinzi hutu kuzungumza hivyo akapigwa risasi ya kichwa na kuangukia miguuni mwa raisi.
“Yesu wangu…….!!”
Raisi Donald alizungumza kwa woga mwingi sana na ubaya wa washambuliaji wa hawa walinzi wamevaa miwani maalumu ambazo zinawafanya waone vizuri kwenye giza totoro. Walinzi walio salia wa raisi Donald wakaanza kuitoa kimaso maso ili kumzuia mshambuliaji. Mimi na Livna tukamshika raisi mikono yake na kuanza kukimbia huku tukiwa tumeinama, kitendo hicho kikawafanya walinzi wa raisi Donald wote kufa kwani tunamfanya Winy kuweza kuwadungua vizuri na bunduki yake haitoi mlio kwani ameifunga kiwambo cha kuzuia risasi hizo. Tukafanikiwa kufika kwenye gari tulilo waambia Winy na timu yake waliandae.
“Tuondoke tuondoke”
Linvna alizungumza na Martin akaliweka sawa gari hili na kuanza kuondoka kwa kasi eneo hili la chini.
 
“Mke wangu jamani?”
“Yupo gari la nyuma muheshimiwa”
Msichana mmoja wa Livna alimujibu raisi Donald aliye ishusha pumzi yake taratibu. Moyoni mwangu nikajikuta nikijawa na furaha kubwa sana ya kushangilia ushindi nilio upata kwa kusaidiwa na hawa wezangu.
“Muheshimiwa ni kitu gani mwilini mwako kinaruhusu satelaiti kukuona”
Livna alizungumza huku akiwa amemtazama raisi.
“Ni…..nina kimoja hapa mkononi”
Raisi Donald alizungumza huku akitetemeka sana. Kwa haraka Livna akaanza kukivua raisi Donald koti lake la suti kisha akakunja mkono wa shati lake hili jeupe.
“Naombeni kisu”
“Unataka kufanyaje!!?”
Raisi Donald alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka kwa woga.
 
“Tunahitaji kukitoa hicho kifaa ni lazima Dany na timu yake watakufwata popote uendapo na ukumbuke upo Tanzania na si Marekani na yeye anaijua Tanzania vizuri kuliko unavyo fikiria”
“Sa..a…wa”
Livna akachukau kisu alicho kabidhiwa na mtu wake ambacho kina incha kali sana, pasipo uruma wala wasiwasi akaanza kupasua sehemu raisi Donald aliyo sema. Taratibu akatoa kidude kidogo sana, kilicho akafungua kioo cha gari na kukitupa.
“Una kingine ndani ya mwili wako?”
“Sina labda kiatu cha mguu wa kushoto”
Livna kwa haraa akamvua raisi kiatu hichi cha garama, akakitazama tazama kwa haraka kisha akaanza kuigandua kikanyagio cha soli kwa kutumia kisu hichi, alipo fanikiwa kukifunua, tukaona kifaa kingine kidogo kinacho wawezesha walinzi wa raisi hata wakiwa nchini Marekani kujua kwamba raisi wao yupo eneo gani. Livna akakitupa kifaa hichi na kumrudishia raisi Donald kiatu  chake huku kikiwa hakina kikanyagio cha soli.
“Una kingine?”
“Saa hii”
Raisi Donald akaivua saa yake akamkabidhi raisi.
“Huna kingine?”
“Hapana”
“Mke wako anacho?”
“Ahaa, mkufu alio uvaa”
“Yanka mvueni mke wa raisi mkufu wake na muutupe”
“Poa dakika sifuri”
 
“Ni wa garama sana, dola laki mbili?”
“Una garama kubwa kuliko maisha yako?”
Livna alizungumza kwa msisitizo hukua kimtazama raisi Donald Bush usoni mwake.
“Hapana”
“Acha utupwe na hii saa yako ya garama nayo ninaitupa”
Livna akafungua kioo kidogo na kuvitupa vitu hivi.
“Tunafanya hivi vyote ni kwa ajili yako la sivyo Dany atatuweka kati na akifanikiwa kufanya hivyo, muheshimiwa mziki wake hata mimi ninaujua”
Livn alizidi kuzungumza maneno ya kumtisha raisi Donald Bush juu yangu.
“Tunaelekea wapi?”
“Kwenye nyumba salama kwa muda, na baada ya hapo utaratibu mwengine utafwata”
Uzuri wa gari hizi zina ving’ora vinavyo fanya magari mengine barabarani kupisha njia, jambo linalo warahisishia madereva wetu kuzidi kutoroka. Tukiwa barabarani gafla gari moja jeusi linalo fanana na gari hili likaingia mbele yetu na kuongeza mwendo.
 
“Mkuu ni sisi”
“Sawa”
“Ni kina nani wale?”
“Ni kikosi kinazidi kuimarisha ulinzi”
“Ohooo asante Mungu wangu”
Raisi Donald alizungumza hukua kipiga ishara ya msalaba kwa ajili ya kumshukuru Mungu wake. Gari zote nne zikangia kwenye geti kubwa la jumba la Winy. Tukashuka kwenye magari na kwa haraka raisi Donald Bush na Hawa wakaingizwa ndani ya nyumba hii.
“D”
Livna aliniita baada ya kuniona nimeichoma bastola yangu kwa ajili ya kueekea ndani kuwamaliza maadui zangu. Nikasimama huku nikimtazama usoni mwake, akanisogelea karibu yangu na kunitazama kwa macho makali.
“Akilii, akilii ndio inahitaji usikurupuke, na kama kuwaua utawaua, ila tafuta kitu cha thamani kwao kwanza ndio uwaue”
 
“Sijakuelewa”
“Nenda ndani utaelekewa”
Baada ya Livna kuzungumza maneno hayo, akaondoka na kuanza kuwapa majukumu wasichana wake kuimarisha ulinzi wa hili eneo hili. Nikaanza kutembea kwa haraka huku nikifikiria jambo alilo niambia Livna, nikawakuta raisi Donald Bush na Hawa wakiwa wamekaa sebleni huku Babyanka na Win wakiwa wamewaandalia maji ili kusuuza makoo yao. Raisi Donald taratibu akamsogeza Hawa karibu yake na kumlaza begani mwake.
“Vipi hujapata mstuko wowote tumboni mwako?”
Raisi Donald alizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa mahaba mengi ndani yake.
 
“Hapana mume wangu, ni mstuko tuu, ila nipo sawa”
Nikachukua kiti kimoja na kukiweka mbele ya raisi Donald Bush pamoja na Hawa, taratibu nikaka huku bastoka nikiwa nimeishika vizuri. Nikawatazama kwa dakika kadhaa hadi wao wenyewe wakawa wananishangaa.
“Kijana mbona unatushangaa?”
Raisi Donald Bush alizungumza huku akiupeleka mkono wake wa kulia kwenye tumbo la Hawa na kuanza kulipapasa taratibu taratibu. Nikafungua kifungo cha shati langu, taratibu nikaiinamisha sura yangu chini, nikaanza kuvua sura hii ya bandia hadi ninaimalizia na kuinyanyua sura yangu na kuwatazama raisi Donald na Hawa, wote wakabaki wamenitumbulia macho hata mkao  wa kimahaba walio ukaa ukavurugika kila mtu akakaa jinsi anavyo jua yeye mwenyewe huku mwili wake ukiwa unawatetemeka, kwani yule wanaye muogopa na waliye mkimbia huko walipo toka yupo mbele yao. 
 
ITAENDELEA
“Haya sasa ule msemo wa USIYE MPENDA AMEKUJA, ndio ulio wakuta raisi Donald na Hawa. Dany yupo mbele yao unahisi ni nini kitakacho tokea na kuendelea katika story hii ya kusisimua?. Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )