Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 25, 2019

Aliyekuwa Kamishna Mkuu TRA Kitilya na wenzake kusomewa maelezo ya mashahidi Feb.8

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Februari 8, mwaka huu kuwasomea maelezo ya mashahidi (commital) aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na mwenzake wawili wanaokabiliwa na mashtaka 58 yakiwemo ya utakatishaji fedha.
 
Hatua hiyo imefikiwa baada ya jana upande wa utetezi kueleza hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi kupinga maombi ya upande wa mashtaka ya kutaka kesi hiyo ihairishwe kwa siku 14 wakieleza kuwa wapo katika hatua za mwisho za kufaili taarifa hivyo wanaomba siku hizo kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo.
 
Upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Masumbuko Lamwai ulidai, kuwa washtakiwa hao wamekaa ndani kwa miaka mitatu, kisha kesi hiyo ikafutwa kiujanja ujanja na kuileta tena hivyo wanashangaa ni kitu gani kinakwamisha watu hao wasisomewe maelezo ya mashahidi.
 
“Watu hawa wameshakaa ndani miaka mitatu sasa, walifutiwa kesi kiujanja na kuleta tena kesi hii ili wakae tena ndani, hivi ni kitu gani kinazuia commital (maelezo ya mashahidi), alidai na kuongeza kuwa ...Wiki iliyopita walisema leo (Jana) watawasomea na sasa wanasema wapo kwenye hatua za mwisho watueleze hiyo hatua,”.
 
Awali Wakili wa TAKUKURU Leonard Swai alidai, kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa wanaomba tarehe nyingine ili wakamilishe zoezi la kuwasilisha taarifa kwani wapo katika hatua za mwisho.
 
Mbali na Kitilya washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, Kamishna wa Sera ya uchambuzi wa Madeni kutoka Wizara Fedha na Mipango, Bedason Shallanda na Msaidizi wake Alfred Misana.
 
Katika mashtaka hayo washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kughushi, moja la kuongoza uhalifu, 49 utakatishaji fedha, mawili ya kutoa nyaraka za uongo, kujipatia fedha kwa njia ya udanyanyifu moja na shtaka moja la kutoa nyaraka kwa nia ya kumdanganya kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango.
 
Wanadaiwa kati ya Machi 15, mwaka 2013 na Januari 10, mwaka 2014 ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya washtakiwa wote walijipatia Dola za Kimarekani Milioni sita wakionesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa kupitia Kampuni ya Egma T Ltd.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )