Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 10, 2018

Tazama Hapa Kilichoendelea Mahakamani Kesi ya Amber Rutty na Mpenzi Wake

juu
Msanii Nascat Abubakar ‘Amber Rutty’ na mpenzi wake Said Mtopari, wamefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo, Desemba 10, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi yao.

Amber Rutty na Said Mtopari walifika mahakamani hapo wakiwa na Mchungaji Daudi Mashimo ambaye aliwawekea dhamana pamoja na mshtakiwa wa tatu, James Delicious.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka manne, ambapo shtaka la kwanza, Amber Rutty, anadaiwa kutenda kosa la kumruhusu Said Mtopali kumuingilia kinyume na maumbile Oktoba 25, 2018 , kosa ambalo amelikana. Katika shtaka hilo pia Mtopali anadaiwa kati ama baada ya Oktoba 25, 2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile.

James Charles naye anakabiliwa na kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018, James alisambaza video za ngono kupitia makundi ya WhatsApp.

Kosa la nne ni la kusababisha kusambaa kwa picha za ngono linalomkabili Amber Rutty na Mtopali, ambapo inadaiwa kati ya Oktoba 25, 2018 walisambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp, jambo ambalo wamelikana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi January 10, 2019 itakapokuja kutajwa tena kutokana na upande wa mashtaka kutokamilisha upelelezi.
chn
ap
Loading...
ad

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )